Kwanza, kampuni iliyosajiliaw kwenye anuani iliyowekwa kwenye mkataba haihusiani na mambo ya nishati! Kabla ya kuingia kwenye mkataba huo kampuni ya RDC ilikuwa haijawahi kufanya ugavi wa umeme mahali popote!
pili,
maneno kuwa:
The supplier has the equipment, and the financial and technical capability to construct, install, commission, operate and maintain, such a a plant as required by TANESCO
yalikuwa hayana ukweli wowote. RDC haikuwa na uwezo, haikuwa na vifaa, na haikuwa na fedha za kuendesha mradi huo! Ni kwa sababu hiyo mabenki ya Marekani yalikataa kuwapa fedha kwani hawakuwa na Credit history ya kutosha kuomba mamilioni ya dola!
kwenye mkataba wenyewe, kipengele 15:14 ndicho kinaleta shida hasa baada ya kuruhusu mkataba "kuuzwa" kwa Dowans na hakuna anayesema uliuzwa kwa kiasi gani na kama kwa kufanya hivyo siyo kuvunja mkataba! Kipengele kinasema: (msisitizo wangu)
"This agreement is intended solely for the benefit of the Parties and nothing in this Agreement shall be CONSTRUED to create any duty to, standard of care with reference to, or any liability to, or confer any right of suit or action on any Person NOT a part to this Agreement other than to the extent it has been granted specific rights or benefits in the Agreement"
Kipengele hicho hakiachi nafasi kwa Dowans kununua mkataba huo kwani hakuna mahali popote ambapo aidha panaonesha kuwa RDC na Dowans ni kampuni zinazohusiana au mahali ambapo RDC ilikufa na nafasi yake kuchukuliwa na Dowans.
Kwa vile lugha ya sheria huwa inanisumbua, kipengele hiki kina maana gani:
15:16
No review and approval by TANESCO of any agreement, document, instrument or specification proposed by the Supplier (RDC) shall relieve the Supplier from any liabitity that it would otherise have had for its negligence in the preparation of such agreement, document, instrument or specification or failure to comply with the applicable Laws of Tanzania with respect thereto, or to satisfy the Supplier's obligations under this Agreemeent, nor shall TANESCO be liable to the Supplier or any other person by reason of its review, acquiescence or approval of an agreement, document, instrument or specification"
Kwa maneno mengine, endapo TANESCO baada ya kupitia nyaraka au hati mbalimbali baada ya kuingia mkataba huo na wakagundua kuwa RDC imefanya makosa ya aina fulani basi TANESCO isiishikilie RDC kwa makosa hayo. Na wao RDC wanaahidi vivyo hivyo. (apply that to selling the contract to Dowans!)
Sasa kipengele cha kushangaza zaidi ni masuala ya fedha. Wakati mwanzoni kabisa mkataba unasema kuwa:
The supplier has the equipment, and the financial and technical capability to construct, install, commission, operate and maintain, such a a plant as required by TANESCO
inakuwaje basi watake serikali ya Tanzania kuwadhamini ili wapate mkopo wa kufanyia biashara?
Haya nimewaanzia hapo...