Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Status
Not open for further replies.
Wajameni,
Naongezea kidogo tu. Marehemu John Kennedy aliwahi kumchagua mdogo wake Robert kuwa Attorney General. Wamarekani wengi wanakubali kuwa he was the best Attorney General. Lakini bunge likapitisha sheria kuwa rais asiwe na haki ya kumchagua ndugu yake, mke wake, mtoto wake kushika nafasi muhimu serikalini. Inaitwa nepotism!
 
Jasusi said:
Wajameni,
Naongezea kidogo tu. Marehemu John Kennedy aliwahi kumchagua mdogo wake Robert kuwa Attorney General. Wamarekani wengi wanakubali kuwa he was the best Attorney General. Lakini bunge likapitisha sheria kuwa rais asiwe na haki ya kumchagua ndugu yake, mke wake, mtoto wake kushika nafasi muhimu serikalini. Inaitwa nepotism!
Jasusi I dont get you properly and I beg ur padon..does this implies that b'se a president is a muslim he should not have appointed RO as DG even if he does posses all the potential? clarify please!
 
Bw. Rashid Nampongeza sana kwa kuchukua nafasi hiyo!.. Ni kijana shupavu na sisi wanamaskani wa Maisara tunajua hilo, na wala haitaji kuweka cv yake hadharani, kwa kuwa tu baadhi ya watu hawamjui...!
 
Unajua niye vijana msiingilie mambo kwa pupa, mambo ya Othman tuliyajadili mwaka jana kule BCS alipoanza kujigamba mitaani kuwa atakuwa mkuu mpya wa usalama, kama JK akishinda. Sasa nyinyi kinachowafanya muwe so hyped na hii issue sielewi ni nini,

Kama ni data hamna, tena hata kuwaita usalama ni kuwapa cheo cha bure maana mzee wa usalama Babu Ubwete alikuwa na data, nyinyi hamna data, ila ni watapeli tu mnataka kupewa data hapa,

Mimi data ninazo tena sio tu ninazo ila kila siku kazi yangu inanipa opportunity ya kuziona data in making, kwa sababu ninawaona watengeneza data kila siku, haya nimewapeni data za kutosha kwa rookies wa hii forum, nyinyi hata huyo Othman I doubt kama mnamjua zaidi tu ya blah! blah! hapa,

One thing tu ni kwamba mko London, na mlikuwa mnamuona lakini hamumjui, yes, kuvamia kwenu hii forum ni plus kwa forum na tunawaomba hiyo nguvu yenu muiweke kwenye kila issue sio ya Othman tu, halafu msikimbie baada ya michango michache,

But, hata kama anawatuma huyo jamaa, mwambieni nipo hapa na ninazo data, Itatiro ni mshikaji wangu na nimesoma naye shule, nimefika mpaka kawo Mahenge Kuliboma, sina mpango wa kumjadili hapa, na pia ameoa cousin wa mshikaji wangu mwingine ambaye ni owner wa Clouds, Mzee Kusaga, kwa hiyo sio kwamba ninamsikia kwenye radio au magazeti,

Cha maana mnachoweza kufanya ni kumwambia Mzee JK, kuwa wananchi wanafuatilia mambo yake kwa makini na hawezi kumpandisha mkenge mtu yoyote, yote anayoyafanya tunayaona, na huyu mzee EL naye mumwambie kuwa aache kutafuta 10% kwa Wahindi mwambieni tunayaona yote na jinsi Wahindi wanavyomkimbia, na hasa huyo agent wake anayemtuma, tunayaona yote hatujalala,

Ninarudia tena kuwa kwa maoni yangu Othman, hana uwezo wa kufanya kazi aliyopewa, na amepewa kwa kujuana na sio uwezo wa kikazi, NO! sasa kuendelea na haya makelele bila data ni waste of time ya wananchi, nyinyi mnadai kuwa anao uwezo, na mimi ninasema hata aliyempa uwezo wa kutuongoza hana, ndio maana anakuwa rafiki na watu kama anaowapa kazi nzito, hapa nitoe heshima zangu kwa Mzee Ng'wandu, kwa kuapa kuwa ni bora afe kuliko kuendelea na siasa ya bongo!

Off course I am a little bit impressed, yaani mmenikumbusha BCS kidogo ila tatizo tu hamna data na siwezi kuendelea kuwapa, ila mkizitoa tu anytime niko ready, nimetoa data za kutosha kwenye hii mada, mimi ni imara naona mzee mmoja hapo unaniota maana kila maneno matano lazima unitaje taje, badala ya kuweka data, CV ya Othman ndio hiyo hiyo ya kusoma Bulgaria, na kuruka vyeo kama ndege, haya yote yanawezekana ONLY IN TANZANIA!
 
