Hivi unajua nini misingi ya utawala wa serikali zilizoko duniani?
Hapana sijui. Ila kwa uelewa mdogo tu, serikali za nchi tofauti zina misingi tofauti.
Kama kila mtu ana Mungu wake (ambao ndio ukweli)
Si kweli. Kuna ambao hawaamini mungu.
..na huyo Mungu hajaidhinishwa na chama kuna ubaya gani wanachama kumsifia Mungu wao?
Hakuna ubaya kwa manachama kumsifia na kumuabudu mungu wake au kutoabudu at his/her own personal time. Kutumia msemo wa tulianza na mungu, tunamaliza na mungu ni kukinzana na chama ambacho hakijaidhinisha mungu.
Kwa wasio muamini Mungu madhali hawabaguliwi kwa imani yao kuna shida gani
Shida ipo kwa sababu mungu huyo hajaidhinishwa na chama lakini washabiki nyie mnaidhinisha na kutumia msemo ambao unabagua wasioamini mungu.
Pia
"tulianza na mungu,
tunamaliza" inaonyesha wingi wa watu, kitu ambacho si kweli. Mzee Baregu na wanachama wengi tu mnawatenga hapa.
Kuna mwanachama ambaye aliambiwa sifa ya kuingia kwenye chama ni kumwamini Mungu? Tuhuma za udini, ukabila, ukanda, ubaguzi, usomi, upendeleo na yanayofanana na hayo katu hazitakoma wala hazitaachwa kutolewa maana ndiyo silaha pekee waliyo nayo maadui wa CHADEMA.
Kama unajua hilo kwa nini muwape watu points za kirahisi na vitu vya kuongea. Shehe akiwaambia waumini wake "waone wale na msemo wao, hakuna mungu mwingine wanaomzungumzia isipokuwa wa kikristo".. Huoni unawasaidia waeneza propaganda hizo? Kwa sababu mungu hajaidhinishwa na chama kwa nini usitumie msemo mwingine wenye sera za chama uepuke maneno maneno ya propaganda?
Hata wahenga walisema Wanadamu (FISI WENU) ngwamba hawaachi kwamba. Watasema tu labda uwanyang'anye ndimi zao. Lakini hiyo isiwazuie wanachama wao kumsifu Mungu wao kila mmoja kwa imani au dini yake.
Kila mmoja afanye kwa muda na nafasi yake lakini si kutumia mgongo wa chama ambacho hakijaidhinisha mungu.
Hali mbaya iliyoko FISI WENU na serikali yake haitokani na kumkumbatia Mungu bali ni kinyume chake. Hivyo kusema kuwa tusichanganye dini na siasa ni sawa lakini Mungu na siasa hawagombani na Yeye ndiye muanzilishi wa siasa (kwa taarifa yako).
Kama mungu na siasa hawagombani kwa nini siasa na dini hazichanganywi? Mungu kuwa muanzilishi wa siasa that is another debate for some other time.
Binadamu asipokuwa na hofu ya Mungu maovu yake yanakithiri, huharibu siasa na vitendo vyake vinamzidi mnyama.
Kuna research yoyote juu ya hili kwa sababu kutumia reasoning kidogo tu, "maovu" hutendwa na watu tofauti wenye imani na wasio na imani.
Tanzania imekuwa na hali mbaya kwa sababu watawala (si viongozi) wake hawana hofu ya Mungu japo wana dini zao.
Smh..
Huyu Mungu anayesifiwa na watu humu ni yule ambaye hana dini, anayeaminika kuwa muumba wa vinavyoonekana na visivyoonekana.
Chama hakijaidhinisha huyu mungu mwenye dini au asiye na dini hivyo msifu huyo mungu at your own private time si kwa kutumia mgongo wa chama.
Anayenyeshea mvua wabaya na wema.
Miaka 51 ya uhuru hiyo mvua imelenga watu gani wanaoteseka? Usichanganye haya mambo.
Mwenye kuangaza kwa jua mchana na mwezi usiku na kutupa pumzi ya bure siku zote bila kujali uovu wala utakatifu wetu. Tofauti zetu za aina zote kwake yeye ni mapambo kama yalivyo maua machoni mwetu. Kwake hakuna mkristo wala muislam, hakuna kafiri wala mpagani maana wote twaitika kwake. Huyo ndiye anayestahili kusifiwa. Huyo ndiye kwenye siasa na mambo mengine muhimu unapenda kuanza naye na kumaliza naye.
Kama ni hivyo kwa nini Scandinavians ambao wengi hawaamini mungu wana low crime rates, low levels of corruptions, good standards of living compared na waafrika ambao wengi wanaamini mungu?
Kwa kweli ni vema tena inapendeza "KUANZA NA MUNGU NA KUMALIZA NA MUNGU".
Chama hakijaidhinisha mungu kwa sababu za kutochanganya siasa na dini/mungu, hivyo msemo huo usiutumie kwa mgongo wa chama. Kama mmeshindwa kuelewa na hapa basi tena.