RE: F. Mbowe mbona umetelekeza jimbo ?

RE: F. Mbowe mbona umetelekeza jimbo ?

Nakumbuka mwanzoni mwa 2010 alitangaza kuwa kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa chama atakuwa na majukumu mengi hivyo atakuwa anasaidiwa kazi zake na wabunge wa viti maalumu wa mkoa wa kilimanjaro akiwemo mtoto wa Ndesa,hadi leo sijawahi kuwaona popote HAI

Kama ana majukumu ya kichama si bora aachie ubunge tunahitaji mbunge serious na si maneno matupu. Hatujamchagua Lucy Owenya tumemchagua Mbowe aliyetafuta ubunge kwa mbwe mbwe na nguvu nyingi huku akitoa ahadi lukuki
 
Mi ni mwana CDM na siandiki kwa ushabiki bali kilio cha kweli. Na ninaandika kwa sababu sina njia nyingine ya kumweleza mbunge wangu.
Sitaki niingie kwenye majungu bali nataka nimkumbushe Mbunge wangu wa Hai Mh .Freeman Mbowe kuhusu kwa nini tulimchagua na yeye mwenyewe atueleze kwanini hajatutendea haki wapiga kura wake.
Nataka nimweleze kuwa tulimchagua atusaidie kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kwenye upande wa miundombinu, Elimu, maji n.k.

Mh. Mbunge wangu umetutelekeza na haya siyo majungu sisi tuna majonzi kwa jinsi ambavyo umekaa mbali na kutuacha tukiteseka.
Kwa leo naongelea tu jambo moja la miundombinu ya barabara:
Barabara zote za Kata ya Machame Mashariki sehemu za Lyamungo Kilanya, Sinde, na kati ziko taabani nitataja chache;
1. Maili sita Narumu hadi Kijiweni hali ya barabara ni mbaya na ni mashimo matupu na barabara haipitiki.
2. Kijiweni hadi kwa Elitira Mengi barabara ni mbovu mno haipitiki ni mashimo haswa eneo la Kwa akina Matinga, kwa Hans Kileo hali ni Mbaya na watu wamekata tamaa. Daraja la mto weruweru linaloonganisha Lyamungo na Nkuu tangu liharibiwe na mafuriko na kuharibu vyuma vya pembeni liko katika hali ya hatari.
Humo humo maeneo ya mtoni upande wa Lyamungo mahali ilipotokea land slide barabara inakaribia kufungwa kwani tumeshindwa kupata msaada wa kupasua mawe yaliyoanguka na kuifanya barabara kuwa nyembamba.
Mbunge ulitembelea daraja la wereweru na kuahidi kulifanyia ukarabati lakini hadi leo hii hujatimiza ahadi yako.
3. Barabara ya kutoka Nkuu Ndoo na kuunganisha na ya Kimbushi kwenda Uduru iko katika hali mbaya ni mashimo na inapitika ilimradi.
Barabara ya Kijiweni hadi Kilanya na makeresho ni mashimo matupu hali inayosababisha usafiri wa kufika kituo cha afya Umburi kuwa shida kabisa.
Ninajua mwaka huu hujafika kabisa

Tunajiuliza maswali je kwa nini umetutelekeza kata hizi za Machame mashariki, Machame kati?
Mbunge jirani yetu wa Moshi Vijijini Mh Cyril Chami anamalizia barabara zake kwa kasi ya ajabu na mbaya zaidi zinaishia mpakani mwa jimbo lako Mr. Mbowe. Na hili linatupa maumivu zaidi.
Kuna tatizo gani mheshimiwa mbona umetutelekeza au umeamua hiki kiwe kipindi chako cha mwisho na kwamba hutarudi tena kuomba kura?.

Mkuu ungekuwa unafika jimboni kuitisha mikutano haya maswali yangeishia kwenye mikutano lakini imekuwa siyo riziki hatukuoni zaidi ya pale Bungeni kupitia TV.