Mzee Hakimbiwi mtu hapa hata siku moja, na hatubadili majina hata siku huku tukitoa maneno yale yale, ndio maana wanaforum wanakuwa "BIASED" maana wanaona ujinga at its best,

Wanaona jinsi juha mmoja anavyojaribu kujigeuza kuwa majuha wengi ili akubalike kwenye forum, maana huyu juha mmoja hajui kuwa hata akiingia na jina lake moja linatosha kinachotakuwa hapa ni message, ila masikini juha kama Yohana mjinga aliyeweka maziwa kwenye mfuko wa suruali haelewi kuwa ni juha!

Hakimbiii mut hapa, mbuzi weee!
 
Ninaungana na Mzee Es kuuliza kwamba kwa nini watu wote wapya maongezi yao yako kwenye hii mada tu na si zaidi ya hii ? Kunani hapa ?
 
Wanabodi,

Hodi hodi na heshima zenu, hapa naona mambo ni mazito lakini maadamu tunajadili mustakabadhi wa taifa letu nawaombeni busara itumike tujadili kwa busara na kuheshimiana.
 
Mzee Kibunango,

Heshima yako mkuu, ni siku nyingi toka enzi zilee sijakusia, karibu mzee bado tupo tunaendeleza yale yale, nimekusikia mkuu na point yako ni clear bila matusi na inaeleweka,

Halafu kwa wenzetu wenye majina mengi ambayo we cannot keep it up nayo, hebu jibuni maswali ninaona kuna maswali mengi wanabodi wanawauliza lakini hayajibiwi ila ni Es tuuuuuuuuuuu!,

Kuna mzee anauliza miaka ya aliyosoma hizo shule huyo Mzeee? Mimi sikujua kuwa Ilboru shule aliyosoma Mtikila ina sifa kiasi hicho mbona makubwa haya!,

Kwa Mzee Yomba Yomba,

Heshima yako mkuuu, hatupendi matusi ila tu tunalazimishwa na wageni bro!, wewe ndie mgeni mmoja tu in the last one week kuingia bila matusi karibu na message yako imeeleweka bila hata ya kutukana!
 
Kivuli, Wangekuwa siyo hao misheni sasa hivi wewe na Raisi wako mngekuwa mnaongea kiarabu na zaidi ya hapo mngekuwa Iraq wearing suicide bombs!
 
kulingana na maelezo ya Mtafiti inaelekea RO ana elimu na uzoefu wa kazi kustahili madaraka aliyokabidhiwa. Tumuache afanye kazi yake.

naona pia topic imechukua sura ya ushabiki wa kidini na inachefua kupita kiasi.
 
WHAT AUSTRALIA HAS SAID

What a great way of saying the truth. England should really pay attention and listen to this Australia speech: Muslims who want to live under Islamic Sharia law were told on Wednesday to get out of Australia, as the government targeted radicals in a bid to head off potential terror attacks. A day after a group of mainstream Muslim leaders pledged loyalty to Australia at a special meeting with Prime Minister John Howard, he and his ministers made it clear that extremists would face a crackdown. Treasurer Peter Costello, seen as heir apparent to Howard, hinted that some radical clerics could be asked to leave the country if they did not accept that Australia was a secular State and its laws were made by parliament. "If those are not your values, if you want a country that has Sharia law or a theocratic state, then Australia is not for you", he said on national television. "Immigrants, not Australians must adapt. Take it or leave it. I am tired of this Nation worrying about whether we are offending some individual or their culture. Since the terrorist attacks on Bali, we have experienced a surge in patriotism by the majority of Australians. However, the dust from the attacks had barely settled when the"politically correct" crowd began complaining about the possibility that our patriotism was offending others. I am not against immigration nor do I hold a grudge Against anyone who is seeking a better life by coming to Australia. However, there are a few things that those who have recently come to our country, and apparently some who were born here, need to understand. The idea of Australia being a multicultural community has served only to dilute our sovereignty and our national identity. As Australians we have our own culture, our own society, our own language and our own lifestyle. This culture has been developed over two centuries of struggles, trials and victories by millions of men and women who have sought freedom. We speak mainly ENGLISH, not Spanish, Lebanese or Arabic, Chinese, Japanese, Russian, or any other language. Therefore, if you want to become part of our society, .learn the language. Most Australians believe in God. This is not some Christian, right wing, political push but a fact Because Christian men and women, on Christian principles, founded this nation, and this is clearly documented. It is certainly appropriate to display it on the walls of our schools. If God offends you, then I suggest you consider another part of the world as your new home, because God is part of our culture. We will accept your beliefs and will not question why, all we ask is that you accept ours and live in harmony and peaceful enjoyment with us. If the Southern Cross offends you or you don´t like a "Fair Go" then you should seriously consider a move to another part of this planet. We are happy with our culture and have no desire to change and we really don´t care how you did thingswhere you came from. By all means, keep your culture but do not force it on others.

