Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Mtetezi wa wanyonge, mtetezi wa kilombero, mtetezi wa maskini wa Tz hebu ona Kilombero wanavyokulilia, ona watz wanavyokulilia, ona CDM wanavyokulilia, ona JF tunavyokulilia amka basi japo utuage, tukusalimu mara ya mwisho Regia.Dah!! RIP REGIA.
 
Amekufa Siku ya Sabato..

20:8-11 katika orodha ya Amri Kumi:
Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya mlango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
 
sina cha kusema,ila naamini mungu ametuondolea jiwe atatuwekea jiwe.
innalillah wa innalillah raajun.
 
OMG,

Nafungua JF naona picha kubwa, nikasema wanamfanyia Regia promo gani?

Naona R.I.P, nataka kama nisiamini, labda anasema R.I.P kwa mtu mwingine? Lakini this is too much, ukiweka jina la mtu na R.I.P maana yake amefariki.

Reality kicks in. Amefariki.

Pamoja na differences zetu zote bado alikuwa mbunge wetu, na saa nyingine nikaanza kujisikia kama kawa mbunge wa JF, complete with reporting back here.

May all beings attain enlightenment.
 
sijawai kutokwa na chozi ukubwani.
Sikujua kuna siku itakuja kutokea ivyo.

Ila leo posti hii iliniliza nilipoifungua mchana wa saa 7.

Kweli imeniuma na itaniuma daima.
Tulikupenda na tunakukumbuka milele na daima.
Bwana kakupenda zaidi .
Bwana ametoa bwana ametwaa.
Jina lake lihimidiwe.
 

Pumzika kwa amani na umeonyesha mfano wa kutakana msamaha katika maisha yetu. Ushupavu wako wa kupigania demokrasia na maendeleo ya kweli nchini mwetu ni wa kugwa. Upambanaji wako licha ya ulemavu ulikuwa nayo ni funzo kwetu kuwa ulemavu si sababu ya kutojishughulisha na kuongoza watu. Nasema ulikuwa ni mshumaa uliowaka na kuzimika haraka, lakini simulizi na mguso wako utadumu. Upumzike katika Amani ya Milele! Amina!
 
Upumzike kwa Amani Dada Regia. Tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi.Mungu awajalie nguvu wanafamilia yake wote katika kipindi hiki kigumu sana.
 
Rest in peace kamanda, mwanaharakati, mpambanaji na sauti ya vijana na kina mama wa Tanzania. Mungu ailaze mahali pema paradiso roho ya marehemu.Amina
 
Duuh! Hii dunia kweli ni mapito.So young to go but what else could we do???!!! RIP Regia!
 
bwana alitoa, bwana ametwaa jina la bwana liheshimiwe> rest in peace regia.
 

Kwahiyo wasabato hawafi siku ya sabato? Acha masihala bwana. Mungu agenda zake hapangi na binadamu wa aina yoyote. Anapanga jinsi inavyompendeza.
 
Kwahiyo wasabato hawafi siku ya sabato? Acha masihala bwana. Mungu agenda zake hapangi na binadamu wa aina yoyote. Anapanga jinsi inavyompendeza.

mkuu, hilo file la sir godi lenye agenda umeshalipiga chabo nini, hebu tumegee kidogo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…