Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Tumieni akili achaneni na siasa ,mvua ya mwezi Wa December 2017 imesababisha watu wengi kulima na kuivishia pamoja na kusababisha mahindi kuwa mengi na bei ya chini kwa hiyo ihukumu mvua kunyeesha, mfano sasa kwa wale waliolima nyanya wwnapiga hela kinoma ndo kilimo kilivyo
Hapo anayepaswa kutumia akili ni wewe mkuu,
Hiyo mvua iliyonyesha mwaka jana ilikuwa ya miujiza haijawahi kunyesha before? mbona hatukuwahi kufikia hali hii? Uzalishaji ulikuwa wa kawaida kama miaka mingine

Hapa kuna matatizo makuu mawili

1.Serikali Kufunga mipaka na kuwazuia wakulima kuuza mahindi nje
2.Maghala ya kuhifadhia chakula ya serikali (NFRA) kutonunua chakula cha kutosha yani maghala ya serikali ni meupe
 
Uhakika wa kupata lishe kwa kumuumiza mkulima? Yani mkulima masikini wa mwisho kijijini auze mahindi kwa hasara ili wewe upate milo mitatu?
halafu 80% ya tz population ni wakulima unamaanisha hao wote (80%) wazidi kukandamizwa kwenye umasikini ili ww ununue unga 200tsh?
Kilimo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine na kama ishu ni kumnufaisha mlaji bila kujali maslahi ya mzalishaji basi na mfuko wa cement uuzwe 5000, soda100, mafuta Lt 500tsh au ikiwezekana watuwekee bure kwenye magari,
Kama hayo hayawezekani why mkulima?? yeye pia anatumia rasilimali muda,mbolea,nguvu, madawa, usafiri nk kwenye uzalishaji.


Huu ni ubinafsi wa hali ya juu sana!!
Binadamu sisi ni wabinafsi sana.
 
Ndio, it means hadi omba omba watakula walau milo miwili kwa siku, tumpongeze rais kwa kuwatetea masikini, au mlitaka unga upande bei kama sukari ili mpate cha kuongea?

Acha unazi wa ovyo mzee!

We tangu lini watu wakashindwa kununua unga wa ugali?

We mahindi kuporomoka hadi 20000 sawa kwako?

Yaani inamaana kwa yield maximum ambayo ni gunia 20 kwa ekari mtu auze apate laki nne?
 
Ukiona hivyo ndo ujue sasa thaman ya Tz shiling inaimarika[emoji23][emoji23],..kwamba ,..kwa lak 1 unatumia miez m3.saf sana..sasa inabid iwe hiv had kwenye nyama,sio yashuke maharage na unga tu.
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late. Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake
Hii nchi sijui ni nani aliyeiroga.
 
Uongo mtupu. Kahama bado gunia la mahindi Tsh. 48000.
Kuna sehemu bei hazishuki sana. Hapo Kahama mzunguko wa pesa ni mkubwa ukilinganisha na Sumbawanga. Usafiri wa kutoka na kuingia Sumbawanga ni wa shida na hivyo kuathiri biashara na sehemu zilizo jirani na mji huo. Mahindi yaliyovunwa mwaka jana huko Sumbawanga kama tulivyoelezewa hayakupata wanunuzi baada ya kuzuia kuuzwa nje ya nchi. Hivyo basi ni wazi bei ya bidhaa hii imeshuka kupita kiasi katika mji huo.
 
Hivi mahindi elf 27000 ni nchi gani huko, maana hapa Musoma mahindi tunanunua debe elf10 kwa maana ya tsh60000 kwa gunia, kama kuna watu wana mihela yao simtuletee huku
 
Kama nawaona ambao wamechukua mikopo ili walime na wakafanya jitihada shambani halafu mwisho wa siku hali yenyewe ndio hii tu apoelekea watz wengi watakuwa na ugonjwa stress kupindukia
 
Mahindi naona ni zao la chakula kwa hiyo kuzuia kuuzwa nje ni sahihi maana hiyo pia ingeleta food scarcity nchini. Mi naona hii ni fursa nzuri ya watanzania kununua chakula cha kutosha na kuweka store ili mipaka ikija kufunguliwa wawe na food security ya kutosha.
 
-Uza unga badala ya mahindi
-tengeza chakula cha kuku na uuze kwa wafugaji,
upatikanaji wa chakula cha mifugo nafuu itanenepesha mifugo na kuongeza idadi yao kiasi kwamba sasa hata kuku utamnunua kwa tsh 1500,
hiyo ndo faida ya mass producing inafanya soko linakuwa saturated na bei kuwa nafuu kwa chakula,
ndo maana nchi zilizoendelea huwezi kusikia baa la njaa,sababu watu wanaproduce zaidi ya mahitaji,
na baki inakwenda ku be utilized kwa matumizi mengine,ndo maana utakuta product kibao kama cornflakes,tortila chips,methano etc
 
Mahindi naona ni zao la chakula kwa hiyo kuzuia kuuzwa nje ni sahihi maana hiyo pia ingeleta food scarcity nchini. Mi naona hii ni fursa nzuri ya watanzania kununua chakula cha kutosha na kuweka store ili mipaka ikija kufunguliwa wawe na food security ya kutosha.
Uko sawa mkuu
 
Back
Top Bottom