mchukiaufisadi
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 546
- 193
Pole Serikali, kwenye zoezi hili la kuunganisha mifuko, ndipo mtajua madhara ya PPF kuzidisha wafanyakazi kwa sababu zilizokuwa si za msingi.Mwaka 1999 PPF ilipunguza wafanyakazi wengi sana na kuwa na mkakati wa kuibadilisha kuwa ya kiteknilojia zaidi yenye wafanyakazi wachache, weredi, na walio elimu sahihi ya kuendesha mfuko huo. Zoezi hili liliendeshwa hadi mwishoni mwa 2001 ambapo hadi Mkurugenzi wa Utawala Bwana D Magwiza alipunguzwa. Katika zoezi hili PPF iliwalipa wafanyakazi wake mamilioni ya pesa yalifikia mapaka Tshs 200,000,000 kwa mtu mmoja
Baada ya hapo organisation structure ilionyesha wafanyakazi wasiozidi 100.
Baada ya kuondolewa Mkurugenzi Mkuu wa wakati huo Bw. N Nsemwa na kuingia kijana rijali, W Erio, alianza kuajiri bila mpangilio na kufikia hatua ya kugombana na Mkurugenzi wa Utawala Marehemu Osca Mwachang'a na kuendelea kugombana na aliyekaimu nafasi hiyo baada kufariki Mwachang'a. Huyu aliyekaimu aliandamwa na hatimaye Bwana Erio akamfukuza kazi bwana Emanuel Kakuyu kwa kumzushia uongo (PCCB fanyieni kazi na hili).
Kutoka idadi tarajiwa ya wafanyakazi wasiozidi 100 waliopendekezwa na wataalamu wa PricewaterhouseCooper mwaka 1999, Bwana Erio kwa nia ya pendezesha na kujaza watoto wa vigogo(eg wa Musiba, lumbanga, Mbega, Jaji Kileo, Jaji Maina, Warioba, Anna Mkapa nk) idadi ilifika karibu 300 na kulazimisha kufukuza wapangaji PPF house wa ghorofa ya nane, ya tatu, ya kwanza na Mezanine ambazo zilikuwa zimekodishwa ili wafanyakazi wapate sehemu za kukaa na kufanya kazi.
Kwa kuwa uajiri ulikuwa sio kwa manufaa ya mfuko, imefikia wakati sasa wamejaa mno na sasa wametangaza kupunguza wafanyakazi (redundancy) na wanaopunguzwa watalipwa kila mtu kati ya Milioni 90 na Milioni 300 ambazo kama sio uajiri usiokuwa wa kiadilifu mfuko usingeingia gharama hizi
PCCB naomba mchunguze sababu za kuajiri watu wengi hivyo katika kipindi cha miaka mitatu tu (2009 hadi 2011) na sasa 2012 wanaliingiza shirika kwenye gharama za kupunguza na kutumia MABILIONI ya shilingi kwa tamaa zao binafsi.
PCCB iichunguze Management ya PPF kati ya 2007 na sasa na bila kuiacha BODI hasa iliyokuwa chini Kaimu Mwenyekiti wa Bodi Dr, Kapalata. Bodi hii lazima ijibu namna ilivyotumia madaraka yake vibaya.
A lot of money itatumika kulipa kwenye kuwapunguza.