Ridhiwani akabidhi Ambulance Jimboni

Ridhiwani akabidhi Ambulance Jimboni

Gia ya kukwepa kutumbuliwa majipu.............. atatumbuliwa tuuuuu! maadam majipu anayo... ha ha haaa hadi rahaaaa
 
Taifa halihitaji vijana wezi kama huyu.Ovyooo.Subiri tunamjia.
WanaJF,

Moja ya vijana ambao taifa hili halina budi kuwatazama kwa jicho la tatu ni Ridhiwani Kikwete. Hii ni kwa kuwa ni kijana ambae yupo kwenye fungu la vijana 'asset' wa hii nchi na sio 'liability'.

Katika hatua ya kutimiza ahadi zake kwa wananchi wake wa jimboni Chalinze, Ridhiwani akabidhi ambulance ambayo ameahidi wakati wa kampeni kwenye hospital ya Chalinze siku ya jana.

Ahadi hii imetekelezwa kufuatia makabidhiano ya kompyuta katika shule takribani tano ambazo nazo zinapatikana katika jimbo lake hilo la Chalinze.

Aidha, mbunge huyo kijana alipohojiwa juu ya uwezo wake wa kutekeleza ahadi zake kwa kasi alieleza ripota wetu kuwa, yeye hawezi kungoja pesa za mfuko wa jimbo ili kufanya maendeleo kwa wananchi wake badala yake atajitahidi kutumia hata vyanzo vyake vya ziada ikiwemo pesa za tozo za uwakili na mapato yatokanayo na kodi ya nyumba yake ili kusukuma maendeleo jimboni kwake Chalinze.

Ndugu wanaJF, hii ndio aina ya vijana ambao hili taifa linahitaji. Sio wale wanywa viroba watembea na majeneza kutwa kucha huku wamama wajawazito wanakosa huduma bora za afya na mbunge amekazania tu, "eti mbunge sio kazi yangu kuboresha huduma ya afya, hiyo ni kazi ya serikali". Mawazo hayo yamepitwa na wakati na ndio yamefanya wakina Kafulila, Wenje, Mkosamali na yule Kiwia kupigwa chini vibaya na wananchi wao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Tumuunge mkono Ridhiwani.

View attachment 308505
 
Mwenyewe anaona fahari tunavyomuogopa, najuta kuzaliwa kwenye nchi kama hii, unaibiwa alafu aliyekuibia anakuletea dharau, hizi ni dharau
Hiyo gar ampelekee baba yake,

Mkuu hii nchi ndipo ilipofikia mbaya zaidi hata walio soma wana shabikia upuuzi kama huu.Tz ukiwa masikini huna sifa ya kuwa kiongozi hadi uwe na kitu mkononi
 
Alikuwa wapi? Mleta mada , vp hujapewa kaposho ili ugeuze upepo wa UDA?
 
Riz labda asset huko Msoga huyu ni miongoni mwa watu wasiotakiwa?Juzi hili

Ikiwa CHADEMA walikuwa tayari kumpa Lowassa urais..basi hata shetani akitangaza nia ya urais CHADEMA hawana uhalali wa kumnyooshea kidole Shetani kuwa hafai. Maana yake Lowassa ni mchafu kuliko hata shetani mwenyewe.
 
Money laundering. A drop in the ocean.
Kwanza aeleze,at 28 ? amepata wapi mabilioni aliyo nayo? Kama si kuwafanya wapumbavu watu wanao 'sweat' kupata hela ya halali. Hii 'token bonhomie' does not wash!
 
Kuna watu akili zao zimejaa wadudu:what: Huyu katumwa kuleta habari za kusifiana hapa jf:what: eti ni asett:what: asett ya huko kwenu labda:what: na wakati mwingine usilete upuuzi humu😡
 
Huyu dogo nae jipu huyu. Atatumbuliwa tu. Tena litanuka sana hili maana usaha wake mhhh.
 
hiyo gari mbona kama ya msaada toka canada! maana ubavuni kuna bendera ya Canada.
 
Back
Top Bottom