Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Revealing: TANESCO inaidai IPTL Tshs Bilioni 321...

Kwahiyo madai yenu ni yapi nyie kina Kafulila? Chenji au fedha ya escrow yote? Kama ni chenji imetoka wapi wakati kabla ya IPTL haijaanza kupokea hizo capacity charge na malipo mengine kulikuwa na hukumu ya ICSID ya mwaka 2001 iliyoshusha Capacity charge na IPTL walikubaliana nao ndio uzalishaji ulipoanza 2002. Hakuna chenji na fedha ya escrow ni haki ya IPTL na tusubiri ripoti ya kihasibu ya CAG tuone itasema nini siyo haya mat@pishi yenu.
Kwahiyo kusingekuwa na mgogoro wa wawekezaji ( mechmar na VIP ) walioomba kufunguliwa kwa escrow account haya yote yasingekuwepo?

Huelewi.....CAG amesema ni fedha za umma ....... uwe mpole tu ..........
 
Huelewi.....CAG amesema ni fedha za umma ....... uwe mpole tu ..........
mkuu imemkata maini mwenzio ha ha ha nadhani hatakuwa tu mpole ila atakuwa amepatwa na tumbo la kuhara kabisa!!!
 
Wewe acha kuhangaika .....hii ni comment ya Zitto leo hapa JF alafu unaibua magazeti ya enzi hizo ......soma hapo pekundu ...........

ZITTO ndio mdudu gani huyo? Kwahiyo wewe unataka huyo Zitto wako ndie awe msemaji wa mwisho kwangu hayo si mawazo yake kwa maslahi yake.

""Katika hali ya sasa ambapo mambo mengi yako hadharani waheshimiwa wabunge wawili ambao wamejitokeza waziwazi kutaka kuwakamata wezi na wala rushwa, hasa kwa suala la akaunti ya ESCROW, sijui wanafanya makusudi wakijua au kwa kutojua.
Kampuni ya Malaysia ya Mechmar iliyokuwa kinara katika mchezo imejitoa na sasa shughuli siyo za kuzalisha umeme bali ni kushitakiana mahakamani ndani na nje ya nchi.
Kuhusiana na akaunti ya ESCROW ukweli usiopingika ni kwamba fedha ambazo ziliwekwa humo ni za IPTL kutokana na makusanyo ya malipo ya uuzaji umeme kwa TANESCO ambazo zilikuwa hazijagawanywa kwa matumizi ya uwekezaji, uendeshaji au gawio kwa wanahisa.

VIP Engineering and Marketing ilipopeleka maombi ya kuondoa shauri Mahakamani ili iuze hisa zake za asilimia 30% jambo hilo lilitokana kwamba tayari mnunuzi alishanunua na kumiliki hisa asilimia 70% za Mechmar. Kimantiki PAP ndiyo walikuwa wanamiliki mitambo, mali na fedha za akaunti ya ESCROW na hivyo PAP alikuwa na fedha za kutosha kumlipa VIP Engineering and Marketing.
Wanaojitokeza zaidi sasa hivi ni maofisa wa ubalozi (Uingereza) kutetea maslahi ya Benki yao ya Standard Chartered of Hong Kong ambayo imekuwa ikishirikiana na kampuni ya Mechmar katika mambo ya uwekezaji na utoaji mikopo ambayo inazua utata. Benki ya Standard Chartered of Hong Kong imefungua kesi dhidi ya IPTL na serikali ya Tanzania kuhusu akaunti ya ESCROW.
Jambo la kujiuliza ni kwamba katika suala zima la akaunti ya ESCROW ambayo wabunge wamelivalia njuga benki ya Standard Chartered inaishtaki serikali ya Tanzania na kuidai zaidi ya dola za kimarekani milioni 150 kutoka kwenye akaunti ya ESCROW. Kwa nini kesi hiyo isifunguliwe Tanzania?
Je, kama fedha hizo zinazodaiwa ni za Standard Chartered ambaye anadai ni mmiliki wa IPTL, nini itakuwa hatima ya upanuzi wa uzalishaji ambao IPTL ilikuwa imepanga na kubadilisha mitambo kutoka kutumia mafuta mazito kwenda kutumia gesi? Je, kweli gharama za umeme zitapungua?""
 
Rugemarila mwizi tu mkuu...Ila just for curiosity and connecting dots.Standard Chartered ni benki ya wapi?

Standard Chartered ni ya Uingereza huko, ila ina matawi mengi tu Nchi zinazoendelea na Africa.

Hawa wanaosema hela zote za IPTL, kama ni hivyo na kwamba hakuna ubishi sasa kwanini ziko kwa Escrow na sio mifukoni kwao?
 
Hivi hii nchi ni yatima?!

Nchi hii borauwe mjinga utalalausingizi mnono.Lakini kamaunaakili timamu utaona kilakitu hakiendi sawa naunaweza ukawazahiidhuluma tunayofanyiwa sisi wanyonge hadi ukaona bora ufetu. Lakini yote 9_ 10 is to make decision.
 
Standard Chartered ni ya Uingereza huko, ila ina matawi mengi tu Nchi zinazoendelea na Africa.

Hawa wanaosema hela zote za IPTL, kama ni hivyo na kwamba hakuna ubishi sasa kwanini ziko kwa Escrow na sio mifukoni kwao?

Isijekuwa tunachezeshwa ngoma tusiyoijua...hapa naiona uingereza ikitetea maslahi ya benki yao...Standard Chartered.
 
Hivi ripoti halisi haiwezi kupatikana tulinganishe na hio watakayoichakachua.

Report halisi ndiyo iliyowasilishwa na CG bungeni na kukabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma Mhe Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Sina shaka kwamba ataitendea haki Jamii ya Tanzania kwa kutoa ukweli wa report na uovu wote uliofanyika.
 
Watu wengi wamekuwa wakikopeshana kudhulumiana na kadhalika na kupelekana mahakamani kufungua kesi za madai.
Kuna taarifa kuwa TANESCO inainai IPTL na wengine wana sema IPTL inaidai TANESCO.Sijui nani mkweli.

Kwa nini kama wanadaiana wasipelekani mahakamani? Wapelekane bungeni?

Swali langu kwa wanasheria na wabunge ni je kesi za madai siku hizi huwa zinapelekwa bungeni? Spika ndie aweza amua hizo kesi au majaji wa mahakama?
Naomba jibu

Wenu mtiifu EAST AFRICAN EAGLE
eastafricaneagle@gmail.com
 
Jesus....Akaunti ilikuwa na bilioni 306 ......good enough hizi zilikuwa ni fedha za umma.....mbaya zaidi Tanesco inaidai IPTL bilioni 321.......hakika nawaambia....hii ngoma italeta historia mpya nchi hii.........kama bado kuna Watanzania waliobaki na chembe za uzalendo lazima tusimame pamoja sasa kuliko wakati wowote......
Tujikumbushe
 
Back
Top Bottom