Redundancy kubwa kutua NSSF/PPF/GPF

Sheria ya mwanzo iliyounda NSSF ilisisitiza ni marufuku kwa fedha za michango ya washirik kuwekezwa katika miradi isiyo na kinga ya Serikali. Miradi ya kibiashara ikifilisika fedha za washiriki inapotea. Kwa hiyo fedha za michango zilikuwa zinawekezwa katika Goverment securities e.g Treasury Bills na Goverment long term stocks.

Kwa hiyo ni kule kukiuka haya maagizo ya guarantee kumefanya NSSF ikaribie kufilisika. Sio tu kwamba wafanyakazi watapunguzwa, bali wale wanaotegemea kulipwa fedha zao za pensheni kwa maisha yao ya uzeeni wamepoteza.

Hii italeta mlipuko mkubwa wa vuguvugu la mageuzi nchini. Nafikiri kitakachofanyika ni serikali kuingiza pesa ili wafanyakazi wa hilo shirika waendelee kulipwa hadi baada ya uchaguzi 2015 ili kusiwepo na kitu cha ku-instigate huo mlipuko wa madai pamoja na mageuzi.
 
NSSF imefilisiwa na uongozi wa mdini Dau, amejitajirisha pamoja na maofisa waliomzunguka kwa kupitia miradi mikubwa ya ujenzi, wakishirikiana na makandarasi na baadhi ya viongozi wa ccm! Nina uhakika na ninachokisema

hapa hamna udini mkuu! huu ni utendaji mbovu na kukosa maadili, na kuwa na wasomi wasiokomboka kielimu! mana hela zinafilisiwa kisiasa mkuu! au zimeendesha ishu gani za kidini yoyote mkuu? unakosea! wakulaumia ni serikali isiyo makini! je?tanesco nayo udini? trl zamani kama trc na udini? fikiria vizuri mkuu!sio kitu kidogo tu tunakimbilia udini, udini tunauleta wenyewe kama ivi! na haya ni matokeo ya ufisadi ambao umeanza muda mrefu tu!sasa ndo depreciation time mkuu! kama TRA wakiboronga nao utasema ukabila? au udini? mana nao hela zinatumiwa kisiasa zaidi! kwenye kichwa chako kwa sasa vuta udini we upambanaji wa watanzania mbele! ni hayo tuu
 
This time hatukubali, hii serikali imeshaona kuwa wafanyakazi ni mazezeta, nikiacha kazi kwenye NGO nikawa mfanyabiashara niache milioni mbili zangu huko hadi miaka 55? this is stupid
 
Mzee mwenzangu, uwekezaji wa hii mifuko umekuwa na msukumo wa kisiasa sana. Kuna pressure kubwa kutoka kwa wanasiasa na sasa tumepatikana. Kila mfuko una matatizo yake lakini NSSF una matatizo zaidi when it comes to investment. Ukitaka kucheka, tafuta list ya board members wa WAMA!

Yaani hasira nisije pita kwenye screen bure! Kwa ufupi ni kwamba sector nzima ya pension funds hapa bongo inahitaji overall! 1.
1. Na hii kazi SSRA hawaiwezi! Mana walifeli hata kabla hawajaanza! - kwa kukubali Kuwa regulated na BoT na wizara ya kazi - siasa!
2. Sihitaji ku over emphasize ni jinsi gani ma MD wa hii mifuko wana underperform, na kutuumiza.
3. Solution iliyopo ni sie wananchi tupige presha wote wamwagwe ndo tutaona uozo wao na kuikomboa future yetu.
 
This is hooliganism.mimi nafanya kazi secta binafsi,mgodi umefungwa au nimefukuzwa au mkataba umeisha.you mean nikae miaka hamsini ndio nipate pesa zangu.jamani mwenye ka idea hapa anieleweshe jamani.
 
Sheria ya mwanzo iliyounda NSSF ilisisitiza ni marufuku kwa fedha za michango ya washirik kuwekezwa katika miradi isiyo na kinga ya Serikali. Miradi ya kibiashara ikifilisika fedha za washiriki inapotea. Kwa hiyo fedha za michango zilikuwa zinawekezwa katika Goverment securities e.g Treasury Bills na Goverment long term stocks.

