MUSSA ALLAN
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 18,925
- 13,280
Seif al Islam. ...
Ambulence anazozitoa huwa hazidumu. Zinakuwa za kuchukulia ujiko kwenye media halafu baada ya miezi 3 hazionekani. Zilishakuwepo ambulence zaidi ya nne baada ya kufariki Bwana Mdogo. Moja ni Mazda, nyingine ni Mkonga nyingine ya kichina sijui inaitwaje... Na zote hivi sasa hazipo.
Ukibahatisha ndani ya miezi mitatu hii ya kupigia picha ukawa na hitaji la kumpeleka mgonjwa tumbi utaambiwa changia wese laki 2, mara tusaidie kuazima tairi kwa mtu mradi mgonjwa wako afe tu
bavicha huu wimbo wa riz sijui tajiri sijui nani kawafundisha,,masikini wanywa viroba wakishakariri kitu NI TABU...........ha ha ha ha,HAMY-D katika ubora wake......tunashukuru mkuu kwa post yako, ila muulize Riz hii Ambulance kweli inalingana na hela alizotupiga katika miaka kumi ya uongozi wa baba yake?
si mlisema tusubiri babake aachie urais?,kumbe tena mpaka aachie na umwenyekiti?,Ngoja baba yake aachie kiti cha chama tuone ...............!!
Kati ya Riz na Lowassa nani anatakiwa awe jela?!? Ni lini Riz ameingia serikalini kusimamia fedha za umma? Je hilo fisadi lenu Lowassa...si limetuibia kwa miaka zaidi ya 30...zee lilafi kweli lile.
WanaJF,
Moja ya vijana ambao taifa hili halina budi kuwatazama kwa jicho la tatu ni Ridhiwani Kikwete. Hii ni kwa kuwa ni kijana ambae yupo kwenye fungu la vijana 'asset' wa hii nchi na sio 'liability'.
Katika hatua ya kutimiza ahadi zake kwa wananchi wake wa jimboni Chalinze, Ridhiwani akabidhi ambulance ambayo ameahidi wakati wa kampeni kwenye hospital ya Chalinze siku ya jana.
Ahadi hii imetekelezwa kufuatia makabidhiano ya kompyuta katika shule takribani tano ambazo nazo zinapatikana katika jimbo lake hilo la Chalinze.
Aidha, mbunge huyo kijana alipohojiwa juu ya uwezo wake wa kutekeleza ahadi zake kwa kasi alieleza ripota wetu kuwa, yeye hawezi kungoja pesa za mfuko wa jimbo ili kufanya maendeleo kwa wananchi wake badala yake atajitahidi kutumia hata vyanzo vyake vya ziada ikiwemo pesa za tozo za uwakili na mapato yatokanayo na kodi ya nyumba yake ili kusukuma maendeleo jimboni kwake Chalinze.
Ndugu wanaJF, hii ndio aina ya vijana ambao hili taifa linahitaji. Sio wale wanywa viroba watembea na majeneza kutwa kucha huku wamama wajawazito wanakosa huduma bora za afya na mbunge amekazania tu, "eti mbunge sio kazi yangu kuboresha huduma ya afya, hiyo ni kazi ya serikali". Mawazo hayo yamepitwa na wakati na ndio yamefanya wakina Kafulila, Wenje, Mkosamali na yule Kiwia kupigwa chini vibaya na wananchi wao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Tumuunge mkono Ridhiwani.
View attachment 308505
bado tunakwenda hata kwa wasambaza maugali - sijui kama ataponamo.Kachelewa sana. Waulize akina Dogo Janja wa Arumerumeru japo hajihusishi na maugali lakini alitoa mapema siku nyingi tu