RE: F. Mbowe mbona umetelekeza jimbo ?

RE: F. Mbowe mbona umetelekeza jimbo ?

Mi ni mwana CDM na siandiki kwa ushabiki bali kilio cha kweli. Na ninaandika kwa sababu sina njia nyingine ya kumweleza mbunge wangu.
Sitaki niingie kwenye majungu bali nataka nimkumbushe Mbunge wangu wa Hai Mh .Freeman Mbowe kuhusu kwa nini tulimchagua na yeye mwenyewe atueleze kwanini hajatutendea haki wapiga kura wake.
Nataka nimweleze kuwa tulimchagua atusaidie kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kwenye upande wa miundombinu, Elimu, maji n.k.

Mh. Mbunge wangu umetutelekeza na haya siyo majungu sisi tuna majonzi kwa jinsi ambavyo umekaa mbali na kutuacha tukiteseka.
Kwa leo naongelea tu jambo moja la miundombinu ya barabara:
Barabara zote za Kata ya Machame Mashariki sehemu za Lyamungo Kilanya, Sinde, na kati ziko taabani nitataja chache;
1. Maili sita Narumu hadi Kijiweni hali ya barabara ni mbaya na ni mashimo matupu na barabara haipitiki.
2. Kijiweni hadi kwa Elitira Mengi barabara ni mbovu mno haipitiki ni mashimo haswa eneo la Kwa akina Matinga, kwa Hans Kileo hali ni Mbaya na watu wamekata tamaa. Daraja la mto weruweru linaloonganisha Lyamungo na Nkuu tangu liharibiwe na mafuriko na kuharibu vyuma vya pembeni liko katika hali ya hatari.
Humo humo maeneo ya mtoni upande wa Lyamungo mahali ilipotokea land slide barabara inakaribia kufungwa kwani tumeshindwa kupata msaada wa kupasua mawe yaliyoanguka na kuifanya barabara kuwa nyembamba.
Mbunge ulitembelea daraja la wereweru na kuahidi kulifanyia ukarabati lakini hadi leo hii hujatimiza ahadi yako.
3. Barabara ya kutoka Nkuu Ndoo na kuunganisha na ya Kimbushi kwenda Uduru iko katika hali mbaya ni mashimo na inapitika ilimradi.
Barabara ya Kijiweni hadi Kilanya na makeresho ni mashimo matupu hali inayosababisha usafiri wa kufika kituo cha afya Umburi kuwa shida kabisa.
Ninajua mwaka huu hujafika kabisa

Tunajiuliza maswali je kwa nini umetutelekeza kata hizi za Machame mashariki, Machame kati?
Mbunge jirani yetu wa Moshi Vijijini Mh Cyril Chami anamalizia barabara zake kwa kasi ya ajabu na mbaya zaidi zinaishia mpakani mwa jimbo lako Mr. Mbowe. Na hili linatupa maumivu zaidi.
Kuna tatizo gani mheshimiwa mbona umetutelekeza au umeamua hiki kiwe kipindi chako cha mwisho na kwamba hutarudi tena kuomba kura?.

Mkuu ungekuwa unafika jimboni kuitisha mikutano haya maswali yangeishia kwenye mikutano lakini imekuwa siyo riziki hatukuoni zaidi ya pale Bungeni kupitia TV.

Naomba uelewe miundo mbinu imekuwa mibovu kuliko kipindi cha mbunge awaye yeyote na sijui kwa nini au ni kwa sababu wewe umejaliwa chombo cha kuruka angani hukanyagi huku chini ukaonja joto ya mashimo!
Hatutaki kufanya haraka kukuita mbunge jina kwani inawezekana umeshaweka mikakati inayosubiri utekelezaji. Hakuna mtu anaamini eti mbunge hajui ubovu wa barabara katika jimbo lake huku akijua umebaki mwaka mmoja atahitaji kufanya kampeni kupitia barabara hizo hizo ambazo kama hazitatengenezwa zitakuwa hazipo kabisa.

Mimi nimetumwa na sina hobby ya uongozi wa aina yoyote katika chama chochote bali maendeleo.