This is OUR COUNTRY, OUR LAND, and OUR LIFESTYLE and we will allow you every opportunity to enjoy all this. But once you are done complaining, whining and griping about our Flag, Our Pledge, Our Christian beliefs or Our Way of Life, I highly encourage you to take advantage of one other great Australian freedom: THE RIGHT TO LEAVE. If you are not happy here then LEAVE. We didn´t force you to come here. You asked to be here. So accept our country . "I´d be saying to clerics who are teaching that there are laws governing people in Australia, one the Australian law and another the Islamic law. That is false. If you can´t agree with parliamentary law, independent courts, democracy and would prefer Sharia law and have the opportunity to go to another country, which practices it, perhaps, then, that´s a better option" Costello said. Asked whether he meant radical clerics would be forced to leave, he said those with dual citizenship could Possibly be asked to move to the other country. Education minister Brendan Nelson later told reporters that Muslims who do not want to accept local values should " clear off " Basically, people who don´t want to be Australians and they don´t want to live by Australian values and understand them, well then they can basically clear off" he said. Separately Howard angered some Australian Muslims on Wednesday by saying he supported spy agencies monitoring the nation´s mosques.

England .ARE YOU LISTENING ??
 
Ila anachosema kivuli kina ukweli ndani yake!!!

Viongozi wengi wametuibia sana na walikuwa wakristu!!

Lakini anapokosea ni pale anaposema jamaa ni papa!


Ila ninakubaliana naye kuwa inaonekana hii topic ni beef kati aya watu wa Mahiga. Na kuna wengine kazi yao ni kuvuruga mjadala wa kushabikia bila kama vile wamenyweshwa dawa!!

Ila pia kuna ukweli kuhusu ushabiki wa dini!!!

Why Mahiga??
Na hili ni baya zaidi!!

Muacheni RO achape kazi. Ila tu ajue watu wako macho na tunamtegemea alibebe jahazi la usalama wa viongozi vizuri na Usalama wa viongozi punguzeni kunyanyasa wananchi wenye mitizamo tofauti au wanaokuwa na mawazo tofauti na usalama wa viongozi wenu!!!


hii topic ifutwe maana matuzi sana ni babu kubwa ninona hata SAM has lost .....

bye
 
Mkuyuga,
Unajua wale wote wanaoshabikia UDINI ni kama wewe wanaosema kuwa Wakristu wametuibia sana. Hebu niambie Mwaka 1985 hadi 1995 kiasi gani cha pesa kiliibiwa? Tanzania ya wakati ule ilikuwaje? Rais alikuwa mkristu? Kigoma, Mwinyi, Chavda nk walikuwa nani hao? Can you explain rule of law, good governance between 1985 1nd 1995? Hivi mmesahau? Ok sio ukristu au ui Slam, ni weakness ya watu kama ninyi ambao mnatumiwa na dini na kujisahau kuwa ni watanzania; that is most slavery than any! The good thing is that christian do not think that they are a part of a christian culture or in other words european, but you guys are ready even to kill to serve for the Islamic-Arab culture!
 
My original beef ilikuwa ni kwamba Othman hana uwezo wa kazi aliyopewa, na kwamba amepewa kwa upendeleo,

Sasa ya Mahiga, Itatiro, Udini, Matusi, Ma-PAPA Pepe-Kale, Mtoto wa kijiweni na maskani, ni nini na yametoka wapi? Ninaona guys now you are making good of your intentions yaaani kuivuruga mada, halafu mnaonekana kuwa mna obsession na ES, maana haliwatoki jina What is up?

Hakuna anayemzuia Othman kufanya kazi yake mbona Kombe hakuna aliyemzuia pamoja na uwezo wake mdogo alifanya baadaye ukweli ukajisema ndio uzuri wa huko usalama, wazee wa huko hawana mchezo,

nitaisema point moja tu ambayo ninaiona kuwa ni kichekesho, kuwa Mahiga hawezi kuwa mkuu wa usalama bongo kwa sababu ta technologia, lakini anaweza kuwa Mwenyekiti wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, UN?

I mean nimeona mnajitahidi kumpalilia Othman good works, lakini mbona mmegeuka kuwa Simba na Yanga? Halafu acheni matusi, hivi nyinyi watu wa kambi ya JK/Othman, mbona siku zote mpaka muwe na matusi?

Mimi Es nimeona kazi yenu lakini bado I am not convinced kuwa Othman ana uwezo wa kazi hiyo, kwa hiyo ningewaomba tukubaliane kutokubaliana matusi na kutuletea Wazaire kina papaaaaaaa! tena kwenye usalama mara Saigon mbona mnataka kutupeleka vichochoroni? Hakuna anayemzuia Othman kufanya kazi, wala bosi wake JK, lakini ni lazima tuwazungumze.

