RC Hapi: Mimi ni mtu hatari, usiniudhi, usinichezee!

RC Hapi: Mimi ni mtu hatari, usiniudhi, usinichezee!

Ni baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa,mdogo wangu na Mwanasheria mwenzangu Ally Hapi. Alikuwa akielekea kutoa amri ya kukamatwa,kuwekwa ndani,kuhojiwa na kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Diwani wa Viti Maalum huko Iringa kwa tiketi ya CHADEMA.

Kadiri ya clip ya video niliyoitazama kwa MillardAyo,kuna Mzee mmoja alilalamika kwa RC Hapi kuwa amebomolewa nyumba yake kwa amri ya Mwenyekiti na Diwani huyo wa CHADEMA. Mlalamikaji akajitambulisha kama Mwenyekiti wa Tawi la CCM.Mwanamama mhusika alijitetea bila mafanikio. Akakamatwa na askari wa kike wa JWTZ baada ya kukosekana kwa askari wa kike wa Polisi.

Kimsingi,maneno ya aina hiyo yamekuwa ya kawaida kwa Wakuu wa mikoa na wilaya nchini. Yana tija gani? Yaendelee?
Kumbe,nilkua sijafahamu.ahsante mtoa maada. Kawa hawafanyi Nazi zao,wacha waisome nmba.DC piga kazi.madiwani wengi,wamejisahau.
 
Kilio changu ni kwa madiwani wa kata hasa wa chadema huku kusini.ni wa vivu.km wakuu wa mikoa yote wangekua km hapi,ingekua saf san
 
vijana. tunasikitika sana jinsi vijana wsliopewa mamlaka wanapokwenda kinyume....
 
Ukiwa unatumia mali za serikali unageuka Mungu mtu, unasahau na mengine!!. Tupo pamoja
 
Watayatamka sasa lakini kuna siku yatatamkwa na wengine yakiwalenga wao lakini watataka kuomba msamaha lakini watakuwa wamechelewa kwani adhabu ya Mungu hapa hapa duniani itakuwa imetimia na watakuwa bado wanatafakari na kufikiria pale watakapokufa nini hasa kitatokea kwao kama Mungu amewahukumu hapa Duniani kwa adhabu kubwa hivi je Baada ya kufa itakuwaje?
labdaukiwakaburini sioohaii
 
Is very unfortunate wazee wa aina ya Jaji Samata walio tayari kusema, kukemea na kushauri juu ya tabia na maneno kama haya bila woga ni kama kwa sasa hawapo, natamani viongozi wakumbuke unaokua kwenye nafasi hizo na mamlaka hayo hata ukiongea jambo la kijinga bado watu watacheka na kukupigia makofi kila mtu kwa sababu yake ila siku nafasi na mamlaka yakiondolewa ndio wataelewa somo vizuri.
True!
Kama kijana mdogo Hapi amesema maneno ya umimi, basi hajui siasa za nchi hii.

Aelewe kuwa he is dispensable, atashangaa sana siku akitemwa.
 
Hivi askari wa JWTZ anaruhusiwa ku arrest?
 
Huyu ilibidi ahojiwe anauhatari gani.!
 
Tatizo la viongozi kuwa wao ndiyo mapolisi na mahakimu wakati huo huo. Hata rais huwa haagizi hivyo huwa anaagiza uchunguzi na hatua kuchukuliwa. Sasa una muweka mtu ndani baada ya kusikiliza malalamiko ya upande mmoja, je baadaye ikionekana uliye mweka ndani hana kosa utamfidiaje. Wakuu wa wilaya na mikoa wengi wamekuwa madikteta hawafuati sheria na taratibu kabisa
Hapo n kW Wahehe aangalie sana bwn mdogo huu,Asome vzuri histri ya Kleruu vs Mwamwindi,
 
Tatizo la viongozi kuwa wao ndiyo mapolisi na mahakimu wakati huo huo. Hata rais huwa haagizi hivyo huwa anaagiza uchunguzi na hatua kuchukuliwa. Sasa una muweka mtu ndani baada ya kusikiliza malalamiko ya upande mmoja, je baadaye ikionekana uliye mweka ndani hana kosa utamfidiaje. Wakuu wa wilaya na mikoa wengi wamekuwa madikteta hawafuati sheria na taratibu kabisa
Hapa unawaonea hao wakuu wa mikoa na mwanzilishi wa wake unamjua na sio kama ameacha anajua athari zake na yeye amejitoa na msala amewaachia wateule na hizo sinema zina baraka zake 100% msikingie kifua kabisa.
 
