Redundancy kubwa kutua NSSF/PPF/GPF

Redundancy kubwa kutua NSSF/PPF/GPF

Mwanaharakatihuru

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2012
Posts
477
Reaction score
120
Vyanzo vinaeleza kwakuwa Watanzania wamekubaliana kuchukua malipo yao katika umri wa miaka 55 au 60 kwa lazima basi wafanyakazi wengi wa NSSF watapunguzwa katika ile hali ya kupunguza gharama za uendeshaji.

Pia wafanyakazi watakao punguzwa ni wale waliolikisha mapema taarifa za kupitishwa kwa sheria mpya mapema na wenye mrengo ule wa kuiwajibisha Serikali.

Vita ni vita mura hata mbuzi hukimbia
 
Hiyo ndiyo solution?

Hatua ya kwanza kwa NSSF ingejitoa kwenye ambitious projects kama vile Daraja la Kigamboni, uzalishaji wa umeme Kiwira, ili ku spare vijisenti vyetu.
 
mhhh kazi kweli kweli uwezo wao wa kufikiria ndio umeishia hapo.....
 
Vyanzo vinaeleza kwakuwa Watanzania wamekubaliana kuchukua malipo yao katika umri wa miaka 55 au 60 kwa lazima basi wafanyakazi wengi wa NSSF watapunguzwa katika ile hali ya kupunguza ghrama za uendeshaji.

Pia wafanyakazi watakao punguzwa ni wale waliolikisha mapema taarifa za kupitishwa kwa sheria mpya mapema na wenye mrengo ule wa kuiwajibisha serikali.

Vita ni vita mura hata mbuzi hukimbia

Kulikisha? Nilidhani muswada ulipelekwa bungeni mwezi April, 2012 na kupitishwa kwa ndiyo na sasa umeshasainiwa na raisi hivyo ni sheria. Na tayari mamlaka ya kusimamia mifuko ya jamii SSRA tayari imetoa PRESS RELEASE kuhusiana na kusitishwa kwa fao la kujitoa. Sasa mambo ya ku-leak yanatoka wapi?
 
Nadhani nyie hamjastuka.. Pesa zimejengea maghorofa sasa mkianza kuzichukua si watafilisika?.. Nyingine wamekopeshana 'kiaina'
 
Vyanzo vinaeleza kwakuwa Watanzania wamekubaliana kuchukua malipo yao katika umri wa miaka 55 au 60 kwa lazima basi wafanyakazi wengi wa NSSF watapunguzwa katika ile hali ya kupunguza ghrama za uendeshaji.

Pia wafanyakazi watakao punguzwa ni wale waliolikisha mapema taarifa za kupitishwa kwa sheria mpya mapema na wenye mrengo ule wa kuiwajibisha serikali.

Vita ni vita mura hata mbuzi hukimbia

Hakuna mtanzania mpumbavu wa kukubali malipo ya namna hiyo! tutapigana kufa kupona!
 
Huu utakua maumivu kwa sie vijama,maisha mafupi yalaaa.
Swali:Hii inawahuhusu hata waajiriwa kampuni binafsi?
 
Sheria ya mwanzo iliyounda NSSF ilisisitiza ni marufuku kwa fedha za michango ya washirik kuwekezwa katika miradi isiyo na kinga ya Serikali. Miradi ya kibiashara ikifilisika fedha za washiriki inapotea. Kwa hiyo fedha za michango zilikuwa zinawekezwa katika Goverment securities e.g Treasury Bills na Goverment long term stocks.

Kwa hiyo ni kule kukiuka haya maagizo ya guarantee kumefanya NSSF ikaribie kufilisika. Sio tu kwamba wafanyakazi watapunguzwa, bali wale wanaotegemea kulipwa fedha zao za pensheni kwa maisha yao ya uzeeni wamepoteza.
 
Kikwete; Jakaya Mrisho ni janga la kitaifa!:spider:
 
kwanza hatujakubaliana, mimi ni mwanachama wa NSSF mwaka wa kumi sasa, hakuna aliyekuja kuniuliza km nakubaliana na huo mpango au vipi, nasikis tu wabunge wanatupangia jinsi ya kutumia pesa zetu, ila wao watachukua mafao yao pindi ukomo wa ubunge wao utakapofikia. so wafanyakazi muone hapo hki imetendeka?
 
jamani kikwete apimwe damu yake(dna) ukute si mtanzania!? hawezi kufanya mambo ya kihuni hivi, anatuchukuliaje cc jamani??
 
