RC wa Arusha atembelea Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
PIX 1.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela (katikati), akiwasili katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha yanapofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akielezea kuhusu mpangilio wa washiriki katika maadhimisho hayo.
PIX 3.jpg

Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Ubia kati ya Sekta Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha, Enock Kivelege, akitoa elimu kuhusu idara hiyo kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Arusha walipotembelea Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
PIX 2.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela (kulia), akitambulishwa kwa watumishi wa Idara ya Sera, na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (katikati), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Kushoto ni Mchumi kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Mwanaidi Kanyawanah.​
 
Back
Top Bottom