RE: F. Mbowe mbona umetelekeza jimbo ?

RE: F. Mbowe mbona umetelekeza jimbo ?

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
652
Reaction score
607
Mi ni mwana CDM na siandiki kwa ushabiki bali kilio cha kweli. Na ninaandika kwa sababu sina njia nyingine ya kumweleza mbunge wangu.

Sitaki niingie kwenye majungu bali nataka nimkumbushe Mbunge wangu wa Hai Mh .Freeman Mbowe kuhusu kwa nini tulimchagua na yeye mwenyewe atueleze kwanini hajatutendea haki wapiga kura wake.

Nataka nimweleze kuwa tulimchagua atusaidie kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kwenye upande wa miundombinu, Elimu, maji n.k.

Mh. Mbunge wangu umetutelekeza na haya siyo majungu sisi tuna majonzi kwa jinsi ambavyo umekaa mbali na kutuacha tukiteseka.
Kwa leo naongelea tu jambo moja la miundombinu ya barabara:

Barabara zote za Kata ya Machame Mashariki sehemu za Lyamungo Kilanya, Sinde, na kati ziko taabani nitataja chache;

1. Maili sita Narumu hadi Kijiweni hali ya barabara ni mbaya na ni mashimo matupu na barabara haipitiki.

2. Kijiweni hadi kwa Elitira Mengi barabara ni mbovu mno haipitiki ni mashimo haswa eneo la Kwa akina Matinga, kwa Hans Kileo hali ni Mbaya na watu wamekata tamaa. Daraja la mto weruweru linaloonganisha Lyamungo na Nkuu tangu liharibiwe na mafuriko na kuharibu vyuma vya pembeni liko katika hali ya hatari.

Humo humo maeneo ya mtoni upande wa Lyamungo mahali ilipotokea land slide barabara inakaribia kufungwa kwani tumeshindwa kupata msaada wa kupasua mawe yaliyoanguka na kuifanya barabara kuwa nyembamba.

Mbunge ulitembelea daraja la wereweru na kuahidi kulifanyia ukarabati lakini hadi leo hii hujatimiza ahadi yako.

3. Barabara ya kutoka Nkuu Ndoo na kuunganisha na ya Kimbushi kwenda Uduru iko katika hali mbaya ni mashimo na inapitika ilimradi.

Barabara ya Kijiweni hadi Kilanya na makeresho ni mashimo matupu hali inayosababisha usafiri wa kufika kituo cha afya Umburi kuwa shida kabisa.

Ninajua mwaka huu hujafika kabisa.

Tunajiuliza maswali je kwa nini umetutelekeza kata hizi za Machame mashariki, Machame kati?

Mbunge jirani yetu wa Moshi Vijijini Mh Cyril Chami anamalizia barabara zake kwa kasi ya ajabu na mbaya zaidi zinaishia mpakani mwa jimbo lako Mr. Mbowe. Na hili linatupa maumivu zaidi.

Kuna tatizo gani mheshimiwa mbona umetutelekeza au umeamua hiki kiwe kipindi chako cha mwisho na kwamba hutarudi tena kuomba kura?.

Mkuu ungekuwa unafika jimboni kuitisha mikutano haya maswali yangeishia kwenye mikutano lakini imekuwa siyo riziki hatukuoni zaidi ya pale Bungeni kupitia TV.

Naomba uelewe miundo mbinu imekuwa mibovu kuliko kipindi cha mbunge awaye yeyote na sijui kwa nini au ni kwa sababu wewe umejaliwa chombo cha kuruka angani hukanyagi huku chini ukaonja joto ya mashimo!

Hatutaki kufanya haraka kukuita mbunge jina kwani inawezekana umeshaweka mikakati inayosubiri utekelezaji.

Hakuna mtu anaamini eti mbunge hajui ubovu wa barabara katika jimbo lake huku akijua umebaki mwaka mmoja atahitaji kufanya kampeni kupitia barabara hizo hizo ambazo kama hazitatengenezwa zitakuwa hazipo kabisa.