[h=2]ZIARA YA MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYANI HAI[/h]Posted by Woinde Shizza at 5/13/2014 12:59:00 PM

[TABLE="class: tr-caption-container, width: 100%, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Hai, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa chama hicho Kijiji cha Mtakuja, Mzee Ally Mbatia. Mbowe yuko katika ziara ya kukagua uhai na kuimarisha ujenzi wa chama katika ngazi ya chini kabisa ya chama hicho, msingi, kwenye maeneo ya vitongoji mbalimbali katika vijiji vya Jimbo la Hai.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

​
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye. Viongozi hao walikutana juzi eneo la Bomang'ombe, wilayani Hai, kila mtu akiwa katika ziara yake. Wakati Mbowe alikuwa anaendelea na ziara ya kuzungukia wananchi latika vijiji mbalimbali jimboni kwake Hai, Medeye alikuwa katika ziara yake binafsi maeneo ya jimbo hilo.

​
c.c Mwana Kwetu kwahiyo huko sio JIMOBNI kwake???

Mkuu nakushauri kama hutoki Hai utuache sisi wenye uchungu na kura zetu na za wazazi wetu tuongee kwani hii siyo mada ya kisiasa . Tunadai committment aliyoitoa alipochukua ubunge No more

Unajuaje Mimi sio MwanaHai? Kabla ya yeye alikuwepo Mbunge wa CCM aliyoahidi alitelekeza ? Or is just the same GAME blame GAME...

Watu wa CCM hawalaumiwi... ndio wenye Majimbo Mengi nchini sasa hapo NCHI yetu si INGEKUWA BORA ? Mnahangaika na JIMBO LA HAI ambalo ukilinganisha na Majimbo Mengine lyanayoongozwa na wana CCMinaMaendeleo kupita kiasi

1. Kuna Hospitali - Machame Hospital
2. Kuna Shule - Machame GIRLS
3. Kuna chuo cha Uganga
4. Kuna hoteli safi ya kitalii
5. Kuna Barabara ya Lami
6. Kuna Maji

Sasa nenda JIMBO la JIRANI tu la Mwana CCM CYRIL CHAMI... Barabara ni VUMBI mpaka leo na ndiko alikotoka Mama Mkapa...

c.c
MVUMBUZI
 
Mkuu nakushauri kama hutoki Hai utuache sisi wenye uchungu na kura zetu na za wazazi wetu tuongee kwani hii siyo mada ya kisiasa . Tunadai committment aliyoitoa alipochukua ubunge No more

It,s true mkuu ndiyo maana tangu mwanzo nime declare interest kwamba huu uzi siyo wa kisiasa ndiyo maana ukawekwa hapa Habari Mchanganyiko.

MSALANI kanielewa bila shaka,..
 
Last edited by a moderator:

Sasa Kama ni PERSONAL VENDETTA... then It is between U and him ?? Kwanini Unaiweka DUNIA NZIMA waione kama ni hivyo???

Watanzania HATUJUI SIASA -- Tunafikiria VYAMA Vya SIASA ndio Opportunities zetu za kupata Maisha BORA; Kila mtu anakimbia FANI yake i.e UALIMU; BIASHARA; UKARANI; UDEREVA wote kwenye SIASA na IWALIPE kama haiwalipi Mnakimbilia CHAMA KINGINE...

It is a SHAME... we think POLITICS is FEEDING OUR LOUSY STOMACH...

Then who invited you in this conversation?

Mind your own business you dude,.

We only need people from HAI Constituency to discuss our matters,..
 
Hizo picha za Mbowe yuko Bomangombe ambao ni mjini, nimetaja kata za Machame Mashariki, Machame kati tena alikozaliwa Regnald Mengi barababara ni terrible. Mwezi huu nimekuwepo huko nilikotaja kwa sababu ndiko kwetu na hata leo nimetokea huko nakwambia nimepita kwa gari kwa shida mno mno. Narumu ni pot holes hakuna barabara mle
 
Then who invited you in this conversation?

Mind your own business you dude,.

We only need people from HAI Constituency to discuss our matters,..
Achana na vizabina zabina hawa wako kila mahala wakinunua kesi zisizo wahusu. Nani kamwambia Hai kuwa na Lami basi tumefikia mwisho wa kuhitaji maendeleo!.
 
Acha upuanguani kijana wala usipende kuonyesha udhaifu wako kwa watu , hapa umeandika uharo gani sasa .
Then who invited you in this conversation?

Mind your own business you dude,.

We only need people from HAI Constituency to discuss our matters,..
 
MMBUNGE HATENGENEZI BARABARA1 NI WAJIBU WA SERIKALI, KAJIFUNZE CIVICS FORM ONE NDO UJE tujadili
 
Ushauri wa bure kwa brother Freeman Mbowe ni kwamba aelewe sifa ya baba mwema ni kuitunza familia yak na siyo kuvaa suti na kuwapa watu ofa mabarabarani. Na pia mcheza kwao hutunzwa.
Aache ukamanda wa mijini akaufanyie jimboni mwake ndo tutamwelewa ili kwa sasa yuko highly disconnected na wapiga kura wake
 
Unajuaje Mimi sio MwanaHai? Kabla ya yeye alikuwepo Mbunge wa CCM aliyoahidi alitelekeza ? Or is just the same GAME blame GAME...

