RC Mtaka yupo sahihi. Ni kweli kabisa viongozi wetu hawana uchungu na elimu ya watoto wetu

Namna alivyo ongea Mtaka ni Kama anavyo ongea Tundu Lisu, kujifanya wewe unafahamu Mambo kuliko wenzako na kuliwasilisha Jambo kwa kebehi na majivuno ata Kama una ujumbe sahihi lakini kuwakilisha kwako kwa majivuno na kiburi si tu binadamu wenye uelewa watakushangaa lakini ata Mungu hapendi wenye Viburi.

Kiburi na dharau kimemletea Lisu matatizo mengi, Mtaka alikua anapendwa na wengi lakini wale wenye ufahamu na wanyenyekevu wa Mambo wata anza kua na wasiwasi nae juu ya tabia ambayo hawakua waki ifahamu Kama alikua nayo.
 
Wewe nguchiro ukilaza wako mpelekee mkeo na wanao. Mtaka mmemtisha na yeye ana familia inayomtegemea na mbaya zaidi wanafiki kama ninyi mmejaa nchi hii, hivyo baba wa watu ameona isiwe tabu.
Mkuu wala usingemjibu kwa heshima hivyo, huyu ni just baadhi ya mifano ya kilicho elezwa na UZI, UZI uko wazi sana kwamba Watanzania wengi ni wanafiki, unafiki huo ndio umesababisha hata soko la Kariakoo kuungua so huyu ni moja kati ya sample hizo
 
Mkuu wala usingemjibu kwa heshima hivyo, huyu ni just baadhi ya mifano ya kilicho elezwa na UZI, UZI uko wazi sana kwamba Watanzania wengi ni wanafiki, unafiki huo ndio umesababisha hata soko la Kariakoo kuungua so huyu ni moja kati ya sample hizo
Shukrani mkuu. Nimeshampotezea huyu mchumia tumbo.
 
Watanzania wana roho mbaya sana mkuu.
na upumbavu mwingi sana. mtu una akili timamu unamsupport waziri ambaye watoto wake hawasomi shule za kata.....ujinga wa watanzania wengi bado wanaamini kuwa jukumu la kusomesha watoto wao ni la serikali
 
elimu ni nzuri ndio maana imepewa masaa 9, masaa mengine wanafunzi wajifunze stadi za maisha......kwanza wakae makambi na wakeshe kwa ajira gani??.....maana elimu yetu practically haipo vizuri.....
 
Hawa viongozi wapo kuua elimu yetu ili waendelee kututawala
Kweli kabisa ndio maana hawataki kuboresha mazingira ya shule zetu ili kusudi watoto wao waje kuwa watawala wa watoto wetu ambao wamepitia mfumo wa elimu duni na kama wazazi tusipoamka na kuibana serikali basi watoto wetu watabaki kuwa wasindikizaji
 
Nchi hii inashindwa kupiga hatua inayotakiwa kimaendeleo kwa sababu ya hawa wasomi wetu wenye vyeti lukuki, huku wakikosa kabisa maarifa vichwani mwao! Ndalichako tangu aingie kwenye siasa, amepoteza kabisa ule weledi aliokuwa nao enzi zile akiwa Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa!...
Kwanza mbna ndalichako kazi yake sioni, maan madaraka yake yote yapo Tamisemi. Khaaaaah
 
Kuna baadhi ya nchi kiongozi lazima watoto wake wasome shule za serikali.

Sikumbuki vizuri ni mwaka gani lakini kuna waziri mmoja Uingereza alikosolewa vikali kumpeleka mwanae shule binafsi, akajitetea mtoto wake alikua na ulemavu uliohitaji uangalizi wa karibu. Hata hivyo ikaja hoja kwamba kwanini serikali wasiwe na shule za aina hiyo kwakua watoto wenye hayo matatizo wapo wengi?

Waliweka hivyo ili kuweka msisitizo wa viongozi kuona umuhimu wa kuboresha huduma za umma.
Na ndo inatakiwa hata hapa.
 
Mtaka yuko sahihi sana. Tena sana. Changamoto kwangu ndogo ni moja tu. Asingegusia kabisa kuhusu Waziri kama Waziri aliwahi kuongea ujinga huko nyuma. Yeye angeng'ang'ania tu kusema waweke kambi, wasome kwa bidii, watumie muda mrefu kusoma. Hilo tu
 
Mtaka ni aina ya viongozi ambao hawataki makuu hasa endapo asilimia kubwa ya watu anao waongoza wana hali duni kimaisha, typical Nyerere style......unaona anavyosisitiza kwamba wao watoto wao wanasoma kule.....viongozi wasio na ubinafsi ndo wanahitajika kwa sasa kwani wanakuwa wanahisi shida za wananchi na wanakuwa tayari kuyachukua kama matatizo yao wenyewe....
 
