Ratiba ya mapokezi ya Lema kesho Arusha!

Ratiba ya mapokezi ya Lema kesho Arusha!

Hii yote itagharimu kiasi gani?

He has won the case, maisha yaendelee.

Hizi sarakasi za mapokezi na maonyesho itatofautisha vipi CHADEMA na CCM.

Nilidhania watu watashauri gharama, fedha na resource hizo zipelekwe somewhere else. Arusha tayari ngome yenu. Pelekeni hizo nguvu sehemu nyingine.

Mnawapa maadui wenu points rahisi sana. Kesho UHURU likiandika "Mbowe na Lema wachoma mabilioni ya chama kusheherekea ushindi" mtashangaa?

Washabiki wa CHADEMA wana hatari ya kukiua chama chao zaidi hata ya CCM. Kwa mfano baadhi ya washabiki wengi wanapenda slogan ya "tumeanza na mungu, tumemaliza na mungu". Kwenye siasa kuna mungu? Jifunzeni kutenganisha siasa na mungu.

Katika mazingira haya ya udini ukisema "umeanza na mungu, umemaliza na mungu" ni waislam wangapi watakua tayari kuwa wanachama? Wao si watahoji Allah yupo wapi? Wahindi nao? Wasio na dini je? Chama hakina dini, mwacheni mungu wenu huko huko. Hapa shabikieni itikadi na sera za chama.

Mku mungu hana upande wote wanamuabudu
 
Ndugu introvert, 'Mungu' ni Kiswahili sanifu na fasaha kwa huyo Muumba ambaye kwa Kiarabu sanifu ni 'Allah' - neno ambali pia kwa usahihi linatumika katika muktadha wa Kiislamu kwa wazungumzaji wa Kiswahili kusisitiza chimbuko la dini yao. Kama mdau alivyojaribu kueleza, kwa vile tunazungumza katika Kiswahili ni muafaka kabisa kutumia neno 'Mungu' bila kujali imani. Hayo ya imani kwamba 'Mungu' ni wa wakristu na 'Allah' ni wa waislamu yanapenyezwa na wenye imani kali ambao inabidi ifike mahali tuwapuuzie vinginevyo nchi itasimama kama maji kwenye mtungi. Watatwambia na wimbo wa taifa tuufute ambao unasema 'Mungu ibariki Afrika... Mungu ibariki Tanzania'. Mtunzi aliyetunga huo wimbo wala hakuwa na chembe ya kubagua mtu, bali alitumia Kiswahili sanifu.

Naelewa unachosema, swali langu ni kwa nini muwape sababu hao wenye siasa kali na kwa nini msemo huo utumike kwenye chama ambacho hakijaidhinisha mungu?

Kwenye wimbo wa taifa hapo kuna kosa na wimbo huo ubadilishwe kwa sababu nchi ina watu wanaoamini na wasioamini mungu.
 
Kweli Tanzania maajabu yanazidi kuongezeka, nimesoma ratiba ya mapokezi ya mbunge wa Arusha mjini bwana LEMA eti ataenda kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa na chama tawala, barabara ambazo hata kumi hakuchangia, kusimamia wala kuratibu! cha kushangaza sijui hata kama ana uelewa wowote wa mambo ya UHANDISI wa barabara hadi akakague.... mi nilifikiri muda huu bwana LEMA angeacha mbwembwe na kutafuta umaharufu binafsi na kujikita zaidi katika ILANI za chama chake na kutekeleza ahadi zake alizowahaidi waNAARUSHA ambazo karibu zote hajazitekeleza zaidi ya kujitafutia umaharufu binafsi ambao hauna tija kwa WANAARUSHA na wanaCHADEMA WOTE TANZANIA
 
Acha upopompo wewe.
Wanachama wa cdm wana imani zao na ndio wanaosema hivy, siyo katiba ya chama!! tumia common sense.

Mwislamu anayekipenda Chadema ruksa kusema -Tulianza na Allah, tutamaliza na Allah! na Mhindi nae ruksa kutaja anachoamini...lakini general term ni MUNGU.!

Wewe uko overSensive na dini wewe, na watu wa aina yako ndiyo wanaovuruga nchi hii. Tuache tafsir fyongo.

Nipo oversensitive kwa sababu vitu hivi havichanganywi. Watu wa aina yangu hatuwezi kuvuruga nchi, ila nyinyi mnayoyaona haya na kupuuzia.

Tulianza na Mungu na tumemaliza na Mungu,wao wanapesa CCM sisi Chadema tunaMUNGU tunayempigania

Hii imekua crusade au jihad? PakaJimmy mtu kama huyu si wa kupuuza na kusema niko oversensitive.
 
kama kuna jambo unalifanya bila Mungu basi ni ovu. Lazima uanze na Mungu na endelee kuwa nae mpaka mwisho. Allah si kiswahili ila inamaanisha Mungu. Wahindi, budha, waislam, wakristo wote wakisema Mungu wanamaa Mungu

That's another debate for some other time. Chama hakina dini wala mungu. Mwanachama ana uhuru wa kuabudu au kutoabudu at his/her own personal time si kutumia mgongo wa chama kuleta misemo ya mungu. Period.
 
