nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,673
- 14,052
Naam hili jambo nilikuwa nalichukulia poa...lakini baada ya kuamua kufuatilia kidogo naanza kupata uthibitisho pasi kuwa na shaka juu ya mzunguko wa maisha ya viumbe sisi bin adamu.
Kwa kifupi sana tafiti ni nyingi lakini......nilipata kuishi nyanda za juu kusini mwa Tanzania nikiwa kijana mdogo miaka mingi sana iliyopita.
Nilikuwa nina rafiki yangu Mbulushi...rafiki yangu huyu kwa bahati mbaya alifariki.
Siku ya siku sina hili wala lile nikiwa katika nchi ya mbali sana nikakutana na kijana mmoja amefanana na yule rafiki yangu kwa zaidi ya asilimia 90%...nikabaki namshangaa...kitu cha ajabu na yeye kama alikuwa ananishangaa...nikamuuliza ulishawahi kuishi.
Tanzania...akasema hapana hata Neno Tanzania ndio leo analisikia.
Ajabu zaidi anasisitiza kwamba ananifahamu lakini hakumbuki ni wapi tulisha wahi kuonana
Mahali ambapo nilipata mshituko niliona alama katika mkono wake wa kulia sawasawa na yule rafiki yangu,,,(alama hii naikumbuka kwa sababu alianguka na baiskeli akachanika na kushonwa katika hospitali ya Aga khan)....sasa huyu jamaa anasema hiyo alama amezaliwa nayo hivyohivyo.
Nikijaribu kumuuliza yeye asili yake ni wapi anasema ni Afganistan na hana ndugu wala jamaa Afrika.
Kwa kifupi sana 1.Sauti yake 2.Ongea yake 3.Namna anavyotembea ni yule marehemu kabisa kabisa.
Yule Marehemu leo angekuwa na miaka kama 70 hivi na huyu niliyekutana nae yuko kwenye miaka ya 30 katikati.