Ukitaka kujua kwamba umejaza mkojo huko kichwani kwako jiulize maswali haya;
- Kilimo ni biashara au sio biashara? Na kama ni biashara maana yake unatakiwa ufanye feasibility and viability study, maana yake ni kwamba kabla ya kulima unapaswa kuangalia sera ya serikali husika kuhusu zao husika, hili la kupiga marufuku utoroshaji mahindi kwenda Kenya lipo kila siku, si jipya, pia unaangalia projected demand and supply katika soko husika, hizo hesabu unazopiga hadi zinaleta negative huwa zinapigwa kabla ya kufanya biashara yoyote ile, sio kilimo tu, na jibu ukipata zero au negative maana yake hiyo biashara sio viable muda huo, kwahiyo tafuta biashara / zao lingine la kulima. Mmefanya biashara na mmepata hasara kama wafanya biashara wengine wanavyopata hasara hapa nchini, kwani nyie ni akina na nani hadi msipata hasara? Unataka nikupeleke kariakoo ukasikie vilio kule au unafikiri ni nyinyi tu mnaopata hasara? Mbona mkipata faida hamji kugawana nasi hizo faida, shove your losses up your a#$ and shut it!
matusi ni dalili ya kupaniki, tulia lete hoja vizuri utaeleweka.
wakulima wamefanya utafiti wao wakagundua mahindi ni zao ambalo muhimu kwani asilimia kubwa ya watz na nje ya Tz wanakula hicho chakula, wakaingia sokoni wakatafuta inputs wenyewe Mungu akawajaalia wakavuna.
mshangao unakuja kwa hawa mnaojiita serikali msikuwa na uchungu na wakulima kwa kuwazuia kumalizia chain yao ya biashara(kufika sokoni kwa bei waliokusudia) bila kujali kuwa nyie kama serikali hiki chakula mtakinunua kwa bei amabyo ni reasonable ili kumsaidia huyu mkulima ila kumdidimiza, shame on you.
Unataka mkulima wa matombo anaelima zao linaloendana na mazingira yake tena kwa kuhangaika na kutafuta inputs mwenyewe bila msaada wa hiyo serikali yako na afanye fisibility study ili kujua kipaumbele cha
serikali na siyo
soko ilihali kilimo hicho hicho bado hiyo serikali haioneshi kipaumbele kwenye kilimo???
serikali yako ndo haifanyi utafiti juu ya gharama zinazotumiwa na wakulima, ingelizifanya isingewaambia wasiuze kule ambako kunawapatia faida.
serikali yako imefanya jitahada gani kuwatafutia soko ili gharama za wakulima zirudi na kilimo kiwe na tija hata kwa mkulima mdogo wa kilimo cha mkono zaidi ya kuwaambia wasipeleke kwenye soko zuri.
unafurahia frame za kariakoo kufungwa kuwa ndo sehemu ya maendeleo na kipaumbele chenu kama serikali au ndo
kipimo chenu cha uchumi kupanda kwa kuwakamua kodi kubwa, na hamjitathmini kwa nini wanafunga zaidi ya kushangilia na kutoa matusi.
sikushangai kama rais wako tu nae anapaniki anapoambiwa ukweli itakuwaje wewe. mjitathmini hakuna kinachofanyika kama unashangilia kitu kisichokuwa na matokeo chanya.