- Source #2
- View Source #2
Kupitia mitandao ya kijamii, kumekuwepo taarifa inayodai kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, amejiunga rasmi Chama Cha Mapinduzi (CCM). Chapisho hilo linadai: “Rasmi Freeman Mbowe ametimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM).”
Chapisho lina ujumbe ufuatao:Kwa muda mrefu, zimekuwa zikisambaa fununu zinazodai kuwa Freeman Mbowe alikuwa akisurubuisha au kukisaliti chama chake, CHADEMA. Taarifa hizo zimehusishwa pia na mabadiliko ya uongozi ndani ya chama hicho, ambapo Tundu Lissu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Hata hivyo, kupitia ufuatiliaji wa maneno muhimu yanayohusiana na taarifa hiyo, hakuna taarifa rasmi iliyobainika kuthibitisha kwamba Freeman Mbowe amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aidha ufuatiliaji zaidi kupitia mitandao ya kijamii ya CCM na freeman mbowe hakuna ushahidi unaonyesha kuwa mwenyekiti huyo amejiunga rasmi wa chama cha CCM na vyombo vya habari vikubwa nchini tanzania havikuchapisha taarifa hiyo hivyo kuthibitisha kuwa taarifa hiyo ni potoshi
Licha ya kutokuwepo kwa uthibitisho, chapisho hilo linalopotosha linatumia mbinu mbalimbali za kuwashawishi watumiaji kubofya viungo vinavyowaelekeza kwenye makundi sogozi ya mitandaoni
Sambamba na hilo picha ambayo imetumika kuelezea chapisho hilo imetengezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde