Michango ya Harusi na SendOff

Rare123

New Member
Jun 12, 2021
1
0
Habari wanajamii,

Mimi ni software developer, nilikuwa nina idea ya kutengeneza app/tool ya kusaidia kufuatilia na kukumbusha watu ahadi za michango kwa ajili ya harusi na sendoff.

App ina lengo la kutatua kero zifuatazo kwa mtu anayefuatilia, kukusanya na kutoa taarifa za makusanyo ya michango kwa kamati.

1. Kushindwa kutuma message za pamoja( za mkupuo) kwa watoa ahadi wote zenye taarifa zao kama jina, kiasi cha ahadi, kiasi kilichobakia pia na siku zilizobakia kufikia harusi au sendoff kuwakumbusha kutoa ahadi zao.

2. Kutuma ujumbe kwa mtu aliyemaliza ahadi yake tayari kisa yuko tu kwenye list ya broadcast na asipotolewa manually anakumbushwa tena mfano. ukiwa unatumia Whatsapp broadcast.

3. Kulazimika kuedit mkeka kila wakati ahadi imelipwa au kupunguza. Ukiwa na mkeka mrefu kwa ujumbe wa kutuma kwa kamati Whatsapp inabidi unscroll weee mpaka umfikie mtu wa kumuedit na Kisha kutuma kwa group.

App/tool itakuwa na uwezo wa;

1. Kuupload mkeka mzima kwa pamoja kutoka kwenye excel ukiwa na majina, namba ya simu na kiasi cha ahadi za watoa ahadi wote. Pia kuingiza taarifa za mtu mmoja mmoja.

2. Kirekodi kiasi kilicholipwa na mtoa ahadi kila malipo yanapofanyika na taarifa hizi zitatumika kujua kila mmoja amebakiza kiasi gani.

3. Kuandaa message kwa kila mtoa ahadi yenye taarifa zake binafsi kama jina, kiasi alichoahidi na kiasi kilichobakia. Message zinaweza kutumwa kwa waliomaliza kuwashukuru kwa kumaliza ahadi zao au kwa waliopunguza ili kuwakumbusha kumalizia ahadi zao.

4. Kushare mkeka mzima moja kwa Moja kwenye group la kamati bila haja ya kuanza kucopy mkeka, kumuedit halafu kutuma tena.

Kama ulishawahi kuwa au upo katika kitengo cha michango ya harusi au sendoff katika kamati na unaona tool/app ya namna hii inakufaa na ungependa kuwa nayo naomba kupata taarifa zako ili kuweza kukupatia taarifa mbali mbali wakati inaandaliwa pia kupokea maoni yako na kuwa miongoni mwa watu wa kwanza watakaoitumia itakapokuwa tayari.

Jaza Fomu ya Taarifa
 
Back
Top Bottom