WanaJF,
Moja ya vijana ambao taifa hili halina budi kuwatazama kwa jicho la tatu ni Ridhiwani Kikwete. Hii ni kwa kuwa ni kijana ambae yupo kwenye fungu la vijana 'asset' wa hii nchi na sio 'liability'.
Katika hatua ya kutimiza ahadi zake kwa wananchi wake wa jimboni Chalinze, Ridhiwani akabidhi ambulance ambayo ameahidi wakati wa kampeni kwenye hospital ya Chalinze siku ya jana.
Ahadi hii imetekelezwa kufuatia makabidhiano ya kompyuta katika shule takribani tano ambazo nazo zinapatikana katika jimbo lake hilo la Chalinze.
Aidha, mbunge huyo kijana alipohojiwa juu ya uwezo wake wa kutekeleza ahadi zake kwa kasi alieleza ripota wetu kuwa, yeye hawezi kungoja pesa za mfuko wa jimbo ili kufanya maendeleo kwa wananchi wake badala yake atajitahidi kutumia hata vyanzo vyake vya ziada ikiwemo pesa za tozo za uwakili na mapato yatokanayo na kodi ya nyumba yake ili kusukuma maendeleo jimboni kwake Chalinze.
Ndugu wanaJF, hii ndio aina ya vijana ambao hili taifa linahitaji. Sio wale wanywa viroba watembea na majeneza kutwa kucha huku wamama wajawazito wanakosa huduma bora za afya na mbunge amekazania tu, "eti mbunge sio kazi yangu kuboresha huduma ya afya, hiyo ni kazi ya serikali". Mawazo hayo yamepitwa na wakati na ndio yamefanya wakina Kafulila, Wenje, Mkosamali na yule Kiwia kupigwa chini vibaya na wananchi wao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Tumuunge mkono Ridhiwani.