RC Pwani: Sherehe za harusi zinaweza kuahirishwa kwa hekima ya kulinda Afya za Watu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge alisema maelekezo ya Wizara ya Afya ni ya kusimamiwa kwa kuchukua tahadhari kwanza katika sehemu zote za huduma kwa kuhakikisha kuna maji tiririka, vitakasa mikono, kukaa mbali kati ya mtu na mtu na watu kuvaa barakoa.

Kunenge alisema serikali imeshatia maagizo na kufafanua kuwa, sherehe za harusi zinaweza kuahirishwa kwa hekima ya kulinda maisha ya muhusika na watu wengine na kushauri kama ni lazima wahudhuriaji wawe wachache na ifanyike eneo kubwa litakalotoa nafasi ya watu kukaa mbalimbali huku kinga zikizingatiwa.

“Kwa mfano mtu anaweza kufunga ndoa akafanya sherehe baadaye hali ikikaa sawa, kuliko hivi ni hatari kwake na kwa watu wengine.

Hekima itumike hapa kwa mfano, mtu kafunga ndoa na sherehe ni watu 50 akifanyia Uwanja wa Mkapa utamlaumu? Kwa vyovyote huyu amejali, watu watakaa mbali mbali,” alieleza Kunenge.

Kunenge alisisitiza pia kuwa, matukio ya misiba pia si salama watu kujazana kwa kuwa maambukizi mengi yanatokea huko hivyo aliwataka wananchi wa Pwani kuwaachia majirani wachache na familia kumaliza masuala ya misiba ili kupambana na janga hili.
 
Back
Top Bottom