Mimi nimetumwa na sina hobby ya uongozi wa aina yoyote katika chama chochote bali maendeleo.
 
mkuu utatukanwa hadi basi wanachadema watakuambia mbunge hakusanyi kodi
je kama mbunge hakusanyi kodi kwanini tuendelee kumchagua?
_Nilishawahi kumwambia mbowe,vijiji vya USWAA,SHARI NA KYERI hazina huduma nzuri ya zahanati wala mochori ila hakunielewa hadi siku ya kura
 
Namshukuru mleta mada,..Nilitaka kuanzisha Uzi na mimi nitoe yangu ya moyoni,.

Mh . Mbowe naona kasahau nyumbani kabisa!!

Kuna wakati unafika tunasema afadhali angebakia Mh . Fuya ingawa alikuwa CCM.
 
mh. freeman Mbowe utajisifu kwa maendeleo gani kwa wana hai?
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hakuna kitu, naona wananchi wameamka na makosa hayatafanyika tena.

wanasema kabanwa na majukumu ya chama kitaifa!
 
Last edited by a moderator:
Namshukuru mleta mada,..Nilitaka kuanzisha Uzi na mimi nitoe yangu ya moyoni,.

Mh . Mbowe naona kasahau nyumbani kabisa!!

Kuna wakati unafika tunasema afadhali angebakia Mh . Fuya ingawa alikuwa CCM.

Yes Mbowe nafikiri hajafanya lolote la maana hata mikutano hafanyi na hajui kero za wananchi amebaki kuruka juju kwa juu. Mi natoka maeneo aliyosema mtoa mada ni kweli ameshindwa sijui next year atakuj kuwaambia nini wananchi na inabidi ajue wana usongo naye
 
Mbowe ni mmoja wa wabunge wa CHADEMA ambao 2015 hawatachaguliwa tena. Ni mmoja wa wabunge walioshindwa kutekeleza angalau moja tu ya ahadi zao walizotoa kwa wananchi mwaka 2010.
Wengine ambao bunge watalisikia tu ni:
  1. Tundu Lissu
  2. Halima Mdee
  3. Godbless Lema
  4. John Mnyika
  5. Joseph Mbilinyi
  6. Mch. Msigwa

etc...
 
Mi ni mwana CDM na siandiki kwa ushabiki bali kilio cha kweli. Na ninaandika kwa sababu sina njia nyingine ya kumweleza mbunge wangu.
Sitaki niingie kwenye majungu bali nataka nimkumbushe Mbunge wangu wa Hai Mh .Freeman Mbowe kuhusu kwa nini tulimchagua na yeye mwenyewe atueleze kwanini hajatutendea haki wapiga kura wake.
Nataka nimweleze kuwa tulimchagua atusaidie kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kwenye upande wa miundombinu, Elimu, maji n.k.

Mh. Mbunge wangu umetutelekeza na haya siyo majungu sisi tuna majonzi kwa jinsi ambavyo umekaa mbali na kutuacha tukiteseka.
Kwa leo naongelea tu jambo moja la miundombinu ya barabara:
Barabara zote za Kata ya Machame Mashariki sehemu za Lyamungo Kilanya, Sinde, na kati ziko taabani nitataja chache;
1. Maili sita Narumu hadi Kijiweni hali ya barabara ni mbaya na ni mashimo matupu na barabara haipitiki.
2. Kijiweni hadi kwa Elitira Mengi barabara ni mbovu mno haipitiki ni mashimo haswa eneo la Kwa akina Matinga, kwa Hans Kileo hali ni Mbaya na watu wamekata tamaa. Daraja la mto weruweru linaloonganisha Lyamungo na Nkuu tangu liharibiwe na mafuriko na kuharibu vyuma vya pembeni liko katika hali ya hatari.
Humo humo maeneo ya mtoni upande wa Lyamungo mahali ilipotokea land slide barabara inakaribia kufungwa kwani tumeshindwa kupata msaada wa kupasua mawe yaliyoanguka na kuifanya barabara kuwa nyembamba.
Mbunge ulitembelea daraja la wereweru na kuahidi kulifanyia ukarabati lakini hadi leo hii hujatimiza ahadi yako.
3. Barabara ya kutoka Nkuu Ndoo na kuunganisha na ya Kimbushi kwenda Uduru iko katika hali mbaya ni mashimo na inapitika ilimradi.
Barabara ya Kijiweni hadi Kilanya na makeresho ni mashimo matupu hali inayosababisha usafiri wa kufika kituo cha afya Umburi kuwa shida kabisa.
Ninajua mwaka huu hujafika kabisa