Kwanza mbna ndalichako kazi yake sioni, maan madaraka yake yote yapo Tamisemi. Khaaaaah
Ndalichako kwenye hili saga kaangushiwa jumba bovu tu na watu wasiopenda awepo pale lakini mtu wa kwanza anayetakiwa kulaumiwa ni ummy mwalimu kwakuwa ndiye amepewa jukumu la kusimamia elimu lakini muda wote yuko ofsini anakula kiyoyozi alafu anatoka na matamko ya ajabu ajabu mara shule hazina walimu wa physics sasa anashindwa nini kuwaajiri??
 
Mtaka yuko sahihi sana. Tena sana. Changamoto kwangu ndogo ni moja tu. Asingegusia kabisa kuhusu Waziri kama Waziri aliwahi kuongea ujinga huko nyuma. Yeye angeng'ang'ania tu kusema waweke kambi, wasome kwa bidii, watumie muda mrefu kusoma. Hilo tu
Hatutafika popote kama tutaendelea kufichana kuambiana ukweli kwenye mambo ya msingi kama hili la elimu. Kwa hapa tulipofikia tunahitaji akina mtaka wengi zaidi wenye ujasiri wa kusema ukweli mchungu bila kupepesa macho wala kuoneana aibu ili hatua muhimu ziweze kuchukuliwa kunusuru elimu ya watoto wa watanzania maskini
 
Pamoja na approach aliyoitumia ila alichokisema RC antony mtaka ni ukweli uliochelewa kusemwa kwa sababu ni kwa miaka mingi sana elimu yetu imekuwa ikifanyiwa siasa na kuharibiwa na viongozi tuliowapa dhamana ya kuisimamia.

Mara kadhaa kumekuwa kukitolewa matamko yasiyo na kichwa wala miguu kuhusiana na elimu yetu na hakuna anayehoji, matokeo yake tumeacha wanasiasa ndio wawe waamuzi wa mwisho wa hatma ya maisha ya watoto wetu katika suala zima la elimu na mbaya zaidi viongozi hao hawana uchungu wowote kwa sababu watoto wao hawasomi shule zetu hizi za kata almaarufu kama shule za yebo yebo.

Ni juzi tu nimetoka kumsikia waziri wa TAMISEMI ambaye amepewa dhamana ya kusimamia elimu ya msingi na sekondari akisema wamemaliza tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi mashuleni.

Kwa kauli hiyo ya waziri kama mtu una uchungu na elimu unaweza kujikuta unatumia lugha ngumu kama aliyotumia Antony Mtaka kukemea uongo huo. Kwa sababu sisi wazazi tunaosemesha watoto wetu kwenye hizi shule za kata ndio tunajua adha wanazopata watoto wetu ikiwemo kukosa vipindi kwa sababu ya kutokuwa na walimu wa sayansi lakini waziri anatoka usingizini na kulipuka kwamba tatizo la walimu wa sayansi limekwisha. Hivi waziri kama huyu unaweza kusema ana uchungu kweli na elimu ya watoto wetu?

Leo kama taifa tunajadili na kutenga bajeti ya kujenga sanamu lakini wakati huo huo shule zetu hazina walimu wa kutosha na wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati. Sasa tujiulize hivi hilo sanamu lina tija gani kwa taifa kwanini hiyo bajeti isipelekwe kwenye shule zetu kutatua hata changamoto ya madawati ili watoto wetu wasome katika mazingira rafiki yaliyo boreka?

Waziri wa elimu naye yupo yupo tu hana habari ni kama hana kazi ya kufanya kwa sababu majukumu yote ya kielimu kwa sasa yanafanywa na Tamisemi ambayo ipo chini ya Rais labda ndio maana elimu inafanyiwa siasa kwa sababu jambo lolote la kuboresha elimu mfano kuajiri walimu kwenye shule zetu ni hadi Rais atolee matamko kwenye majukwaa ya kisiasa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wa elimu yetu.

Sasa kwa mambo kama haya kwa mtu ambaye yuko well committed na suala la elimu lazima atajisikia uchungu na kutumia lugha ngumu kufikisha ujumbe kwa viongozi labda ndipo wataamka na kuchukua hatua stahiki za kuboresha elimu ya watoto wetu.

Kwa hili nasimama na RC Mtaka kwa 100%.
Mtaka yupo sahihi,elimu yetu inawekwa rehani na aina ya viongozi tuliowachagua.kambi za masomo inaonekana zinasaidia Sana watoto wa kimaskini ambao wazazi wao waliuza mbuzi ,ng'ombe na kuku ili kupeleka watoto wao shuleni.Mtaka hapaswi kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom