Regia hakuumwa,ni asubuhi tu aliamka na huenda alikuwa na mipango yake ya kukamilisha kwa siku ya leo, lakini kufumba na kufumbua hatunaye tena! Tukio hili linatufundisha kuwa Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana, tena yamejaa taabu na shida, laiti tungelijua kuwa kila dakika tunayoipitisha tukiwa hai ni muujiza wa Mungu tungeliomba msamaha wa dhambi zetu kila dakika na kuwa na amani na watu wote.........!!Mungu utuwezeshe kuzihesabu siku zetu, ili siku la kutufika likitufika tufe tukiwa mikononi mwako!!
Nawaombea ndugu wote, watanzania wote na chadema wote wawe na subira na Mungu awapatie wepesi katika kuomboleza msiba huu mzito wa dada yetu Regia.
Mbele yetu ni wewe, nyuma yako ni sisi, Mungu ametwaa kiumbe chake, kazi yake haina makosa