Naomba uelewe miundo mbinu imekuwa mibovu kuliko kipindi cha mbunge awaye yeyote na sijui kwa nini au ni kwa sababu wewe umejaliwa chombo cha kuruka angani hukanyagi huku chini ukaonja joto ya mashimo!
Hatutaki kufanya haraka kukuita mbunge jina kwani inawezekana umeshaweka mikakati inayosubiri utekelezaji. Hakuna mtu anaamini eti mbunge hajui ubovu wa barabara katika jimbo lake huku akijua umebaki mwaka mmoja atahitaji kufanya kampeni kupitia barabara hizo hizo ambazo kama hazitatengenezwa zitakuwa hazipo kabisa.

Mimi nimetumwa na sina hobby ya uongozi wa aina yoyote katika chama chochote bali maendeleo.

nI JUZI TU ALIKUWA ZIARANI HAI
 
Bora hii mada imeletwa hapa jamvini nami nilitaka kuileta long time lakini nashukuru uzalendo wa wote mliochangia kwani hata mimi ni mwadhirika wa uvivu na uzembe wa Mbunge wetu wa Hai Freeman Mbowe.

Huyu Mh. asitegemee kurudi 2015 kutudanganya na maneno matamu kwani hakuna atakaye msikiliza, Utafikiri Hai hatuna Mbunge. majimbo yaliyopakana naye ;jimbo la Siha la mhe. Aggrey Mwanri na Jimbo la Mh. Cyril Chami la Moshi Vijijini unaweza kuona dalili za kuwa na kiongozi wa wananchi lakini si Hai.
Hata wanafunzi wa shule za msingi ukiwauliza Mbunge wa Hai ni nani wanasema Novatus Makunga.

Mkuu wa wilaya anatembelea vijijini kuliko mtu yeyote huku Mbowe akipaa na Ukawa bara na visiwani.
 
Mbowe utaweza wapi masuala ya kitaifa wakati madogo ya Kijimbo yanaonekana kukuelemea broo. Tumekuangalia tukifikiri utarudi jimboni lakini inaonekana no back turn na huku ni kujisau.
Na ukiendelea hivi kuna kila dalili kuua upinzani maeneo ya vijijini kwani hawaoni ulichofanya na hivyo kuamua kuwa na mawazo mbadala.
 
[h=2]MBOWE ATEMBELEA JIMBO LAKE KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO[/h] Posted by Woinde Shizza at 6/10/2014 05:21:00 PM

​

Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwa pamoja na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), wakikagua Dara la Marire, Iwala, ikiwa ni sehemu ya ziara anayofanya kwa ajili ya kufanya tathmini ya miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo inahitaji kupata msukumo wa kuongezewa nguvu za ujenzi na mfuko huo ambao yeye ni mwenyekiti wake.
​
​
Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF) wakikagua moja ya jengo linalopaswa kuwa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Tindigani, ikiwa ni sehemu ya ziara kwa ajili ya kufanya tathmini ya mahitaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayohitaji kuongezewa msukumo na mfuko huo ambao yeye ni mwenyekiti wake.
 
[h=3]Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Ashiriki Zoezi la upandaji wa miti pamoja na kufanya usafi wa mazingira eneo la Bomang'ombe Hai[/h]

​

CIMG0552.JPG
​
CIMG0546.JPG
Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (katika aliyevaa gwanda) akisisitiza jambo akiwa na wanachama wa kikundi cha kijamii cha Chembe Kidevu ambacho kilizinduzi katiba yake ambapo zoezi hilo lilienda sambamba na upandaji wa miti pamoja na kufanya usafi wa mazingira eneo la Bomang'ombe Hai,Picha na Rodrick Mushi. ​

​
 
[h=2]MBOWE ATEMBELEA JIMBO LAKE KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO[/h] Posted by Woinde Shizza at 6/10/2014 05:21:00 PM

​

Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwa pamoja na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), wakikagua Dara la Marire, Iwala, ikiwa ni sehemu ya ziara anayofanya kwa ajili ya kufanya tathmini ya miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo inahitaji kupata msukumo wa kuongezewa nguvu za ujenzi na mfuko huo ambao yeye ni mwenyekiti wake.
​
​
Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF) wakikagua moja ya jengo linalopaswa kuwa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Tindigani, ikiwa ni sehemu ya ziara kwa ajili ya kufanya tathmini ya mahitaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayohitaji kuongezewa msukumo na mfuko huo ambao yeye ni mwenyekiti wake.

