Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Wizi huu unaendelea sababu muhusika mkuu ni Jakaya Kikwete.kama isingekua ya JK alipong'oka lowasa tu watu wangechukuliwa hatua za kisheria na wizi huu ungeisha.
 
Mkiniongezea wiki nyingine Mikataba yote ya madini na gesi inasitishwa rasmi na kufanyika upya.

Makampuni yote yaliyoingia mikataba yajitokeze kwanza ili tuijadili hiyo mikataba upya. Iwapo waliweka hiyo mikataba na wale mafisadi papa niliokwisha wanyonga wiki iliyopita, basi mikataba yao inakufa kifo chema. Wanaanza upya wakitaka. Hii itachukua muda, labda mniongezee wiki nyingine tena ili nikamilishe kazi!

Tukikuongezea wiki nyingine ninaomba suala la kudeal na watu wanaoishi hapa nchini pasipo kuwa na kibali na kufanya kazi pia ilihali wanajijua wao ni wageni(sio rais wa TZ) yakupasa kudeal nao effectively warudishwe wote kwao wote kwa gharama za nchi zao vinginevyo adhabu kali juu yao ifuate.
 
RIPOTI ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kuhusu kashfa ya kuchota fedha zaidi ya sh bilioni 200, kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zilizohifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umeanika madudu mazito yaliyofanywa na vigogo wa Serikali, Tanzania Daima limedokezwa.

Ingawa ripoti hiyo ambayo Tanzania Daima limebahatika kuiona, imekwepa kutaja majina ya vigogo hao na taasisi wanazotoka, lakini inaonyesha kuwa jumla ya fedha za Escrow ni sh bilioni 306 ambazo ni matokeo ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kulipishwa tozo la uwekezaji zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa.

CAG katika ripoti hiyo, anasema Tanesco walipaswa kurejeshewa sh bilioni 321 zilizolipwa ziada kwa IPTL kati ya mwaka 2002 – 2012.

"Hivyo fedha za Escrow ni fedha za umma, yote ilipaswa kurudi Tanesco na shirika kuendelea kuwadai IPTL sh bilioni 15," alisema CAG.

Madudu mengine yaliyoibuliwa katika ripoti hiyo ni kwamba, kampuni ya PAP haikununua kihalali hisa 70% za kampuni ya Mechmar katika IPTL kwani zilizuiwa na Mahakama, hivyo hawana hati halisi za hisa na PAP ilifanya udanganyifu katika malipo ya kodi kwa kutoa nyaraka za uwongo na kuikosesha Serikali Mapato ya sh bilioni 8.7.

Inaeleza kuwa, kosa hili linahusu pia mamlaka ya TRA Ilala, ambao walihusika kufanya mauzo hayo.

Akaunti ya kampuni ya VIP Engineering and Management (VIPEM), ilifunguliwa na mmoja wa wabia wa IPTL, James Rugemalira, ambaye alikuwa akimiliki asilimia 30 ya IPTL huku kampuni ya Mechmar Bhd ya Malaysia ikiwa na hisa asilimia 70.

Kutokana na kiasi hicho cha hisa, Rugemalira amelipwa kiasi cha dola milioni 75 (Shilingi Bilioni 123), zikionyesha kwamba alilipwa kiasi cha dola milioni 7.5 (Shilingi bilioni 12.4) mwaka jana na kiasi kilichosalia alimaliziwa mwaka huu.

Kiasi hicho cha fedha kililipwa kwa Rugemalira na kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh, ambaye kwa sasa ndiye mmiliki pekee wa IPTL baada ya kununua hisa za Mechmar na zile za VIP.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo Gazeti hili imeinasa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Gavana wa Banki Kuu (BoT), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, walivunja sheria kwa kuelekeza kuwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye tozo la uwekezaji isilipwe na kusababisha serikali kupoteza mapato ya sh bilioni 21.

"Waziri kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, hawakufanya utafiti wa kini kuhusu uhalali wa umiliki wa kampuni ya IPTL. Katibu Mkuu alisaini kutoa fedha za Escrow bila kuhakikisha fedha za Tanesco zinarudi, hivyo kusababisha upotevu wa zaidi ya sh bilioni 321," inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Kwa upande wa Tanesco, Mkurugenzi wa Shirika hilo na Bodi yake, hawakutimiza wajibu wao kwa kugeuza maamuzi yao (ama kwa kushinikizwa na Wizara au kwa rushwa), na kulikosesha shirika hilo zaidi ya sh bilioni 321.

Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikaririwa bungeni kwamba fedha hizo sio za umma, ripoti hiyo inaonyesha kuwa ni za umma.

Mgogoro uliosababisha fedha kuwekwa katika akaunti hiyo ya Tegeta ya BoT, ulitokana na Tanesco kugoma kulipa gharama za uwekaji mitambo (Capacity Charge), kwa IPTL mwaka 2006 kwa vile ilibainika IPTL ilikuwa ikitoza gharama kubwa kuliko iliyopaswa.

Akaunti hiyo ya Tegeta, ilianzishwa kwa sababu ya kuhifadhi fedha zote zilizopaswa kulipwa na Tanesco hadi hapo mgogoro baina ya pande hizo mbili umalizike.

