Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Sera ni kila mtu aishi kama shetani! itafika wakati hiyo elfu 20 hutoipata pia! pole mkulima mwenzangu
 
Je wangeruhusu yauzwe nje kisha gunia moja likiwa 120,000/= na kilo ya mahindi ikawa 4,000/= ungelaumu serikali?, kwenda zako huko
Na yangeuzwa yote halafu waanze tena kulia kwa kuilaumu serikali kwa kuruhusu mahindi kuuzwa nje.Mbongo kubadilisha agenda ni dk moja.
 
Cha ajabu zaidi mwezi jana kuna mfanyabiashara kutoka kenya aliingia hadi porini kwetu akanunua gunia kwa bei ya Tsh. 25000/

Kitu ambacho n cha kushangaza sana hakijawah tokea
 
Sioni tatizo, serikali inapaswa sasa inunue mahindi ya kutosha, magari ya jeshi yatumike kusambaza mahindi nchi nzima.

Chakula isiwe kitu tena kwa Mtanzania ,tufikirie mambo mengine ya maendeleo. Maana sasa naamini hata chakula cha kuku kitashuka bei kutokana na Pumba kupatikana kwa wingi.

Kuku watashuka bei ,afya itaboreka safi saana
Napembejeo nazo zitashuka bei ili kupunguza makali kuhudumia mazao shambani
 
Kama ni kweli kazi ipo....
Huyu Bwn amewatia watu umasikini mkubwa kwa amri za kiajabu bila hata kuuliza wakulima!!
Mahindi bei imekufa,mbaazi zimeozea maghalani soko limezibwa!!
Wakuu tumia busara mnauwa uchumi wa nchi!!
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku?

Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
Makamanda ndo walivyo, kazi yao ni kulialia tu: wanaume kama mabinti (lady jide aliimba)
 
Hizi Wizara 2 Kilimo na Mifugo bado hazijapata Mawaziri wajanja
. Ni vuluvulu kila kona.
 
"Mafanikio haya ya kushusha bei ya mahindi hayajawahi kutokea toka nchi ipate uhuru, HAPA KAZI TU" DR ABASS VOICE-MSEMAJI
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku?

Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
Akili yako ni fake wakulima wetumia gharama kubwa wamepata hasara kwa kuvuruga soko.
Wakuu wamefilisi watu, watalipaje madeni ya benki??
Tumia hekima na busara basi??
 
Uhakika wa kupata lishe kwa kumuumiza mkulima? Yani mkulima masikini wa mwisho kijijini auze mahindi kwa hasara ili wewe upate milo mitatu?

halafu 80% ya tz population ni wakulima unamaanisha hao wote (80%) wazidi kukandamizwa kwenye umasikini ili ww ununue unga 200tsh?

Kilimo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine na kama ishu ni kumnufaisha mlaji bila kujali maslahi ya mzalishaji basi na mfuko wa cement uuzwe 5000, soda100, mafuta Lt 500tsh au ikiwezekana watuwekee bure kwenye magari,
Kama hayo hayawezekani why mkulima?? yeye pia anatumia rasilimali muda,mbolea,nguvu, madawa, usafiri nk kwenye uzalishaji.

Huu ni ubinafsi wa hali ya juu sana!!
Huyo chizi umemjibu kisomi sana lakini sidhani kama kakuelewa labda umjibu kwa lugha wanayoongea nduguze wote kijijini kwao huko.
 
Chakula kikiwa bei nafuu mnakasirika badala ya kufurahi. Kweli nyie ziro kabisa. Kwa taarifa yenu wakulima wadogo wadogo ambao ni wengi wanalima mazao ya chakula kwa ajili ya matumizi binafsi na siyo kuuza.
Bei nafuu kwako ni raha vp gharama za uzalishaji za mkulima unamlipa vipi?
 
Huyo chizi umemjibu kisomi sana lakini sidhani kama kakuelewa labda umjibu kwa lugha wanayoongea nduguze wote kijijini kwao huko.
We unadhani thamani halisi ya gunia ilitakiwa liuzwe bei gani??mbona hata likipanda bei mtapiga kelele..kwa sasa goli mmehamishia kwa mkulima..bei ikipanda mtahamishia goli kwa mlaji
 
Hizi taarifa hazina uhalisia! Kwenye mitandao kila mtu anasema lake. Juzi nimenunua dona 25kg Dar kwa 19,000. Sasa unataka kuniambia gunia la kilo 100 liuzwe bei sawa na kilo 25?? Unamdanganya nani?
Hiyo dona umenunua iliyoandaliwa tayari hivyo huyo aliyekuuzia amejilipa gharama zake zote hapo za kuliongezea thamani gunia lake la mahindi la bei chee,ungeniambia umeenda kusaga mwenyewe mahindi yako kwa hiyo gharama ungeeleweka.
 
Koboa hayo mahindi, pumba tengeneza chakula cha nguruwe bei ya nyama inapanda maradufu. Kuhifadhi mahindi yaliyokobolewa ni rahisi sana!
 
We unadhani thamani halisi ya gunia ilitakiwa liuzwe bei gani??mbona hata likipanda bei mtapiga kelele..kwa sasa goli mmehamishia kwa mkulima..bei ikipanda mtahamishia goli kwa mlaji
Sina cha kukujibu.
 
Back
Top Bottom