Kwa hiyo ni kule kukiuka haya maagizo ya guarantee kumefanya NSSF ikaribie kufilisika. Sio tu kwamba wafanyakazi watapunguzwa, bali wale wanaotegemea kulipwa fedha zao za pensheni kwa maisha yao ya uzeeni wamepoteza.

Yaani hapa ndo kle kausemi kuwa sheria ni msumeno unapotimia. Masikini kwa wale watumishi vijana wa umri wa 30s itabidi wsubiri miaka ishirini ijayo ndiyo wapate haki yo. n ikitokea wanfariki kabla ya kufikia huo umri, ndo yatajirudia yle ya watumishi wa afrika mashariki, mweeeeee! Nchi hii imekosa viongozi wenye akili kabisa kuanzia Ikulu hadi mgereza!
 
This is hooliganism.mimi nafanya kazi secta binafsi,mgodi umefungwa au nimefukuzwa au mkataba umeisha.you mean nikae miaka hamsini ndio nipate pesa zangu.jamani mwenye ka idea hapa anieleweshe jamani.

Mkuu mi naona umeelewa sema tu baada ya kuelewa ndo umechanganyikiwa!
 
nani alisema tuna haja na chuo chenye uwezo wa kudaili wanafunzi 40,000.?!!!!!!! kwa nini wasiweke mipango mizuri wakaboresha vilivyopo.................
 
ndio kwanza nina miaka 24 n mwaka m1 kazini........nitauiona kweli hiyo 55?

Hapa ndio utakapoona matumaini ya watanzania kuishi hususani vijana ni mgumu,kufika hiyo miaka 55,lakini si hivyo tu hata huko NSSF,LAPF,PPF ajira zitapungua kwa wafanyakazi wao wale walikuwa wanahusika na malipo no kazi nao wajipange,then maisha mtaani nayo yatakuwa magumu takribani kwa mkoa mmoja kama Dar ni 2Bill kila mwezi inatoka na inakuwa mtaani na waliojitoa sasa tutegemee maisha yasio na uhakika kwa vijana wanaopata kazi kwa mkatabata wa miaka miwil usubiri mpaka 55 non sense!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mwaka 1999 PPF ilipunguza wafanyakazi wengi sana na kuwa na mkakati wa kuibadilisha kuwa ya kiteknilojia zaidi yenye wafanyakazi wachache, weredi, na walio elimu sahihi ya kuendesha mfuko huo. Zoezi hili liliendeshwa hadi mwishoni mwa 2001 ambapo hadi Mkurugenzi wa Utawala Bwana D Magwiza alipunguzwa. Katika zoezi hili PPF iliwalipa wafanyakazi wake mamilioni ya pesa yalifikia mapaka Tshs 200,000,000 kwa mtu mmoja

Baada ya hapo organisation structure ilionyesha wafanyakazi wasiozidi 100.

Baada ya kuondolewa Mkurugenzi Mkuu wa wakati huo Bw. N Nsemwa na kuingia kijana rijali, W Erio, alianza kuajiri bila mpangilio na kufikia hatua ya kugombana na Mkurugenzi wa Utawala Marehemu Osca Mwachang'a na kuendelea kugombana na aliyekaimu nafasi hiyo baada kufariki Mwachang'a. Huyu aliyekaimu aliandamwa na hatimaye Bwana Erio akamfukuza kazi bwana Emanuel Kakuyu kwa kumzushia uongo (PCCB fanyieni kazi na hili).

Kutoka idadi tarajiwa ya wafanyakazi wasiozidi 100 waliopendekezwa na wataalamu wa PricewaterhouseCooper mwaka 1999, Bwana Erio kwa nia ya pendezesha na kujaza watoto wa vigogo(eg wa Musiba, lumbanga, Mbega, Jaji Kileo, Jaji Maina, Warioba, Anna Mkapa nk) idadi ilifika karibu 300 na kulazimisha kufukuza wapangaji PPF house wa ghorofa ya nane, ya tatu, ya kwanza na Mezanine ambazo zilikuwa zimekodishwa ili wafanyakazi wapate sehemu za kukaa na kufanya kazi.

