Kwanini kamati za harusi zinaingia gharama kubwa kwa ajili ya MC?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,348
11,507
Kuna vitu ukikaa ukafikiria sana unaweza kubaki unacheka tu. How come mnatumia budget kubwa kumlipa mtu kwa ajili ya kusema makofi tafadhali, wamependeza hawajapendeza eti bibi harusi kata keki umlishe bwana harusi aisee.

Hongereni sana ma MC kwa kufanya utapeli katika njia ambayo victim anaona ni sawa kweli wajinga ndio waliwao na mtaji wa tapeli ni mbumbuu

Kitu kizuri kuhusu mimi naangazia kuhusu changomoto at the same time natoa suggestions. Taratibu tutafika tu ndoa si jambo la ghafla ni mchakato kuanzia unapokutana na mwenzi wako mpaka pale mnapoamua kuwa ni wakati muafaka wa kufunga ndoa kimsingi mna space kubwa ya wakati kuhakikisha mna arrange kila kitu to perfection siku ya harusi (sherehe).

Hapa nitajikita kwenye case ya kupata MC bora kwa gharama sawa na bure kabisa na kuepuka makanjanja. Kwanza mtu wa kawaida asiye na changomoto yoyote ya kiumbaji ana uwezo wa kuongea tofauti ni kwenye sauti na lafudhi.

Ni jambo la kushangaza sana kwenye koo mbili yaani ya kiumeni na kikeni kukosa mtu ambaye ni mchangamfu anayeweza kusimama mbele ya ukumbi na kusema wamependeza hawajapendeza.

Nachomaanisha MC atoke kwenye familia kama wanafamilia mnajuana strength na weakness zenu nini faida ya MC kutoka kwenye familia kwanza mnapunguza gharama za MC maana nasikia kuna MC anakunja 5M+ within short period of time sasa huyu MC wenu wa familia atapata favor ya kutolipa mchango wa harusi na first priority kwenye chakula.

Incase hamjaridhika na hiyo hoja hapo juu nawapa nyingine hii hapa mtakuwa na muda mwingi wa kujadiliana naye namna mnavyotaka sherehe yenu iwe na mnampa muda wa kutosha wa kufanya rehearsal ili aweze kudeliver to the fullest.

MC msichukie mtafute ishu nyingine za kufanya maana Kataa ndoa imeanza kushika vichwa vya watu.
 
Tafuta pesa mleta mada

Ulofa unakusumbua

Ndugu waache kuserebuka waanze kuhangaika na u MC

Wewe lofa mleta mada gharama za MC kama waziona kubwa ni ushahidi wa wazi kuwa wewe maskini wa kutupwa

Mtu kama wewe usioe utasumbua mke kwa umaskini wako uliokubuhu

Tafuta hela
 
Tafuta pesa mleta mada

Ulofa unakusumbua

Ndugu waache kuserebuka waanze kuhangaika na u MC

Wewe lofa mleta mada gharama za MC kama waziona kubwa ni ushahidi wa wazi kuwa wewe maskini wa kutupwa

Mtu kama wewe usioe utasumbua mke kwa umaskini wako uliokubuhu

Tafuta hela
Ndoa zinakosa amani baada ya harusi sababu ya madeni yote ya nini hayo.

Afu mnakaa miaka kadhaa mnaanza taratibu za talaka
 
Ndoa zinakosa amani baada ya harusi sababu ya madeni yote ya nini hayo.
Uongo
.Michango ya watu inatosha kama mtu ni mtu wa watu ila kama unashiriki kwa wengine utapata pesa hadi zibaki

Wewe utakuwa ni wale hujifanya self contained mitaani hawahitaji mtu yeyote kwa lolote mtu kama wewe ukifika wakati wa kuoa lazima ukione cha mtema kuni yakiwemo madeni

Kwa uandishi wako huu unaonyesha wewe ni mtu wa aina hiyo
 
Hata michango ya harusi ni ujambazi. Inakuwaje mtu apange sherehe yake mwenyewe alafu atake kutuchomoa hela? Kwani ni emergency?
Hushikiwi bunduki kuchangia hutaki usitoe na zamu yako.ikija watu hawatoi

Kwa taarifa yako wengi usipowachangisha ukiwaalika kwenye harusi yako hawaji utabaki mwenyewe na huyo mkeo
Michango ya harusi usiione vile kuna mambo ndani yake usidhani ukiwa na mabilioni yako waweza andaa harusi halafu upelekee watu waje hawaji
 
Hakuna cha uprofeshino wowote vitu vya msingi ni kufuata ratiba na kutotamka maneno yenye ukakasi.

Mtu yoyote anaejitambua anaweza kuhandle harusi ikamalizika salama
Kifupi tafuta hela hizo ni excuse za watu maskini

Mfano nyumbani mtu unakuta ana magari mazuri kibao lakini siku ya Harusi anataka kitu cha tofauti yanaenda kodiwa magari wakati hata nyumbani yapo

Tafuta hela wewe
 
Kifupi tafuta hela hizo ni excuse za watu maskini

Mfano nyumbani mtu unakuta ana magari mazuri kibao lakini siku ya Harusi anataka kitu cha tofauti yanaenda kodiwa magari wakati hata nyumbani yapo

Tafuta hela wewe
Alafu akishatafuta pesa wewe zitakusaidia nini? Hili neno la tafuta peda ni la vijana maskini kwani pesa sio solution ya mambo yote. Muulize mmiliki wa Kampuni inayozalisha Electronics device za Apple pesa ilimsaidia nini?
 
Back
Top Bottom