Tunajiuliza maswali je kwa nini umetutelekeza kata hizi za Machame mashariki, Machame kati?
Mbunge jirani yetu wa Moshi Vijijini Mh Cyril Chami anamalizia barabara zake kwa kasi ya ajabu na mbaya zaidi zinaishia mpakani mwa jimbo lako Mr. Mbowe. Na hili linatupa maumivu zaidi.
Kuna tatizo gani mheshimiwa mbona umetutelekeza au umeamua hiki kiwe kipindi chako cha mwisho na kwamba hutarudi tena kuomba kura?.

Mkuu ungekuwa unafika jimboni kuitisha mikutano haya maswali yangeishia kwenye mikutano lakini imekuwa siyo riziki hatukuoni zaidi ya pale Bungeni kupitia TV.

Naomba uelewe miundo mbinu imekuwa mibovu kuliko kipindi cha mbunge awaye yeyote na sijui kwa nini au ni kwa sababu wewe umejaliwa chombo cha kuruka angani hukanyagi huku chini ukaonja joto ya mashimo!
Hatutaki kufanya haraka kukuita mbunge jina kwani inawezekana umeshaweka mikakati inayosubiri utekelezaji. Hakuna mtu anaamini eti mbunge hajui ubovu wa barabara katika jimbo lake huku akijua umebaki mwaka mmoja atahitaji kufanya kampeni kupitia barabara hizo hizo ambazo kama hazitatengenezwa zitakuwa hazipo kabisa.

Mimi nimetumwa na sina hobby ya uongozi wa aina yoyote katika chama chochote bali maendeleo.

LABDA Unahitaji UONGEZEWE Per.DEM - LUMUMBA hivi hivi Maisha Magumu angalia picha...
Mimi sio CHADEMA nimeona hii toka kwenye WebSite yao nikaona nikusaidie wewe MwanaCHADEMA

[h=2]SATURDAY, JUNE 7, 2014[/h][h=3]TASWIRA- MWENYEKITI WA CHADEMA MH FREEMAN MBOWE AKIWA ZIARANI JIMBONI HAI[/h]

Picha 1&2
Mmoja wa Wanakamati wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo (CDF) Jimbo la Hai akipanga kuni katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Shirimatunda iliyoko wilayani Hai, wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe (Mbunge wa Hai), alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo mfuko huo utasaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Chumba hicho mbali ya kutumika na wanafunzi kwa ajili ya kusomea, pia kinatumika kama stoo ya kuni za kupikia chakula cha wanafunzi shuleni hapo, hali ambayo inadhihirisha kuwepo kwa mahitaji ya vyumba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Picha 3&4

Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akishuhudia uharibifu kwenye moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Weruweru iliyoko wilayani Hai, ikiwa ni sehemu ya ziara yake anayofanya pamoja na kamati yake ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), kwa ajili ya kutathmini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake ili mfuko huo uweze kusaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko huo alielezwa kuwa shimo hilo limekuwa likitumika na wananchi waovu kama 'mlango' wa kuingia na kutoka kwa ajili ya kuiba kuni zinazotunzwa katika chumba hicho cha darasa.