Ni baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa,mdogo wangu na Mwanasheria mwenzangu Ally Hapi. Alikuwa akielekea kutoa amri ya kukamatwa,kuwekwa ndani,kuhojiwa na kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Diwani wa Viti Maalum huko Iringa kwa tiketi ya CHADEMA.

Kadiri ya clip ya video niliyoitazama kwa MillardAyo,kuna Mzee mmoja alilalamika kwa RC Hapi kuwa amebomolewa nyumba yake kwa amri ya Mwenyekiti na Diwani huyo wa CHADEMA. Mlalamikaji akajitambulisha kama Mwenyekiti wa Tawi la CCM.Mwanamama mhusika alijitetea bila mafanikio. Akakamatwa na askari wa kike wa JWTZ baada ya kukosekana kwa askari wa kike wa Polisi.

Kimsingi,maneno ya aina hiyo yamekuwa ya kawaida kwa Wakuu wa mikoa na wilaya nchini. Yana tija gani? Yaendelee?

Maagizo ya namna hiyo yataendelea kuwepo maana muasisi wake ni rais. Na hata rais alimuweka ndani mtendaji wa cdm kwenye safari zake huko serengeti baada ya kusikia tuhuma toka kwa mwanaccm. Hiyo ni Carbon Copy ya akifanyacho mkuu wa nchi. Tabia za aina hii zinaweza kukomeshwa tu iwapo hata rais ataweza kushitakiwa akiwa au ametoka madarani.
 
Tatizo la viongozi kuwa wao ndiyo mapolisi na mahakimu wakati huo huo. Hata rais huwa haagizi hivyo huwa anaagiza uchunguzi na hatua kuchukuliwa. Sasa una muweka mtu ndani baada ya kusikiliza malalamiko ya upande mmoja, je baadaye ikionekana uliye mweka ndani hana kosa utamfidiaje. Wakuu wa wilaya na mikoa wengi wamekuwa madikteta hawafuati sheria na taratibu kabisa

Hukufuatilia safari ya rais huko serengeti. alifanya sawa sawa kabisa na hicho alichofanya huyo RC. Naye alisikiliza upande mmoja toka kwa mwanaccm aliyemtumuhu mtendaji wa cdm kuhusu fedha za umma. Rais akaagiza palepale huyo mtendaji akamatwe na kuwekwa ndani. Hiyo tabia ni fashion kwa sasa na muasisi wake ni rais.
 
Grade 4 inawatosha ninyi wabongo mkaanze kusoma nini maana ya yafuatayo

1) wewe ni nani?? Upo hapa duniani kwa dhumuni gani??

2) utu ni nini ??

3) haki zako za msingi na wajibu wako uwapo popote duniani

4) maana ya siasa na demokrasia ni nini?? nk

Ukishayajua haya utayajua mengi zaidi

Una hasira zilizojikita kwenye nadharia zaidi kuliko uhalisia. Unachoongea huko ulipo sio uhalisia uliopo hapa nchini. Kama kweli wewe ni msomi na unajua unachopigania na kujua haki zako njoo tuokoe kwani sisi tumeshindwa. Ninachokiona kutoka kwako ni kejeli na hasira za kilevi ulichotumia. Njoo huku nchini utekeleze hayo unayoamini, kinyume na hayo hapa tunakuona ni muuza face tu usiye na jipya. Unadhani haya yanayoendelea hapa nchini tunakubalina nayo, au ni jinsi ya kupambana na hali hizo? Wenzako tumejaribu kupambana kwa uwezo wetu lakini mazingira sio rafiki hivyo. Wewe unatuona sisi ni bonge ya mafala bila kuangalia mazingira. Kafie mbele.
 
Back
Top Bottom