Kwa kuwa uajiri ulikuwa sio kwa manufaa ya mfuko, imefikia wakati sasa wamejaa mno na sasa wametangaza kupunguza wafanyakazi (redundancy) na wanaopunguzwa watalipwa kila mtu kati ya Milioni 90 na Milioni 300 ambazo kama sio uajiri usiokuwa wa kiadilifu mfuko usingeingia gharama hizi

PCCB naomba mchunguze sababu za kuajiri watu wengi hivyo katika kipindi cha miaka mitatu tu (2009 hadi 2011) na sasa 2012 wanaliingiza shirika kwenye gharama za kupunguza na kutumia MABILIONI ya shilingi kwa tamaa zao binafsi.

PCCB iichunguze Management ya PPF kati ya 2007 na sasa na bila kuiacha BODI hasa iliyokuwa chini Kaimu Mwenyekiti wa Bodi Dr, Kapalata. Bodi hii lazima ijibu namna ilivyotumia madaraka yake vibaya.
 
Mimi ninachojua,watanzania bado hawajakubali kupata mafao eti baada ya miaka 55 au 60,mmojawapo mimi!!
Maamuzi yangu ntayatoa baada ya kikao kijacho cha Bunge
 
Mzee mwenzangu, uwekezaji wa hii mifuko umekuwa na msukumo wa kisiasa sana. Kuna pressure kubwa kutoka kwa wanasiasa na sasa tumepatikana. Kila mfuko una matatizo yake lakini NSSF una matatizo zaidi when it comes to investment. Ukitaka kucheka, tafuta list ya board members wa WAMA!

H.E. Mama Salma Kikwete
Chairperson of the Board
Hon. Mama Zakia Hamdan Meghji
Vice- Chairperson of the Board
Hon. Mama Mwanamwema Shein
Board Member
Hon. Mama Sophia Simba
Board Member
Hon. Amb. Mwanaidi Majaar Sinare
Board Member
Mama Regina Lowassa
Board Member
Mama Blandina Nyoni
Board Member
Mama Hulda S. Kibacha
Board Member

Mkuu kweli nimedhoofika,maana hata kucheka nimeshindwa..duuuh! Kweli kuna watu hawana hata huruma wala aibu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hapa hamna udini mkuu! huu ni utendaji mbovu na kukosa maadili, na kuwa na wasomi wasiokomboka kielimu! mana hela zinafilisiwa kisiasa mkuu! au zimeendesha ishu gani za kidini yoyote mkuu? unakosea! wakulaumia ni serikali isiyo makini! je?tanesco nayo udini? trl zamani kama trc na udini? fikiria vizuri mkuu!sio kitu kidogo tu tunakimbilia udini, udini tunauleta wenyewe kama ivi! na haya ni matokeo ya ufisadi ambao umeanza muda mrefu tu!sasa ndo depreciation time mkuu! kama TRA wakiboronga nao utasema ukabila? au udini? mana nao hela zinatumiwa kisiasa zaidi! kwenye kichwa chako kwa sasa vuta udini we upambanaji wa watanzania mbele! ni hayo tuu

ni kweli unachokisema mkuu, hamna suala la udini katika uongozi m'bovu, tumepandikizwa suala la udini na magamba, na sisi tunalibeba na kuliendekeza.
 
H.E. Mama Salma Kikwete
Chairperson of the Board
Hon. Mama Zakia Hamdan Meghji
Vice- Chairperson of the Board
Hon. Mama Mwanamwema Shein
Board Member
Hon. Mama Sophia Simba
Board Member
Hon. Amb. Mwanaidi Majaar Sinare
Board Member
Mama Regina Lowassa
Board Member
Mama Blandina Nyoni
Board Member
Mama Hulda S. Kibacha
Board Member

yeah hon...blah blah...hon house maid wa hon.....blah blah...damn it
 
Back
Top Bottom