Alikimbilia ikulu mwaka 1995 akaambiwa bado hajakua kiakili kuwa rais...akanuna kweli kweli akatumia mipesa mingi sana kuingia ikulu ona anavyoaibika sasa!amekopa pesa anashindwa kurudisha
 
Sheria ya mwanzo iliyounda NSSF ilisisitiza ni marufuku kwa fedha za michango ya washirik kuwekezwa katika miradi isiyo na kinga ya Serikali. Miradi ya kibiashara ikifilisika fedha za washiriki inapotea. Kwa hiyo fedha za michango zilikuwa zinawekezwa katika Goverment securities e.g Treasury Bills na Goverment long term stocks.

Kwa hiyo ni kule kukiuka haya maagizo ya guarantee kumefanya NSSF ikaribie kufilisika. Sio tu kwamba wafanyakazi watapunguzwa, bali wale wanaotegemea kulipwa fedha zao za pensheni kwa maisha yao ya uzeeni wamepoteza.

Mzee mwenzangu, uwekezaji wa hii mifuko umekuwa na msukumo wa kisiasa sana. Kuna pressure kubwa kutoka kwa wanasiasa na sasa tumepatikana. Kila mfuko una matatizo yake lakini NSSF una matatizo zaidi when it comes to investment. Ukitaka kucheka, tafuta list ya board members wa WAMA!
 
NSSF imefilisiwa na uongozi wa mdini Dau, amejitajirisha pamoja na maofisa waliomzunguka kwa kupitia miradi mikubwa ya ujenzi, wakishirikiana na makandarasi na baadhi ya viongozi wa ccm! Nina uhakika na ninachokisema
 
Nakumbuka mkurungezi wa Nssf amewai kutangaza kwamba wana hakiba za miaka 50 ijao iweje leo watuwekee masharti magumu ya kuchukua hela zetu kwa mda tuanao taka sisis ? kila mtu anataka ale hela zake mapema. Kuna watu wamemaliza mikataba na waajiri wao wanasubiri kuchukua hela. sasa wakisema mpaka wafikishe miaak 55 hawaoni kama watawaumiza?

Watanzania tuamke, NSSF siyo kama DESI wanamiradi mikubwa sana na pesa zetu wanazifanyia biashara, hatutaki kusikia mipango ya kipuuzi.
 
wa kwanza kupunguzwa kazi awe Mh Raisi Jakaya KIkwete ndie aliyefilisi mifuko hii kwa kutaka sifa kuanzisha miradi kwa fedha za wafanya kazi bila wafanya kazi kufahamu,Kukopa fedha kwa ajili ya kuendeshea kampeni za CCM,Kutumia fedha za mifuko kwa safair zake za kwenda kubembea
 
Sheria ya mwanzo iliyounda NSSF ilisisitiza ni marufuku kwa fedha za michango ya washirik kuwekezwa katika miradi isiyo na kinga ya Serikali. Miradi ya kibiashara ikifilisika fedha za washiriki inapotea. Kwa hiyo fedha za michango zilikuwa zinawekezwa katika Goverment securities e.g Treasury Bills na Goverment long term stocks.

Kwa hiyo ni kule kukiuka haya maagizo ya guarantee kumefanya NSSF ikaribie kufilisika. Sio tu kwamba wafanyakazi watapunguzwa, bali wale wanaotegemea kulipwa fedha zao za pensheni kwa maisha yao ya uzeeni wamepoteza.

Wananchi waliochangia NSSF ni lazima wawatumie wawakilishi wao Bungeni kusisitiza ni jukumu la Serikali kuwalipa mafao yao stahiki. Najua Serikali itatumia fedha zitokanazo na kodi, na miradi ya maendeleo au huduma iitakosa fedha. Lakini hali hii inatokana na uzembe wa Serikali kwa kukiuka Sheria ile ya Mwanzo iliyosisitiza uwekezaji ktk Treasury Bills na long term Govt securities e.g. Bonds etc.
 
Pesa za NSSF/PPF/GPF ni mali yetu sisi wanachama,kwahiyo serikali haipaswi kutu pangia jinsi ya kuchukua au kutumia pesa zetu,hime wanachama tusikubali dhuluma tuamke tuandamane kupinga hili suala kwa msingi huo
 
Back
Top Bottom