kweli tanzania maajabu yanazidi kuongezeka, nimesoma ratiba ya mapokezi ya mbunge wa arusha mjini bwana lema eti ataenda kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa na chama tawala, barabara ambazo hata kumi hakuchangia, kusimamia wala kuratibu! Cha kushangaza sijui hata kama ana uelewa wowote wa mambo ya uhandisi wa barabara hadi akakague.... Mi nilifikiri muda huu bwana lema angeacha mbwembwe na kutafuta umaharufu binafsi na kujikita zaidi katika ilani za chama chake na kutekeleza ahadi zake alizowahaidi wanaarusha ambazo karibu zote hajazitekeleza zaidi ya kujitafutia umaharufu binafsi ambao hauna tija kwa wanaarusha na wanacdm wote tanzania

wacha kukurupuka weweeee.pesa zilitolewa na wb viongozi wa mkoa wakazikalia bila kuzitumia kwa kisingizio wanafanya upembuzi yakinifu,huku wakizitumia pesahizo kulipana posho za vikao. Baada ya chadema chini ya kamanda lema kuanza kupiga kelele ndipo wakashtuka na kuanza kazi ya ujenzi wa barabara.wakati huo wb walisha tishia kuzirudisha.
 
Acha upuuzi wako,Gamba namba moja,nakushauri Vua Gamba Vaa Gwanda,Hivi Rais anapoapa anakamata nini mkononi na akimaliza kuapa anatamka"MUNGU NISAIDIE".Wabunge nao huapa,hata kabla ya kikao cha bunge wanaanza kumwomba Mungu.

Kwa sababu napinga msemo huo mimi automatically nakuwa gamba. So much for great thinking.. Prof. Baregu aliapa kutumia nini?

Ni mambo mangapi magamba wanafanya wakati kuna watu wanalala njaa,Tisheti za kijani na kofia bureeeee!!!!.Uwe unajaribu kufikiria kabla ya kupost.

Mambo ni mengi, haimaanishi tufungie macho baadhi ya mambo na mengine ndiyo tukemee zaidi. Tukemee yote.
 
Hivi unajua majukumu ya Mbunge? Au unadhani Lema ni muhuni kama wewe? Atakagua miradi mingi zaidi ya iliyomo ndani ya ratiba...Ikijengwa chichi ya kiwango nyie ndo wakwanza kusema mbunge kala hela za makandarasi...Hiyo miradi haijengwi kwa fedha za magamba bali ni kodi zetu...hata wewe unaweza kwenda kukagua na kujiridhisha kwa muda wako kwani barabara hizo hawapiti wanachama wenu tu bali ni miradi ya watanzania...Uwe unafikiri kabla ya kuweka post humu...
 
Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.Nina wasiwasi na brain capacity yako.Kikwete anapokuwa anazindua barabara sehemu mbalimbali nchini yeye ni Mhandisi?Huu ni uzuzu wa ajabu.Haihitaji kuwa mhandisi ujue kalvati au mtaro umejengwa chini ya kiwango.Ni akili ya kawaida tu inatosha.
 
wewe ndio kilaza kabisa, nani alikuambia barabara zinajengwa na CCM? serikali ndio inakusanya hela kwa watanzania wote, CCM wanasimamia tu.....anawajibu wa kuzikagua na kuhoji kama haziko katika viwango
, kwani yeye anawawakilisha wanachi wa Arusha

Kweli Tanzania maajabu yanazidi kuongezeka, nimesoma ratiba ya mapokezi ya mbunge wa Arusha mjini bwana LEMA eti ataenda kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa na chama tawala, barabara ambazo hata kumi hakuchangia, kusimamia wala kuratibu! cha kushangaza sijui hata kama ana uelewa wowote wa mambo ya UHANDISI wa barabara hadi akakague.... mi nilifikiri muda huu bwana LEMA angeacha mbwembwe na kutafuta umaharufu binafsi na kujikita zaidi katika ILANI za chama chake na kutekeleza ahadi zake alizowahaidi waNAARUSHA ambazo karibu zote hajazitekeleza zaidi ya kujitafutia umaharufu binafsi ambao hauna tija kwa WANAARUSHA na wanaCDM WOTE TANZANIA
 
Wabunge wamejitolea kulipia magari yao na helikopta zao, malazi, service za magari, chakula na madereva wao. Wananchi wanachanga kufanikisha mkutano. Lengo ni kuhamasisha Tanzania nzima na sio jimbo la Arusha mjini peke yake. Macho na masikio ya Watanzania wengi sana kwa siku ya leo yatakuwa Arusha. Kuna kura nyingi sana zitapatikana leo nchi nzima kwa mambo yatakayofanyika jijini Arusha. We are gaining political momentum.

Waste of resources ni pale unapohonga watu wakafungue kesi za usumbufu zisizo na mbele wala nyuma. Kupoteza hela za walipa kodi kwa mahakamani kuendesha kesi ambazo kwa makusudi kabisa zimefunguliwa kujaribu kuwa keep wabunge wa CHADEMA busy wasiweze kufanya kazi yao vizuri bungeni.

Nakubali inaweza influence voters across the country. Upande wa pili inaweza kuonekana ni matumizi mabaya ya rasilimali kwani Arusha tayari ni ngome ya CHADEMA. Hiyo nguvu ingeelekezwa kwingine ambapo siyo ngome pia inge-influence voters across the country vilevile au na zaidi.

You do not gain a political momentum at your base. You gain it in places you have less votes.
 
Back
Top Bottom