Mkuu Mzito Kabwela wewe siyo wa kwanza kuziona hizi picha na hazitusaidii lolote, umewasikia wana Jimbo hapa Jf wanavyoelekeza lawama kwa mbunge wao.

Sasa unadhani hizo picha ndiyo zitatoa majibu? Tukio gani katika hizo picha limeonyesha umahiri wa Mbowe na asirushiwe lawama?

2015 siyo mbali na vita hii itaanzia hapa Jf hadi Jimboni asipojirudi.
 
Last edited by a moderator:

Mleta mada ameandika hivi....

[h=1]RE: F. Mbowe mbona umetelekeza jimbo ?[/h]
Sasa hizo picha zimejibu swali au bado? Kama bado sema ni wapi hazijajibu tukujibu.
 
Msalani nafikiri Pale Lumumba wamekupandisha Cheo sana, Mbowe Mbona hata juzi alikuwa ziarani kwenye Jimbo lake? wacheni Majungu na Fitna
 
Mkuu. Mzito Kabwela :
kama unataka kumtetea mbunge wetu anza kwa kutuonesha maendeleo aliyoyaleta sio kuonyesha picha za mikutano na ziara.
_
ziara mtu yeyote anaweza kufanya hata wewe.
_Angalia vijiji vya uswaa,shari na kyeri kijografia vimegawanywa na mto kikafu na mto marire hiyo mito ina mabonde makubwa mno!
Hakuna huduma ya zahanati katika hivyo vijiji japo majengo yapo,mbunge ameshawahi kuchukua hatua gani?
 
Last edited by a moderator:
Wacha fitna na Majungu Kijana Majungu si Mtaji ufaidike mbona Juzi tulikua nae kwenye ziara Jimboni kwake? Wacheni kupewa vihela visivyo na Mahana hapo Lumumba ili mchonge story Poor ccm
 
Dr. Chami ni nani? mm niko moshi vijijini huyu mtu hajulikani aliko,,
 
Naomba kuongezea...
1.Barabara inayounganisha vijiji vya wakulima vya mijongweni, weruweru, kiyungi, chekereni kupitia Bonite Bottlers hadi moshi mjini ina mashimo,vumbi na haipitiki ..Bararbara hii imemshinda katka vipindi vyote alivyokuwa mbunge.
 
Mkuu. Mzito Kabwela :
kama unataka kumtetea mbunge wetu anza kwa kutuonesha maendeleo aliyoyaleta sio kuonyesha picha za mikutano na ziara.
_
ziara mtu yeyote anaweza kufanya hata wewe.
_Angalia vijiji vya uswaa,shari na kyeri kijografia vimegawanywa na mto kikafu na mto marire hiyo mito ina mabonde makubwa mno!
Hakuna huduma ya zahanati katika hivyo vijiji japo majengo yapo,mbunge ameshawahi kuchukua hatua gani?
We mgonjwa! kwani kazi ya mbunge ni kujenga zahanati? Kumbe serikali inayotoza kodi kazi yake nini?
 
Wacha fitna na Majungu Kijana Majungu si Mtaji ufaidike mbona Juzi tulikua nae kwenye ziara Jimboni kwake? Wacheni kupewa vihela visivyo na Mahana hapo Lumumba ili mchonge story Poor ccm

Mkuu katika hili hata utuite majina gani lazima tuseme maana sisi ndiyo tunaojua kinachoendelea katika Jimbo letu.

Mh Mbowe kila uchaguzi nampa kura yangu lazima awajibike kwa wananchi waliomchagua.
 
Nakushanga sana Maana kwenye ziara nakuwepo na mimi nimoja wapo hakuna dhambi mbaya duniani kama ya kusema wongo angalia dhambi hiyo isije kukutafuna
 
Back
Top Bottom