Huwezi kusema haina gharama. Kuna wabunge na viongozi wa chama wanasafiri kutoka Dar mpaka Arusha. Kuna gharama za malazi na chakula. Kuna helikopta na magari, hapo kuna gharama za mafuta, services, kulipa madereva etc. Kuna gharama za vyombo vya sauti siku ya mkutano and all that. Hata kama ni pesa yao mfukoni, haina maana, kwa sababu haya yote yanafanywa kwenye jimbo ambalo hata kesho asubuhi uchaguzi ukifanyika chadema itashinda. Huoni kama ni waste of resources?
Kuhusu mungu, dini na imani.. Elewa misingi ya kutochanganya siasa na dini. Leo hii ukiulizwa CHADEMA ni dini gani au inabudu mungu yupi, jibu ni kwamba haina dini wala mungu. Kuna wanachama wa imani tofauti na kuna wasioamini mungu.
Unaelewa kwamba sasa hivi kuna mazingira na harufu ya udini. Mfano ni majibizano na michango ya members hapa. Sasa kama CHADEMA inashutumiwa kuwa chama cha kikristu na wewe unasema "tulianza na mungu, tunamaliza na mungu" .. Hii slogan itatafsirika vipi?
Siasa na dini/mungu havichanganywi. Dini/mungu, that's your personal thing.
ndugu yangu wewe huijui Arusha.hizo helkopter,magari,pikipiki ni mali ya watu binafsi!havijakodiwa na hela za chama kama wafanyavyo ccm.CDM watu hujitoa mwanzo mwisho.hawahitaji kubebwa,kula pilao,kugawiwa kanga,T.shirt,kofia wala tsh.2000/-usifananishe cdm na ccm ya J.KIKWETE.Hii yote itagharimu kiasi gani?
He has won the case, maisha yaendelee.
Hizi sarakasi za mapokezi na maonyesho itatofautisha vipi CHADEMA na CCM.
Nilidhania watu watashauri gharama, fedha na resource hizo zipelekwe somewhere else. Arusha tayari ngome yenu. Pelekeni hizo nguvu sehemu nyingine.
Mnawapa maadui wenu points rahisi sana. Kesho UHURU likiandika "Mbowe na Lema wachoma mabilioni ya chama kusheherekea ushindi" mtashangaa?
Washabiki wa CHADEMA wana hatari ya kukiua chama chao zaidi hata ya CCM. Kwa mfano baadhi ya washabiki wengi wanapenda slogan ya "tumeanza na mungu, tumemaliza na mungu". Kwenye siasa kuna mungu? Jifunzeni kutenganisha siasa na mungu.
Katika mazingira haya ya udini ukisema "umeanza na mungu, umemaliza na mungu" ni waislam wangapi watakua tayari kuwa wanachama? Wao si watahoji Allah yupo wapi? Wahindi nao? Wasio na dini je? Chama hakina dini, mwacheni mungu wenu huko huko. Hapa shabikieni itikadi na sera za chama.
Acha upopompo wewe.Kuhusu mungu, dini na imani.. Elewa misingi ya kutochanganya siasa na dini. Leo hii ukiulizwa CHADEMA ni dini gani au inabudu mungu yupi, jibu ni kwamba haina dini wala mungu. Kuna wanachama wa imani tofauti na kuna wasioamini mungu.
Unaelewa kwamba sasa hivi kuna mazingira na harufu ya udini. Mfano ni majibizano na michango ya members hapa. Sasa kama CHADEMA inashutumiwa kuwa chama cha kikristu na wewe unasema tulianza na mungu, tunamaliza na mungu .. Hii slogan itatafsirika vipi?
Siasa na dini/mungu havichanganywi. Dini/mungu, thats your personal thing.
well said mkuuMkuu hapo kwenye RED, hatuwezi kumpigania MUNGU, hatuna uwezo huo, lakini MUNGU ndiye anayetupigania, sisi tu viumbe dhaifu sana kwa CCM kiasi kwamba bila MUNGU kuwa kati yetu, hatuwezi chochote.
MUNGU atakuwa nasi daima hadi hapo ukombozi wa nchi hii utakapokamilika 2015
Ratiba ya Lema Kesho:
Mapokezi KIA kuanzia Philips saa 2:00 Asubuh
Kwenda kufungua ofisi ya Mbunge kuanzia saa 5:00 Asubuhi
Ukaguzi wa Barabara Zilizojengwa kuanzia saa 6:00 Mchana
Kusalimia akina mama waliomuombea sokoni 7:00 Mchana
Mkutano Kilombero saa 8:00 Mchana
WOOTE MNAKARIBISHWA!
Msafara utakuwa unaongozwa na Wabunge wa Chadema toka Dar es salaam na utahutubiwa na viongozi wa Kitaifa. Msafara huo pia utaongozwa na Helkopta, pikipiki, magari, baiskeli na watembea kwa miguu, maandamano yataanzia Philips hadi ofisi za Mbunge kuelekea viwanja vya kilombero!
Peeoplesssssss!
Nakuja ngoja ninywe chaikaribuni Philips kushaanza kupendeza mambo mwanjamwanja!
Hiyo ratiba ya kwenda kuwasalimia akina Mama wa soko la NMC itakuwa ya Hisia kali sana, wallahi nasema kuna watu hapo watalia machozi ya damu.
Hawa akina mama kwa mamia ni watu walioteseka sana kwa shuruba za polisi na wagambo wa ccm.
Wamekimbia sana wanawake hawa, wameumizwa, wamepoteza fedha na jewellery, kisa kuwakwepa wagambo wanaowatimua huku wakiwa wamebeba vichwani bidhaa zao.
Akina mama hawa bila kujali kupoteza muda, bila kujali nini kingewatokea, bila kujali dini zao, makabila, ukanda, asili, wala umri, walikusanyika kupiga MAOMBI YA AJABU pale NMc, wakimsihi Mungu atawalaye, asimamie hukumu ya G.Lema ili isiingiliwe na maamuzi ya akili za kibinadamu.
Imagine katika mazingira kama hayo, huyo m'baba kesho anafika eneo hilo kwaajili ya KuWASALIMIA TUakina mama hao.
Ni kipengele kipengele kitakachokuwa na mvuto ajabu.
philips tayari marai tupo hapa
Mkuu hapo kwenye RED, hatuwezi kumpigania MUNGU, hatuna uwezo huo, lakini MUNGU ndiye anayetupigania, sisi tu viumbe dhaifu sana kwa CCM kiasi kwamba bila MUNGU kuwa kati yetu, hatuwezi chochote.
MUNGU atakuwa nasi daima hadi hapo ukombozi wa nchi hii utakapokamilika 2015