Posted by Chadema Blogtz at 8:14 PM
 
Mbowe ni mmoja wa wabunge wa CHADEMA ambao 2015 hawatachaguliwa tena. Ni mmoja wa wabunge walioshindwa kutekeleza angalau moja tu ya ahadi zao walizotoa kwa wananchi mwaka 2010.
Wengine ambao bunge watalisikia tu ni:
  1. Tundu Lissu
  2. Halima Mdee
  3. Godbless Lema
  4. John Mnyika
  5. Joseph Mbilinyi
  6. Mch. Msigwa

etc...

Mkuu MSALANI pole sana, huu uzi haujakaa kisiasa hata kidogo,

Hapa tunamjadili Mh Mbowe na Jimbo lake la HAI,. hao wengine uliowataja labda una chuki binafsi nao:

Hawatuhusu sisi,.

Hapa tunamjadili mbunge wetu Mbowe na Jimbo Letu!
 
Last edited by a moderator:

LABDA Unahitaji UONGEZEWE Per.DEM - LUMUMBA hivi hivi Maisha Magumu angalia picha...
Mimi sio CHADEMA nimeona hii toka kwenye WebSite yao nikaona nikusaidie wewe MwanaCHADEMA

SATURDAY, JUNE 7, 2014

TASWIRA- MWENYEKITI WA CHADEMA MH FREEMAN MBOWE AKIWA ZIARANI JIMBONI HAI

Picha 1&2
Mmoja wa Wanakamati wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo (CDF) Jimbo la Hai akipanga kuni katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Shirimatunda iliyoko wilayani Hai, wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe (Mbunge wa Hai), alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo mfuko huo utasaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Chumba hicho mbali ya kutumika na wanafunzi kwa ajili ya kusomea, pia kinatumika kama stoo ya kuni za kupikia chakula cha wanafunzi shuleni hapo, hali ambayo inadhihirisha kuwepo kwa mahitaji ya vyumba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Picha 3&4

Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akishuhudia uharibifu kwenye moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Weruweru iliyoko wilayani Hai, ikiwa ni sehemu ya ziara yake anayofanya pamoja na kamati yake ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), kwa ajili ya kutathmini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake ili mfuko huo uweze kusaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko huo alielezwa kuwa shimo hilo limekuwa likitumika na wananchi waovu kama 'mlango' wa kuingia na kutoka kwa ajili ya kuiba kuni zinazotunzwa katika chumba hicho cha darasa.

Posted by Chadema Blogtz at 8:14 PM

Wewe nenda kamwulize Mbowe mwenyewe kama malalamiko niliyotoa ni batili au ni kweli. Yeye mwenyewe anajua huko nilikokutaja hajakanyaga mwaka mzima na hali ni mbaya. Hakuna cha Lumumba hapa kwa sababu lengo si kupakana matope bali kumshtua usingizini
 
Mbowe ni mmoja wa wabunge wa CHADEMA ambao 2015 hawatachaguliwa tena. Ni mmoja wa wabunge walioshindwa kutekeleza angalau moja tu ya ahadi zao walizotoa kwa wananchi mwaka 2010.
Wengine ambao bunge watalisikia tu ni:
  1. Tundu Lissu
  2. Halima Mdee
  3. Godbless Lema
  4. John Mnyika
  5. Joseph Mbilinyi
  6. Mch. Msigwa

etc...

Umesahau Majina yafuatayo;
a. Riz Kikwete
b. January Makamba
c. Kingunge Ngombale Mwiru

e.t.c
 
Mkuu MSALANI pole sana, huu uzi haujakaa kisiasa hata kidogo,

Hapa tunamjadili Mh Mbowe na Jimbo lake la HAI,. hao wengine uliowataja labda una chuki binafsi nao:

Hawatuhusu sisi,.

Hapa tunamjadili mbunge wetu Mbowe na Jimbo Letu!

