Rav 4 vs Xtrail

nina xtrail ya 2004 toka sbt japan, hii ni ya ukweli sana barabarani kwenye comfortability na stability vilevile inachapa sana mwendo. sina uzoefu na rv4
Hivi hizi engine specs kama xtrail s or xtrail x ipo ni nzuri zaidi..napenda xtrail nataka kuagiza
 
Mkuu tuelimishane,ukiingia kwenye mtandao kuangalia magari,kama vile SBT na Beforward,nikienda kuangalia specs za xtrail nitajuaje kuwa hii iko na turbo na nyingine haina. Nitashukuru kama niatelimishwa kwa yeyote anaejua. Natambua uzi ni wa zamani,lakini siyo mbaya kuufufua.
Nikichangia kuhusu RAV ile ya zamani ni ngumu,ila adui wake ni foleni. Angalau ile killi time ya engine ya VVTI-1ZZ iko poa. Ila usichukue ya D-4Engine,inasumbua labda kwa sababu mafuta yetu au oil zetu siyo classic.
 
Hydraulic ya Gear Box,ina utofauti gani na hizi tulizozoe kununua Total,ORYX na Puma?Je kuhusu Oil ya Diff nayo ni za kawaida au?!
 
X-Trail bomba sana...imetulia sana barabarani...
RAV 4 nimeshakuwa nayo nikaapa sitakaa ninunue ile gari aisee...kila siku shockab mbovu....mara vyuma vinagongagonga...baada ya kusikia wenzangu wana lalamika kama mie nikajua hii gari ina kaugonjwa ....utamalizia ela gereji...

Lakini X trail gari inakamata lami vizuri...imetulia sana...
Lakini X Trail nanunua tena na tena...nikiona model mpya natamani niwe nayo...
Ila RAV 4 pytu...kwanza haina space...full kubanana
 
Hydraulic ya Gear Box,ina utofauti gani na hizi tulizozoe kununua Total,ORYX na Puma?Je kuhusu Oil ya Diff nayo ni za kawaida au?!
Hydraulic ya gear box mostly ni FLUID MATIC J ambayo lita 1 ni kuanzia 50,000 (genuine) na unahitajika atleast 4 litres at per...hio ni tofauti sana na ulizotaja mkuu.
 
Baadhi ya xtrail zenye turbo utaona pale kwenye specification ina neno "GT"
 
Jamaa muongo ww khaa
 
Xtrail ni nzuri sana,hata barabarani iko stable,huyu anaesema spare zake ni shida labda ni kwa new model lakini zile za zamani spare za kumwaga ..
 
Hydraulic ya gear box mostly ni FLUID MATIC J ambayo lita 1 ni kuanzia 50,000 (genuine) na unahitajika atleast 4 litres at per...hio ni tofauti sana na ulizotaja mkuu.
Mkuu,hiyo inauzwa wapi kwa hapa Dar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…