Hata hivyo, Septemba mwaka jana, serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, iliagiza BoT kulipa fedha hizo kwa kampuni ya PAP mara baada ya kuridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kwamba mgogoro baina ya wamiliki wa IPTL na Tanesco umemalizika na hivyo Benki Kuu haina sababu ya kuhifadhi fedha hizo tena.

Uamuzi huo wa kulipwa, ulizua upinzani mkali bungeni ambapo wabunge wawili wa kambi ya upinzani; Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, walidai kuwa zoezi hilo limejaa ufisadi na Bunge liliazimia kwamba suala hili lifanyiwe uchunguzi wa kina na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


Nina wasiwasi sana kama hiyo report iliyofikishwa Tanzania Daima itakuwa haijachakachuliwa... Maana hainiingii akilini kabisa kama kwenye uchunguzi huo wa CAG hakuna sehemu ambayo alitaja pesa ilipotoka kwenye account ya ESCROW ilipelekwa na kuwa deposited kwenye account ipi na ipi na kutaja wamiliki wa hizo account zote....
 
Payment in kind. Kwa hiyo hawa VIP hawakutoa Cash, kwa hiyo 30%?

Halafu ikafikaje $491M?



Huu ndio "wizi wakisheria".

Rugemarila mwizi tu mkuu...Ila just for curiosity and connecting dots.Standard Chartered ni benki ya wapi?
 
Ningebahatika kuwa rais wa Tanzania walau kwa wiki moja tu, kitu ambacho ningefanya ni kuhakikisha kuwa siku ya kwanza ya utawala wangu inatungwa Sheria ya kunyonga wanasiasa waliohujumu uchumi.

Siku ya pili napata orodha ya wahujumu uchumi sugu au mafisadi papa. Siku ya tatu wanafikishwa mahakamani. Siku ya nne kesi inasikilizwa, ushahidi unatolewa na watuhumiwa wanapewa dakika tano-tano tu za kujitetea kila mmoja. Siku ya tano hukumu zinatolewa. Siku ya sita wananyongwa hadharani. Siku ya Saba utawala wangu unaisha. Anaingia rais mwingine!

ili nchi yetu iwe yenye maendeleo sawa na Marekani itabidi tukuongezee mwezi mmoja tu,unatosha
 
Safari hii tutaheshimiana tuu.

Kanu iliondoka kwa kashfa ya huyu huyu kalasinga

Acha weeee...Sio kwa Tanzania hii...Siasa za kenya ziko tofauti ...watu wakiamua kuchukua hatua wanachukua....

Kwa hawa makondooo..mang'ombe watanzania usitegemeee lolote....Sijui nani katuloga....
 
Ukinipa mwaka naanza kuwashughulikia wale wafanyabiashara wote wakubwa ambao wamekuwa wakikwepa kodi. Ikidhihirika wazi kwamba ni kweli walikwepa kulipa kodi: Kwanza, wanatandikwa viboko. Pili, mali zao zinataifishwa. Tatu, wanatupwa gerezani. Na zoezi hili litafanyika nchi nzima.

Usimamizi wa kodi utasimamiwa barabara nchi nzima. Adhabu ya mtu atakayepatikana anadokoa kodi hata kama ni pesa kidogo ni miaka 5 jela. Nchi itaongozwa na utawala wa sheria isipokuwa mimi, rais tu ambaye nitaifanya sheria inisaidie kuongoza kidikiteta. Sheria ya jumla ya mwizi yeyote wa mali ya umma ni kunyongwa hadharani. Sheria ya jumla ya mtu kudharau dini ya mtu mwingine ni miaka 5 jela. Sheria ya jumla kwa wauza sembe ni miaka 20 jela.

System hii ya CCM ya Centralization of Power itafutwa rasmi. Hii ndiyo inayosababisha ufisadi. Nchi itagawanywa katika majimbo na madaraka kamili yatarudishwa katika serikali za majimbo. Magavana wataongoza majimbo na watawajibika moja kwa moja kwangu. Kuiweka nchi katika mstari, kusimamia kodi na kurudisha nidhamu katika utumishi itachukua mwaka mzima. Mnataka kuniongeza muda tena?

Hapana hapa tunakuchionganisha na Marekani tu wakudundeeee mpaka useme ulikuwa wapi kugombea Urais siku zote sasa hivi Shirika la nyumba lingekuwa linajenga nyumba na kuwapa wananchi wa eneo husika bure.
 
hawa nao wameishiwa,kama kweli mmepata hiyo ripoti iwekeni hapa sio mnataletea stori za vijiweni kwenu,Tanzania daima mnakosa credibilty.
 
Ningebahatika kuwa rais wa Tanzania walau kwa wiki moja tu, kitu ambacho ningefanya ni kuhakikisha kuwa siku ya kwanza ya utawala wangu inatungwa Sheria ya kunyonga wanasiasa waliohujumu uchumi.

