RC Hapi: Mimi ni mtu hatari, usiniudhi, usinichezee!

RC Hapi: Mimi ni mtu hatari, usiniudhi, usinichezee!

Ni baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa,mdogo wangu na Mwanasheria mwenzangu Ally Hapi. Alikuwa akielekea kutoa amri ya kukamatwa,kuwekwa ndani,kuhojiwa na kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Diwani wa Viti Maalum huko Iringa kwa tiketi ya CHADEMA.

Kadiri ya clip ya video niliyoitazama kwa MillardAyo,kuna Mzee mmoja alilalamika kwa RC Hapi kuwa amebomolewa nyumba yake kwa amri ya Mwenyekiti na Diwani huyo wa CHADEMA. Mlalamikaji akajitambulisha kama Mwenyekiti wa Tawi la CCM.Mwanamama mhusika alijitetea bila mafanikio. Akakamatwa na askari wa kike wa JWTZ baada ya kukosekana kwa askari wa kike wa Polisi.

Kimsingi,maneno ya aina hiyo yamekuwa ya kawaida kwa Wakuu wa mikoa na wilaya nchini. Yana tija gani? Yaendelee?
Huu utawala kila mtu kawa baunsa hata kama enzi zile za Jk alikuwa kimbau mbau
 
Vyama vya upinzani ni adui namba moja wa taifa la Tz katika udikteta wa awamu ya jpm?
Naona nguvu nyingi sana zinatumika kuudhibiti kuliko juhudi za kudhibiti ujinga na maradhi. Shule hazina walimu wa kutosha wala vitabu lakini fedha zinapelekwa kununua wapinzani ( oil chafu, kwa mujibu wa Nepi Nnauye). Shule za serikali zinazalisha zero kwa juhudi lakini serikali inahangaika na wapinzani. Ipo siku dikteta wetu atakamatwa ashitakiwe the Hague kwa unyama dhidi ya raia wake.
Haitatokea MTU Tanzania kushitakiwa the Hague hata Dikteta Mbowe hatashitakiwa.
 
Hakuwa na haja kabisa ya kuufahamisha umma kuwa yeye ni mtu hatari sana na hataniwi. Watu wote sasa hivi tunajua wateule wote wa awamu hii wanajiona miungu watu. Cha ajabu utakuta watu hawa hawa wanamlauuumu pharao wa misri
 
Nilijuaga ni mtu makini sana.....kumbe nae anatetea gari na mafuta...of course ilipaswa afungue tu kesi kwani ni jambaz au ametumia silaha au ameua tuseme atatoroka? Wafanye wafanyalo ila mwisho wa siku wafahamu kuwa wote sisi ni wanadamu tu vyeo vinapita na mwisho wa siku tutalipwa na kukumbwuka positively kwa wema tunaotenda....
 
Yaani wewe umeshindwa kuleta link.. duh.. na umesikiliza yote na kuja kuandika kama udaku tu..

Huyo mzee umemnukuu vyema?

 
Petro E mselewa

Bongo ni nchi ya wajinga, !

Na ujinga huo utadumu mpaka atakaporudi mwana wa adamu , hakuna kitakachobadilisha kitu mpaka mtakapo pata akili ya kujua haki na wajibu wenu hapo nchini na duniani mlikuja kufanya nini kama kutawaliwa kimabavu kuburuzwa au kuongozwa kwa mujibu wa sheria mlizokubaliana
Ndiyo maana huwa najiuliza hivi katika kudai uhuru "mass" ya watanganyika walijihusisha kweli au walijikuta tu wako chini ya utawala wa weusi wenzao? Kama waliudai sasa kitu gani kilitokea baada ya uhuru kuwafanya wasiendelee kupinga dalili zozote za kuminywa uhuru ule walioupigania?
 
Sijui ni bangi, kokein, heroin au amfetamin wanayotumia wakuu wa awamu hii au ni nini kinachowapa uungu mtu.

Mwisho wa hivi vituko sifahamu ni lini. Tuvute subira!
 
Teh wasio julikana wanaanza kujulikana

Sawa mtu hatari

Yote nimemvumilia ila usenge aliofanya kukamata mtu na askari wa JWTZ haukubaliki popote .
Hizi takataka sijui zinatolewa wapi
 
Una hasira zilizojikita kwenye nadharia zaidi kuliko uhalisia. Unachoongea huko ulipo sio uhalisia uliopo hapa nchini. Kama kweli wewe ni msomi na unajua unachopigania na kujua haki zako njoo tuokoe kwani sisi tumeshindwa. Ninachokiona kutoka kwako ni kejeli na hasira za kilevi ulichotumia. Njoo huku nchini utekeleze hayo unayoamini, kinyume na hayo hapa tunakuona ni muuza face tu usiye na jipya. Unadhani haya yanayoendelea hapa nchini tunakubalina nayo, au ni jinsi ya kupambana na hali hizo? Wenzako tumejaribu kupambana kwa uwezo wetu lakini mazingira sio rafiki hivyo. Wewe unatuona sisi ni bonge ya mafala bila kuangalia mazingira. Kafie mbele.
Embu rudia kusoma ulichoandika uone jinsi kilivyo

Sasa niwasaidie kitu gani mabwege ninyi?? Nani ana hasira??

Buruzweni tuu ninyi ni ng'ombe subirini mkamuliwe maziwa mkichoka mliwe nyama
 
Kuwekwa ndani imekuwa kama kukomeshana...evidence ni pale aliposema leo Ijumaa atoke Jumatatu yaani polisi na mahabusu imekuwa kama sehemu ya kukomesha watu na si sehemu ya kutafuta haki.
 
Embu rudia kusoma ulichoandika uone jinsi kilivyo

Sasa niwasaidie kitu gani mabwege ninyi?? Nani ana hasira??

Buruzweni tuu ninyi ni ng'ombe subirini mkamuliwe maziwa mkichoka mliwe nyama

Punguwan wahed

Huna lolote ww ni muuza face tu huko ulipo, unadhani kuna mtu anashoboka ukisema uko nje? Ww utakuwa ni mtu mapenzi ya jinsia moja, unaongea utadhani ni mtu jasiri kumbe
 
Maneno yanalandana kama ya Isaya 10 : 1-4.👍
Watayatamka sasa lakini kuna siku yatatamkwa na wengine yakiwalenga wao lakini watataka kuomba msamaha lakini watakuwa wamechelewa kwani adhabu ya Mungu hapa hapa duniani itakuwa imetimia na watakuwa bado wanatafakari na kufikiria pale watakapokufa nini hasa kitatokea kwao kama Mungu amewahukumu hapa Duniani kwa adhabu kubwa hivi je Baada ya kufa itakuwaje?
 
Wanajaribu kujifananisha na aliyewateua

Jamaa sijui kawatoa wapi hawa. Sehemu ya kutumia tu busara wanatunisha misuli. CCM amkeni karne ya 21 hii sio ya kuwekana ndani au kutishiwa nyau kitoto toto
 
Ni mshamba wa madaraka na limbukeni. Yana mwisho tutapishana pale central wakati ukifika. Heri wao waliao sasa maana watauona Ukuu wa Mungu.
 
Back
Top Bottom