Ridhiwani akabidhi Ambulance Jimboni

Ridhiwani akabidhi Ambulance Jimboni

WanaJF,

Moja ya vijana ambao taifa hili halina budi kuwatazama kwa jicho la tatu ni Ridhiwani Kikwete. Hii ni kwa kuwa ni kijana ambae yupo kwenye fungu la vijana 'asset' wa hii nchi na sio 'liability'.

Katika hatua ya kutimiza ahadi zake kwa wananchi wake wa jimboni Chalinze, Ridhiwani akabidhi ambulance ambayo ameahidi wakati wa kampeni kwenye hospital ya Chalinze siku ya jana.

Ahadi hii imetekelezwa kufuatia makabidhiano ya kompyuta katika shule takribani tano ambazo nazo zinapatikana katika jimbo lake hilo la Chalinze.

Aidha, mbunge huyo kijana alipohojiwa juu ya uwezo wake wa kutekeleza ahadi zake kwa kasi alieleza ripota wetu kuwa, yeye hawezi kungoja pesa za mfuko wa jimbo ili kufanya maendeleo kwa wananchi wake badala yake atajitahidi kutumia hata vyanzo vyake vya ziada ikiwemo pesa za tozo za uwakili na mapato yatokanayo na kodi ya nyumba yake ili kusukuma maendeleo jimboni kwake Chalinze.

Ndugu wanaJF, hii ndio aina ya vijana ambao hili taifa linahitaji. Sio wale wanywa viroba watembea na majeneza kutwa kucha huku wamama wajawazito wanakosa huduma bora za afya na mbunge amekazania tu, "eti mbunge sio kazi yangu kuboresha huduma ya afya, hiyo ni kazi ya serikali". Mawazo hayo yamepitwa na wakati na ndio yamefanya wakina Kafulila, Wenje, Mkosamali na yule Kiwia kupigwa chini vibaya na wananchi wao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Tumuunge mkono Ridhiwani.

attachment.php
hIVI HII KASI YA RIZIWANI NA MANGUFULI ZINAKWENDA SAMBAMBA??
KAMA NI HIVYO KWA RIZ HAJAUNGA MKONO KAZI YA MANGFULI???
 
ImageUploadedByJamiiForums1448968119.772154.jpg
Hii gari mnaielewa jamani maana ni kama mdoli ivi hata likiaharibila spare unapata wapi. Angeleta mkonge ningemuelewa hapo chezo tu hakuna kitu
 
..kijana ambae kabla baba yake hajawa rais hakuwa na mali nyingi...leo ndie huyu anegawa ambulance jimboni...lazima vyanzo vyake vya mapato tuvijue....kama watanzania tungejua vyanzo halisi vya mapato ya hawa wanasiasa sidhani kama kungekua na kelele nyingi humu...
 
HAMY-D hii gari iko Canada au Canada ndiyo wametoa msaada?
 
Last edited by a moderator:
Hamy D...yawezekana huu ndo mwisho wa akili yako ulipofkia any way kila mtu na akili yake...nmekupuuza...tuone kama atakuwepo kwenye baraza la mawazirii..lijalo
 
Magufuli anamtamani huyo amrukie, yupo kwenye list yake ya wakwepa kodi.
 
Amefanya vema, kuna Watanzaia wengi hata wasio uza madawa ya kulevya walishaanza kuwasaidia wananchi kwa kutumia vipato halali.
 
uliza mbowe alifanya hivyo hivyo mbona hukuuliza

Ulivyojibu umeonyesha upeo wako ulivyo mwenzako a;ekuuliza ni halali kwa mbunge kutoa pesa yake kwaajili ya maendeleo?haja mtaja Riz wala bowe
 
Kwani inauzwa kiasi gani ili tujue ni kweli ni hela zake halali au ni ufisadi
 
hawa wabunge bwana! hatutaki watu wazoeshwe kupewa samaki, tunahitaji wafundishwe kuvua samaki. mfano mmoja ni mbunge wa Bukoba Mjini, alizoea kuwapa pesa watu, na ambulance juu. Baada ya kupigwa chini akachukua ambulance yake. Sasa huyu alikuwa co-joint na HSC, wakwepa kodi wakuu, sasa anajifanya kuwapoza wananchi. hii haifai.
 
Kati ya Riz na Lowassa nani anatakiwa awe jela?!? Ni lini Riz ameingia serikalini kusimamia fedha za umma? Je hilo fisadi lenu Lowassa...si limetuibia kwa miaka zaidi ya 30...zee lilafi kweli lile.

Usitake kumuingiza lowassa kwa kutaka kumsafisha huyu dogo,
 
Back
Top Bottom