gwijimimi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2011
- 7,344
- 3,616
mpaka 2020 hakika hakuna rangi tutaacha kuiona dahNi baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa,mdogo wangu na Mwanasheria mwenzangu Ally Hapi. Alikuwa akielekea kutoa amri ya kukamatwa,kuwekwa ndani,kuhojiwa na kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Diwani wa Viti Maalum huko Iringa kwa tiketi ya CHADEMA.
Kadiri ya clip ya video niliyoitazama kwa MillardAyo,kuna Mzee mmoja alilalamika kwa RC Hapi kuwa amebomolewa nyumba yake kwa amri ya Mwenyekiti na Diwani huyo wa CHADEMA. Mlalamikaji akajitambulisha kama Mwenyekiti wa Tawi la CCM.Mwanamama mhusika alijitetea bila mafanikio. Akakamatwa na askari wa kike wa JWTZ baada ya kukosekana kwa askari wa kike wa Polisi.
Kimsingi,maneno ya aina hiyo yamekuwa ya kawaida kwa Wakuu wa mikoa na wilaya nchini. Yana tija gani? Yaendelee?