Mkuu Chakii you're quite right. Mbowe namfananisha na mtu anayetokezea barabarani akiwa amevaa suti lakini nyumbani analala sakafuni. Sisi ndio tuliomfanya aonekane, aheshimiwe na kuaminiwa pale bungeni lakini ametutelekeza kabisa. Hatuhitaji fedha zake kwanza hawezi kunilipa bali tunahitaji awajibike kutuletea maendeleo kwa sababu aliji commit
 
Wana Hai tuamke tulipo tumdai huyu ndugu yale aliyo ahidi la sivyo tunauziwa mbuzi kwenye gunia
 
Wewe nenda kamwulize Mbowe mwenyewe kama malalamiko niliyotoa ni batili au ni kweli. Yeye mwenyewe anajua huko nilikokutaja hajakanyaga mwaka mzima na hali ni mbaya. Hakuna cha Lumumba hapa kwa sababu lengo si kupakana matope bali kumshtua usingizini

Sasa Kama ni PERSONAL VENDETTA... then It is between U and him ?? Kwanini Unaiweka DUNIA NZIMA waione kama ni hivyo???

Watanzania HATUJUI SIASA -- Tunafikiria VYAMA Vya SIASA ndio Opportunities zetu za kupata Maisha BORA; Kila mtu anakimbia FANI yake i.e UALIMU; BIASHARA; UKARANI; UDEREVA wote kwenye SIASA na IWALIPE kama haiwalipi Mnakimbilia CHAMA KINGINE...

It is a SHAME... we think POLITICS is FEEDING OUR LOUSY STOMACH...
 
Mkuu Chakii you're quite right. Mbowe namfananisha na mtu anayetokezea barabarani akiwa amevaa suti lakini nyumbani analala sakafuni. Sisi ndio tuliomfanya aonekane, aheshimiwe na kuaminiwa pale bungeni lakini ametutelekeza kabisa. Hatuhitaji fedha zake kwanza hawezi kunilipa bali tunahitaji awajibike kutuletea maendeleo kwa sababu aliji commit

Mkuu Mwana Kwetu Mh Mbowe nilimpata kura yangu na mpaka sasa sijaona chochote alichowafanyia wana HAI miaka nenda rudi? Mzee Fuya tulimdharau lakini he did something kiukweli,.
 
Last edited by a moderator:
Mbowe ni mmoja wa wabunge wa CHADEMA ambao 2015 hawatachaguliwa tena. Ni mmoja wa wabunge walioshindwa kutekeleza angalau moja tu ya ahadi zao walizotoa kwa wananchi mwaka 2010.
Wengine ambao bunge watalisikia tu ni:
  1. Tundu Lissu
  2. Halima Mdee
  3. Godbless Lema
  4. John Mnyika
  5. Joseph Mbilinyi
  6. Mch. Msigwa

etc...

jamani wananchi chonde chonde msiwa delete wote,tutakosa waigizaji bungeni mi nshazoea kuwaona bungeni wakizomea na kuigiza,mtanikosesha raha jamani!
 
Sasa Kama ni PERSONAL VENDETTA... then It is between U and him ?? Kwanini Unaiweka DUNIA NZIMA waione kama ni hivyo???

Watanzania HATUJUI SIASA -- Tunafikiria VYAMA Vya SIASA ndio Opportunities zetu za kupata Maisha BORA; Kila mtu anakimbia FANI yake i.e UALIMU; BIASHARA; UKARANI; UDEREVA wote kwenye SIASA na IWALIPE kama haiwalipi Mnakimbilia CHAMA KINGINE...

It is a SHAME... we think POLITICS is FEEDING OUR LOUSY STOMACH...

Mkuu nakushauri kama hutoki Hai utuache sisi wenye uchungu na kura zetu na za wazazi wetu tuongee kwani hii siyo mada ya kisiasa . Tunadai committment aliyoitoa alipochukua ubunge No more
 
Back
Top Bottom