RC Makonda: Dar es Salaam tumetenga hospitali 25 kuhudumia wenye dalili za Corona na mh Rais Magufuli ametupa magari ya wagonjwa 20 yote mapya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mkuu wa mkoa wa DSM Mh. Makonda amesema mkoa wake umetenga hospitali 25 jijini zikiwemo zile za Rufaa na baadhi ni binafsi ili kuhudumia watu wote wanaojihisi wana dalili za corona.

Makonda amesema ukifika katika hospitali hizo utapimwa magonjwa mengine yote na ukionekana uko salama ndipo damu yako itapelekwa maabara kuu kupima corona.

Kadhalika mh Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapa magari mapya ya wagonjwa 20 ili yatumike katika mpango huo.


=====


TAARIFA KWA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM

KUHUSU VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VILIVYOTEULIWA KUCHUKUA SAMPULI YA VIPIMO VYA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU UNAOSABABISHWA NA VIRUSI VYA CORONA(COVID-19)


Ndg.Wananchi wa Dar es Salaam,

Kama mnavyofahamu kwamba Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufuata miongozo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto umekuwa ukiendelea kuimarisha hatua za awali za mchakato wa uchunguzi wa kimaabara wa ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona(COVID 19) hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na visa kadhaa vya watu waliopatikana na ugonjwa wa corona. Lengo ni kuhakikisha kuwa ugonjwa huu wa Corona unadhibitiwa na kutokomezwa kabisa.

Ndg.Wananchi wa Dar es Salaam,

Wahisiwa wote wa Ugonjwa wamekuwa wakipimwa katika Maabara kuu ya Taifa na Majibu yao kupatikana kwa wakati kama Muongozo unavyoelekeza. Changamoto mojawapo ambayo imekuwa ikijitokeza ni kwa baadhi ya watu wenye Dalili za Ugonjwa huu kupita katika vituo kadhaa vya Kutolea Huduma za Afya na hivyo kuchangamana/kukutana na watu kadhaa kabla ya kugundulika kuwa na Ugonjwa. Hali hii inaweza kuchangia kuongezeka kwa visa vya Ugonjwa husika kwa kasi kubwa sana. Hivyo Mkoa umejipanga kupunguza ueneaji wa ugonjwa kwa kuainisha Vituo maalum vya Wahisiwa wanaokidhi vigezo vya tafsiri ya Ugonjwa(suspects) kuchukuliwa Sampuli kwa ajili ya Vipimo vya Maabara katika maabara kuu ya Taifa. Ieleweke kuwa Vituo hivi

havitatumika kupima Samapuli, bali ni vituo vya kukusanyia Sampuli za wahisiwa tu. Aidha, vituo hivi vipya vitawawezesha wahisiwa kupata huduma ya vipimo kwa kuchukuliwa sampuli katika maeneo yao ya karibu kabla ya kuchangamana na watu wengine na kusababisha kusambaza virusi hivyo. Hivyo vituo hivi vitaongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huu hatari wa corona (Covid-19)

Ndg.Wananchi wa Dar es Salaam, Nawataarifu rasmi kwamba Vituo vifuatavyo (Vituo 24 vya Kutolea Huduma za Afya) katika Mkoa vimeteuliwa kutumika Kuchukua Sampuli kutoka kwa wahisiwa na hatimaye kupeleka Sampuli hizo Maabara kuu ya Taifa;

VITUO VILIVYOTEULIWA NI KAMA VILIVYOAINISHWA HAPA CHINI;

VITUO VILIVYOTEULIWA KWA AJILI YA KUCHUKUA SAMPULI ZA UGONJWA WA CORONA(COVID 19) KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

NA HALMASHAURI
JINA LA
AINA YA
UMILIKI(SERIKAL
KATA
KITUO CHA
KITUO
I/FBO/ BINAFSI)
KUTOLEA
(RRH, DH,
HUDUMA
HC)
Hospitali
1
Kinondoni MC
1​
Mwananyamalaya Rufaa
ya MkoaGOVMwananyamala
2​
MagomeniKituo cha
AfyaGOVMagomeni
3​
MikoroshiniKituo cha
AfyaGOVMsasani
4​
ISTClinicPRIVATEMasaki
5​
TMJHospPRIVATEMikocheni
6​
RabininsiaHospPRIVATEWazo
Hospitali
2
Ilala MC
1​
Amanaya Rufaa
ya MkoaGOVIlala
2​
BuguruniHospGOVMnyamani
4​
Mnazi mmojaHospGOVMchafukoge
5​
MuhimbiliNationalUpanga
HospGOVMagharibi
6​
Hindu MandalHospPRIVATEKisutu
7​
Agha KhanHospPRIVATEKivukoni
8​
RegencyHospPRIVATEUpanga
Mashariki


Hospitali
3
Temeke MC
1​
Temekeya Rufaa
ya MkoaGOVTemeke
2​
Mbagala RangiHospMbagala
TatuGOVkuu
3​
YomboHCGOVYombo
4​
TOHSHospPRIVATEChangombe
4
Ubungo MC
1​
SinzaHospGOVSinza
2​
KimaraKituo cha
AfyaGOVKimara
3​
MloganzilaSpecilalized
HospGOVKiluvya
4​
BOCHIHospPRIVATEKibamba
5
Kigamboni MC
1​
VijibweniKituo cha
AfyaGOVVijibweni
2​
KigamboniKituo cha
AfyaGOVKigamboni
3​
Agha KhanHospPRIVATEKibada
JUMLA NI
24
VITUO


Paul C. Makonda

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM
 

Attachments

  • Taarifa kwa Wananchi wa Mkoa wa DSM.pdf
    115.8 KB · Views: 2
Huko kunakotengwa huwa kunawekwa nini kama msaada kwa wagonjwa watarajiwa. Maana kuwa na majengo siyo kutenga sehemu kwa ajili ya wagonjwa bali kuwa na vifaa hitajiwa ndiyo unaweza kusema kwamba umetenga maeneo kadhaa kwa ajili ya wagonjwa wa CORONA.
 
Back
Top Bottom