Ukinipa mwaka naanza kuwashughulikia wale wafanyabiashara wote wakubwa ambao wamekuwa wakikwepa kodi. Ikidhihirika wazi kwamba ni kweli walikwepa kulipa kodi: Kwanza, wanatandikwa viboko. Pili, mali zao zinataifishwa. Tatu, wanatupwa gerezani. Na zoezi hili litafanyika nchi nzima.
Usimamizi wa kodi utasimamiwa barabara nchi nzima. Adhabu ya mtu atakayepatikana anadokoa kodi hata kama ni pesa kidogo ni miaka 5 jela. Nchi itaongozwa na utawala wa sheria isipokuwa mimi, rais tu ambaye nitaifanya sheria inisaidie kuongoza kidikiteta. Sheria ya jumla ya mwizi yeyote wa mali ya umma ni kunyongwa hadharani. Sheria ya jumla ya mtu kudharau dini ya mtu mwingine ni miaka 5 jela. Sheria ya jumla kwa wauza sembe ni miaka 20 jela.
System hii ya CCM ya Centralization of Power itafutwa rasmi. Hii ndiyo inayosababisha ufisadi. Nchi itagawanywa katika majimbo na madaraka kamili yatarudishwa katika serikali za majimbo. Magavana wataongoza majimbo na watawajibika moja kwa moja kwangu. Kuiweka nchi katika mstari, kusimamia kodi na kurudisha nidhamu katika utumishi itachukua mwaka mzima. Mnataka kuniongeza muda tena?