RC Kone ameshindwa kazi, apumzishwe

Jodeny

JF-Expert Member
Mar 26, 2012
201
25
Wakuu wa mikoa wengi wamekuwa wakipambana kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na maisha bora na kupunguza kero zinazowakabili. Wengi wamejikita katika kusaidia wakulima kunufaika na kazi wanazozifanya, lakini kwa huyu Parseko Kone wa Singida mambo yamekuwa tofauti na yeye amekuwa akikandamiza watu wake hasa wakulima.
Mbaya zaidi ni kwamba, huyu jamaa amejikita zaidi kwenye siasa kwa kushirikiana na kundi moja la mafisadi kupanga safu za uongozi ndani ya CCM ili kutimiza malengo yao kisiasa mwaka 2015. Nikiwa mkazi wa Singida mwenye uchungu na babu, kaka, dada na ndugu na jamaa nashauri huyu jamaa atoswe hana la maana analolifanya. Pia, wadau wanaomfahamu zaidi wamwage data ili ajadiliwe hapa jamvini.
 
Hakuna RC hata mmoja anayefanya kazi ya kuleta maendeleo wote ni vibaraka wa ccm na wapo kulinda maslahi ya ccm nakutumikia matumbo yao katiba mpya ifute ma RC na ma DC wote!
 
wanasingida nawajua kazi yao ni majungu tu ndio maana mji ulichelewa sana kuendelea, baada ya huyu Kone kuja Singida ndio ameubadilisha mji sasa umekuwa kivutio lakini wanaompinga hawakosekani ndio hawa! Singida ilikuwa kila mwaka wananchi wanapatwa na njaa lakini tangu ameanza kuhamasisha kilimo cha mtama na uwele kwa mazao ya chakula njaa kushnei, kwenye mazao ya biashara amehamasisha alizeti na asali leo watu wengi vijisenti havikosekani, kahamasisha viwanda vya alizeti vikajengwa Singida hasa kile cha Mount Meru leo soko la alizeti ni la uhakika na vijana wana ajira kibao, hebu angalieni mbunge wenu Dewji anavyo wanyonya mnasubiri kwenda kupanga foleni kwake kuomba badala ya kuhamasisha maendeleo na hana nyumba Singida akija anafikia hotelini,anayebisha aonyeshe Singida before 2006 na ya leo. sasa hivi anajenga hospitali ya rufaa na analeta umeme wa upepo, vijana watapata ajira n.k. mimi si mwanasisiemu ni mtumishi ndani ya mkoa huu naijua Singida na watu wao walivyo wapinga maendeleo.
 
huyu rc ni wa ajabu xaaaanaaaa,aliwahi kutangaza kuwa akiona mwananchi yeyote amelima mahindi ndani ya mkoa wake atayafyeka,cha kushangaza baa la njaa likija chakula cha msaada kinacholetwa ni mahindi, sasa siku moja aliulizwa mbona unatukataza kulima mahindi unataka tulime mtama na uwele tu ilhali njaa ikija una2letea mahindi? unajua alijibu nini! kashfa kwenda mbele,sasa cjui ndo maagizo hayo au ndo uongozi wenyewe! ila nimeamini watanzania sasa wameamka sio kama wa mwaka foteseveni.
 
wanasingida nawajua kazi yao ni majungu tu ndio maana mji ulichelewa sana kuendelea, baada ya huyu Kone kuja Singida ndio ameubadilisha mji sasa umekuwa kivutio lakini wanaompinga hawakosekani ndio hawa! Singida ilikuwa kila mwaka wananchi wanapatwa na njaa lakini tangu ameanza kuhamasisha kilimo cha mtama na uwele kwa mazao ya chakula njaa kushnei, kwenye mazao ya biashara amehamasisha alizeti na asali leo watu wengi vijisenti havikosekani, kahamasisha viwanda vya alizeti vikajengwa Singida hasa kile cha Mount Meru leo soko la alizeti ni la uhakika na vijana wana ajira kibao, hebu angalieni mbunge wenu Dewji anavyo wanyonya mnasubiri kwenda kupanga foleni kwake kuomba badala ya kuhamasisha maendeleo na hana nyumba Singida akija anafikia hotelini,anayebisha aonyeshe Singida before 2006 na ya leo. sasa hivi anajenga hospitali ya rufaa na analeta umeme wa upepo, vijana watapata ajira n.k. mimi si mwanasisiemu ni mtumishi ndani ya mkoa huu naijua Singida na watu wao walivyo wapinga maendeleo.

Hapo bro umesema, RC ni mtu safi na mchapa kazi , mi kila napo kuja singida nakuta mabadiliko , sasa huyu dewj sioni anachofanya , nimewah kununua maji lita 18 kwa 500tsh , sept.12. sasa huyui mbuge kweli? utajiri aliyo nao ameshindwa kumaliza kero ya maji leo miaka.
nyumba hana ipo ya urith tena mmh.
 
mleta mada nadhani sio mkazi wa singida,kwa sisi tunaoishi na kufanya kazi singida Kone na Hassan Liana ni viongozi wa mfano tanzania.kwanza kwa swala la wakulima kawasaidia waliokuwa wanauza alizeti kwa bei za hasara,kwa sisi wafanyakazi kone na liana wanatusaidia sana kupata haki zetu kama vile pesa za kujikimu unapoanza kazi,kodi ya nyumba kulingana na nyaraka za serikali nk.mleta mada nataka nikufahamishe pia tunajenga hospitali kubwa ya kisasa,chini ya uongozi wa kone,tuna mradi mkubwa wa maji kutoka kijiji cha mwankoko pia chini ya kone.mleta mada naona unataka kutuharibia mkoa wetu.Mimi sio mwanaCCM lakini nikiambiwa nimtaje kiongozi mmoja wa CCM,basi nitamtaja Parseko Korne
 
Wakuu wa mikoa wengi wamekuwa wakipambana kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na maisha bora na kupunguza kero zinazowakabili. Wengi wamejikita katika kusaidia wakulima kunufaika na kazi wanazozifanya, lakini kwa huyu Parseko Kone wa Singida mambo yamekuwa tofauti na yeye amekuwa akikandamiza watu wake hasa wakulima.
Mbaya zaidi ni kwamba, huyu jamaa amejikita zaidi kwenye siasa kwa kushirikiana na kundi moja la mafisadi kupanga safu za uongozi ndani ya CCM ili kutimiza malengo yao kisiasa mwaka 2015. Nikiwa mkazi wa Singida mwenye uchungu na babu, kaka, dada na ndugu na jamaa nashauri huyu jamaa atoswe hana la maana analolifanya. Pia, wadau wanaomfahamu zaidi wamwage data ili ajadiliwe hapa jamvini.

Ulitegemea nini kutoka kwa Ex-std VII aliye pata PhD?????
 
Back
Top Bottom