BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete licha ya shughuli zake kubwa za kitaifa kama Naibu Waziri lakini kamwe hasahau Jimbo lake na amekuwa mstari wa mbele kila siku kusukuma na kuchochea shughuli za maendeleo Jimboni.
Katika kuhakikisha wananchi wa Chalinze wanapata huduma na kupata maendeleo zaidi, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshusha Wadau wa Taasisi ya Korea iitwayo Kofih Tanzania ili kushiriki shughuli za maendeleo Jimboni.
Na Jana Ijumaa, Mhe. Kikwete amekuwa na mkutano mzuri na Taasisi hiyo ya Wakorea iitwayo Kofih Tanzania ambapo wamekubaliana ushirikiano kwa miaka 5 utakaowezesha kuimarishwa kwa miundombinu ya afya hasa hospitali ya wilaya ya Chalinze, vituo vya afya na kuwezesha vifaa tiba katika eneo la wakina mama na watoto, na mahitaji ya vifaa vya huduma za dharura na kuwezesha watendaji wa sekta mafunzo ya ujuzi wa juu katika Halmashauri ya Chalinze.
#KaziInaendelea