Watu wa CCM hawalaumiwi... ndio wenye Majimbo Mengi nchini sasa hapo NCHI yetu si INGEKUWA BORA ? Mnahangaika na JIMBO LA HAI ambalo ukilinganisha na Majimbo Mengine lyanayoongozwa na wana CCMinaMaendeleo kupita kiasi

1. Kuna Hospitali - Machame Hospital
2. Kuna Shule - Machame GIRLS
3. Kuna chuo cha Uganga
4. Kuna hoteli safi ya kitalii
5. Kuna Barabara ya Lami
6. Kuna Maji

Sasa nenda JIMBO la JIRANI tu la Mwana CCM CYRIL CHAMI... Barabara ni VUMBI mpaka leo na ndiko alikotoka Mama Mkapa...

c.c
MVUMBUZI

Acha kupiga danadana, tuambie alichokifanya Mh Mbowe jimboni HAI tangu aingie bungeni 2010.

Mwana HAI hawezi kuzungumza maneno kama unayoyasema,..

HAI unaisikia tu Bungeni au katika vyombo vya Habari na hujawahi kufika,. Wewe unadhani tunasema haya kwa kumchafua mtu na wakati sisi wenyewe ndiyo tuliyemchagua?

Lazima tumfanyie assesment tuangalie ni kitu alichotufanyia na kama hajafanya chochote adhabu yake anaijua,...
 
MMBUNGE HATENGENEZI BARABARA1 NI WAJIBU WA SERIKALI, KAJIFUNZE CIVICS FORM ONE NDO UJE tujadili

Who is to mobilize, who is to initiate and who is to voice the voiceless voices!!!!! . Dogo nenda chekechea sitaki nifafanue. Tunajua hawezi chimba barabara yeye siyo bulldozer, hawezi piga msumari yeye siyo fundi seremala lakini anaweze piga kelele resources zikawa mobilised kufanya kazi ya ukarabati wa barabara nk.
 
Hivi mnataka Mbowe awafanyie nini jamani leo hii mnalinganisha jimbo lenu na jimbo la Chami ? Nabii kweli hakubaliki kwao.
Ushauri wa bure kwa brother Freeman Mbowe ni kwamba aelewe sifa ya baba mwema ni kuitunza familia yak na siyo kuvaa suti na kuwapa watu ofa mabarabarani. Na pia mcheza kwao hutunzwa.
Aache ukamanda wa mijini akaufanyie jimboni mwake ndo tutamwelewa ili kwa sasa yuko highly disconnected na wapiga kura wake
 
Yes Mbowe nafikiri hajafanya lolote la maana hata mikutano hafanyi na hajui kero za wananchi amebaki kuruka juju kwa juu. Mi natoka maeneo aliyosema mtoa mada ni kweli ameshindwa sijui next year atakuj kuwaambia nini wananchi na inabidi ajue wana usongo naye

Ni kweli aise hali ni tete wakati kwa Chami kuna lami anamalzia na inaishia mpakani
 
Hivi mnataka Mbowe awafanyie nini jamani leo hii mnalinganisha jimbo lenu na jimbo la Chami ? Nabii kweli hakubaliki kwao.

Mkuu usitufananishe na wengine, tulitakiwa tuwe mbali sana,.

Haya tuambie tangu Mh Mbowe tumchague kuwa mbunge wa Jimbo la HAI kafanya nini?

Usiwe unadakia usilolijua,. Sisi ndiyo tuliemchagua na tunataka atupe majibu ya kuridhisha.
 
Mbowe please came back home waliokutuma bungeni wanakutafuta!!!!
 
Hizo picha za Mbowe yuko Bomangombe ambao ni mjini, nimetaja kata za Machame Mashariki, Machame kati tena alikozaliwa Regnald Mengi barababara ni terrible. Mwezi huu nimekuwepo huko nilikotaja kwa sababu ndiko kwetu na hata leo nimetokea huko nakwambia nimepita kwa gari kwa shida mno mno. Narumu ni pot holes hakuna barabara mle

Tena narumu ndo.usiseme na maeneo ya kupita daraja kuanzia kwa Matinga hadi darajani ukichangia na ile land slide pale kupitika ni shda
 
Back
Top Bottom