Mama kwanza pole kwa majukumu,
Nimeona nitumie njia hii kukushauri,Mimi ninampenda sana mumeo waziri wangu mkuu aliyestaafu,mtu aliyekuwa mchapakazi na mwenye maamuzi magumu.Mama ninakushauri ufungue moyo wako uone ukweli huu na kwa kuwa ninaamini unampenda mumeo utachukua hatua ya kutafakari na kufanya maamuzi magumu.
Mzee wetu anaumwa Mama hakuna haja ya kumfedhehesha mbele za watu,msitiri mumeo ,wanasiasa wanalazimisha kumtumia si kwamba wanampenda kama umpendavyo wewe ila wanapenda pesa zake tu.
Kama ni kujisafisha tayari walimtukana fisadi wameshamsafisha wenyewe,usisubiri yampate ya aibu zaidi,unajua yaliyompata akiwa Chato,kuna siku yatamtokea akiwa amechomekea na waandishi wataweka hadharani.
Mwacheni mzee apunzike amelifanyia taifa hili kazi njema sana,wewe waambie anaenda kucheki Afya then potelea huko urudi siku 3 kabla ya Uchaguzi, lakini wambie wanao pesa alizo nazo Baba yao alitafuta akiwa timamu ni wajibu wao kuzitunza na kuziendeleza na kumshauri wakijua hawana Baba mwingine na hao wapambe baada ya uchaguzi hawatawaona.
Ni ushauri Mama