Siku ya pili napata orodha ya wahujumu uchumi sugu au mafisadi papa. Siku ya tatu wanafikishwa mahakamani. Siku ya nne kesi inasikilizwa, ushahidi unatolewa na watuhumiwa wanapewa dakika tano-tano tu za kujitetea kila mmoja. Siku ya tano hukumu zinatolewa. Siku ya sita wananyongwa hadharani. Siku ya Saba utawala wangu unaisha. Anaingia rais mwingine!

idea yko km yangu tehhhhh
ningeanza na wale wa NBC.. then rada.. Then EPA then Dowans na richmond.. Then tembo.. Iptl. . Then dawa za kulevya n.k
 
Huyu mdudu IPTL kwa nn serikali isivunje mkataba nayo? kama ni kuwalipa tuwalipe tu gharama za kuvunja mkataba na mambo yaishe tu.

Jenerali. kuuvunja sasa hivi ni balaa, kwani hawa mafisadi walishaingia mkataba mwingine mwaka jana na hiyo IPTL ambao utadumu mpaka 2033. Na katika mkataba huo TANESCO itakuwa inailipa IPTL 400m kwa siku! Upo hapo?
 
Watanzania watu wa hovyo sana , hapa tumejikita kujadili ripoti ya CAG na kusahau kabisa ripoti ya TAKUKURU ambazo kimsingi zilipaswa zote zijadiliwe kwa pamoja.
Haiwezekani ripoti ikose majina ya waliopiga hela.
Uhuni tu.
 
ningebahatika kuwa rais wa tanzania walau kwa wiki moja tu, kitu ambacho ningefanya ni kuhakikisha kuwa siku ya kwanza ya utawala wangu inatungwa sheria ya kunyonga wanasiasa waliohujumu uchumi.

siku ya pili napata orodha ya wahujumu uchumi sugu au mafisadi papa. siku ya tatu wanafikishwa mahakamani. siku ya nne kesi inasikilizwa, ushahidi unatolewa na watuhumiwa wanapewa dakika tano-tano tu za kujitetea kila mmoja. siku ya tano hukumu zinatolewa. siku ya sita wananyongwa hadharani. siku ya saba utawala wangu unaisha. Anaingia rais mwingine!


rais wa chama gani please
 
Ningebahatika kuwa rais wa Tanzania walau kwa wiki moja tu, kitu ambacho ningefanya ni kuhakikisha kuwa siku ya kwanza ya utawala wangu inatungwa Sheria ya kunyonga wanasiasa waliohujumu uchumi.

Siku ya pili napata orodha ya wahujumu uchumi sugu au mafisadi papa. Siku ya tatu wanafikishwa mahakamani. Siku ya nne kesi inasikilizwa, ushahidi unatolewa na watuhumiwa wanapewa dakika tano-tano tu za kujitetea kila mmoja. Siku ya tano hukumu zinatolewa. Siku ya sita wananyongwa hadharani. Siku ya Saba utawala wangu unaisha. Anaingia rais mwingine!
mkuu siku ya saba ya kutaifisha mali zote za mafisadi na wahujumu uchumi walionyongwa siku ya sita,siku ya nane unavunja mikataba yote yenye utata, siku ya tisa fukuza wahamiaji haramu wote, siku ya kumi kamata wauza unga wote, siku ya kumi na moja muachie rais mwingine.
 
Mungu ibariki Tanzania

Mkuu unadhani mungu amekosa kazi kiasi hicho hadi aache majukumu yake ya msingi aje kuhangaika na nchi ya wapuuzi kama hii, yaani haya maviongozi yana uroho usio na maana, hivi mtu kama PM anakua na shida gani kiuchumi hadi afanye upuuzi wa hivi? Au hao wezi wenzake hivi wanaiba fedha zote hizo za nini wakati ukishakua kiongozi tayari una maisha mazuri tu?
Yaani mtu anaiba utahisi ataishi miaka 1,000 kumbe hata miaka 100 hafikishi eti.
Mungu keshachoka na mambo yetu bana, ni bora tumuache asaidie watu wanaojielewa.
 
Mwenye ripoti original ailete aise, hawa wezi safari hii lazima tuwaondoe kabisa.
 
Hizo ni porojo, hiyo ripoti iko wapi?

Umenikumbusha story ya yule baunsa aliyemkimbiza Dogo kisa Dogo kamwambia ikifika saa Tisa lazima nije kukutia dole. Wakati anamkimbiza Dogo akaingia nyumbani kwa babu aliyekuwa anatengeneza baskeli hapo nje. Yule Babu akamuuliza Baunsa sababu za kumkimbiza huyo Dogo ndipo baunsa kwa hamaki akasema " Si huyo Dogo kasema ikifika Saa tisa anakuja kunitia dole? Aje sasa anitie"
Babu wa watu kwa upooole akamjibu, Mjukuu wangu, saa hizi ni saa SITA, si Usubiri hiyo saa TISA ifike kama alivyokuahidi kuja kukutia dole? Au Una haraka sana na hilo dole? Baunsa likapaniki na kumtukana yule babu na kuondoka kwa aibu.
Sasa Faiza Foxy, wewe na wenzio si msubiri hiyo saa TISA?
 
uchafu like this cant be manipulated dhana ya responsibility inakuja hapa na mtu lazima aende jela
 
Back
Top Bottom