Kanamusi
Member
- Apr 9, 2020
- 22
- 65
Pamoja na approach aliyoitumia ila alichokisema RC antony mtaka ni ukweli uliochelewa kusemwa kwa sababu ni kwa miaka mingi sana elimu yetu imekuwa ikifanyiwa siasa na kuharibiwa na viongozi tuliowapa dhamana ya kuisimamia.
Mara kadhaa kumekuwa kukitolewa matamko yasiyo na kichwa wala miguu kuhusiana na elimu yetu na hakuna anayehoji, matokeo yake tumeacha wanasiasa ndio wawe waamuzi wa mwisho wa hatma ya maisha ya watoto wetu katika suala zima la elimu na mbaya zaidi viongozi hao hawana uchungu wowote kwa sababu watoto wao hawasomi shule zetu hizi za kata almaarufu kama shule za yebo yebo.
Ni juzi tu nimetoka kumsikia waziri wa TAMISEMI ambaye amepewa dhamana ya kusimamia elimu ya msingi na sekondari akisema wamemaliza tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi mashuleni.
Kwa kauli hiyo ya waziri kama mtu una uchungu na elimu unaweza kujikuta unatumia lugha ngumu kama aliyotumia Antony Mtaka kukemea uongo huo. Kwa sababu sisi wazazi tunaosemesha watoto wetu kwenye hizi shule za kata ndio tunajua adha wanazopata watoto wetu ikiwemo kukosa vipindi kwa sababu ya kutokuwa na walimu wa sayansi lakini waziri anatoka usingizini na kulipuka kwamba tatizo la walimu wa sayansi limekwisha. Hivi waziri kama huyu unaweza kusema ana uchungu kweli na elimu ya watoto wetu?
Leo kama taifa tunajadili na kutenga bajeti ya kujenga sanamu lakini wakati huo huo shule zetu hazina walimu wa kutosha na wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati. Sasa tujiulize hivi hilo sanamu lina tija gani kwa taifa kwanini hiyo bajeti isipelekwe kwenye shule zetu kutatua hata changamoto ya madawati ili watoto wetu wasome katika mazingira rafiki yaliyo boreka?
Waziri wa elimu naye yupo yupo tu hana habari ni kama hana kazi ya kufanya kwa sababu majukumu yote ya kielimu kwa sasa yanafanywa na Tamisemi ambayo ipo chini ya Rais labda ndio maana elimu inafanyiwa siasa kwa sababu jambo lolote la kuboresha elimu mfano kuajiri walimu kwenye shule zetu ni hadi Rais atolee matamko kwenye majukwaa ya kisiasa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wa elimu yetu.
Sasa kwa mambo kama haya kwa mtu ambaye yuko well committed na suala la elimu lazima atajisikia uchungu na kutumia lugha ngumu kufikisha ujumbe kwa viongozi labda ndipo wataamka na kuchukua hatua stahiki za kuboresha elimu ya watoto wetu.
Kwa hili nasimama na RC Mtaka kwa 100%.