RC Makala: Tukiweza kuwadhibiti biashara holela, ajenda ya usafi itawezekana Dar es Salaam

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,823
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anaongelea mambo mbalimbali kuhusu mkoa wa Dar. Miongoni ni suala la wamachinga na kupoa kwa Serikali baada ya kutoa tangazo la kuwaondoa. RC Makala amesema kwasasa wameweka kipaumbele kwenye kutoa elimu na anaamini hawatafika kwenye kutumia nguvu.

RC Makala: Ili kuboresha usafi jiji la Dar lazima tudhibiti ufanyaji biashara holela hivyo nikaona kuna haja ya kuwasaidia watu wetu sio kuwaondoa. Watu kwenye mfereji wameweka zege na kuweka kibanda juu yake, ukiziba?

Tumeanza kuweka vibao, usifanye biashara hapa! Nitoe wito kwa wafanyabiashara, ukiona vibao hivyo usifanye biashara.

Naendelea kutoa elimu, niwaombe mahali kote ambao kumewekwa vibao sio eneo la kufanya biashara. Masoko yako na hayana watu.

Makala.jpg
 
Huyu RC ana matamko mengi sana, mengine sijui yaliishia wapi, ananikumbusha enzi za Bashite.
 
Makala usifuate ushauri wa chadema wa kuwaondoa machinga utapata taabu sana kulingoza jiji.

Chadema wanataka uharibikiwe.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anaongelea mambo mbalimbali kuhusu mkoa wa Dar. Miongoni ni suala la wamachinga na kupoa kwa Serikali baada ya kutoa tangazo la kuwaondoa. RC Makala amesema kwasasa wameweka kipaumbele kwenye kutoa elimu na anaamini hawatafika kwenye kutumia nguvu.

RC Makala: Ili kuboresha usafi jiji la Dar lazima tudhibiti ufanyaji biashara holela hivyo nikaona kuna haja ya kuwasaidia watu wetu sio kuwaondoa. Watu kwenye mfereji wameweka zege na kuweka kibanda juu yake, ukiziba?

Tumeanza kuweka vibao, usifanye biashara hapa! Nitoe wito kwa wafanyabiashara, ukiona vibao hivyo usifanye biashara.

Naendelea kutoa elimu, niwaombe mahali kote ambao kumewekwa vibao sio eneo la kufanya biashara. Masoko yako na hayana watu.

Hiyo njia ya vibao nzuri sana, nashauri aongeze na kuweka kamba usiku na vibao juu Ili wakifika Asubuhi wanakuta serikari ishachukua maeneo yake ya wazi na kuweka jiji katika mazingira mazuri.
 
Safi sana waweke vibao vya kuzuia sehemu maalum za biashara halali na hizo za hovyo hovyo zinazochafua jiji muonekano wake mzuri
 
Makala usifuate ushauri wa chadema wa kuwaondoa machinga utapata taabu sana kulingoza jiji.

Chadema wanataka uharibikiwe.
Machinga mwisho wao uwe kkoo tu na hapo kkoo watafutiwe maduka ya kupanga nashauri serikali iangalie uwezekano wa kujenga flemu za kisasa na kuwakodisha machinga wenye biashara kubwa unakuta mmachinga ana vitu vinavyo tosha kufungua duka ila yupo mabandani
 
Back
Top Bottom