Hiyo ni haki yetu, hakuna wa kumzuia mtu hapa hata awe papa wa zela mbongo! Hapa tusema tuuuu!
 
Chonde nawaomba watu wa matusi waniachie mada yangu .Mimi na wale wakata issue tuendelee kuuuliza juu ya Mzee wetu RO na ukingunge alio ukwaa Mwenye matusi afungiwe kabisa hafai .

tafiti nimesoma mabishano yako na Muggy leo juu ya Ubalozi Holland na kwa bahati nzuri I know the story kwa undani mno kuanzia sasa siamini hata maneno yako uliyo yaleta juu ya RO wewe una lako jambo kama umeweza kugeuza maneno kule ili uaminiwe wakati ukweli unajulikana wazi je nitawezaje kukuamini na habari zako ndefu za RO ?
 
Wakati Mzee Kombe anakuja London na kukutwa na Dola laki tatu hotelini na wazee wa M16, mara mbili je huyu mzee wako mahiri RO wa usalama akiwa pale alifanya nini? Na kama kweli alikuwa mahiri ilikuwaje wazee wa M16 wakazirudisha bongo hizo hela wenyewe?

One thing ni lazima nikubali kuwa umejitahidi katika kumtetea RO na hasa hapa mwishoni, off course kuna some of the positives ninaziona kwenye maneno yako ingawaje mengi ni kamba na siasa za propaganda, lakini kuna some ukweli kwa hiyo mzee ulipoanza nilikuwa na 10% positive tu on RO, sasa angalau umeniongezea nimekuwa na 25%, na hasa huu mchango wako wa mwisho, ila tu ninakuomba upunguze OBSESSION na mimi, maana inakufanya uwe blind na kupoteza maana ya hoja pale unaponing'ang'ania tuuuuuu, humu kuna wazee kama kina Aljazeera ambaye ni mwalimu huko Mlimani wamekuuliza maswali, na kuna watu wengi wamekuuliza maswali lakini huwajibu umekazana na mimi tu,

Sikiliza bro! Bongo ni nchi yangu na JK ni mshikaji wangu wa damu, lakini akikosea sina msamaha, nilipokuwa kambi ya JM wakati wa uchaguzi nilikuwa ninamuambia ukweli all the time, baada ya uchaguzi nikamuambia with a straight face kuwa familia yangu lazima ile na iendelee kutesa kwa hiyo I have to go with the winner, lakini we remain friends, nafikiri hio inakusumbua maana unaonekana huna mazoea ya watu kuelewa na kuishi na reality,

Sasa unajaribu kumfanya RO kuwa ni malaika, yaani hiyo ndio tunaita blind love huuoni ukweli kabisaaa, kuwa amerushwa vyeo kwa kasi ambayo sio ya kawaida, kwamba ni mwaka jana tu alikuwa London kabla ya uchaguzi, ila in the between ameweza kuwa assistant mpaka mkurugenzi, hiyo inawezekana tu kwenye Ari mpya na kasi mpya bro! Mimi siunamapenzi ya kijinga bro, ukweli ninakubali lakini uozo hapana, toka JK awe rais positive nilizoziona na kuzisifia ni,

(1). Hotuba yake ya kwanza bungeni,
(2). Alipochagua makatibu wa wizara,
(3). Alipofumkuza Mahalu na kutangaza kuwa ni sababu ya wizi, ( I consider this to be the best moment of his presidency so far),
(4). Alipokataa kukaa hoteli za dola 5,000 kwa siku huko majuu na (ambazo BM alikuwa akiiishi huko nje na bado mpaka leo bado anazitumia sijui nani anazilipia!
(5). Alipomchagua EL kuwa PM
(6). Alipomlazimisha Mahita kuondoka kabla ya wakati,

That is all niliyoyaona, now guess what kwenye hayo yote hakuna hata moja la kuwasaidia wananchi kundokana na umasikini, au kuongeza uchumi, au kuongeza uzlishaji wa kilimo, au kuongeza ajira!

I do not care watu wengi wasio na uwezo aliowachagua, lakini kwenye Makamba, RO, na Mapuri, hapo nimekataa kabisaa kuwa haukuwa uchaguzi mzuri au wa haki kwa taifa na wananchi waliomchagua, hakuwafanyia haki na ninarudia kuwa kadri ninvyoongea na watu wa huko kwa RO, ndio ninazidi kuionea huruma nchi yangu, ila sitatoa data tena on him maana kwenye hizi siku tatu nimezifuatilia kwa undani sana! Mungu ataibariki tu nchi yetu pamoja na uhuni wote inaofanyiwa nchi yetu na wananchi wake,

Kwa kumaliza ni kwamba kuna kumfanyia kazi tajiri na kumpenda tajiri kwa moyo, ni vitu viwili tofauti na haviingiliani unless anayezi-face hizo choice ni mbu mbu mbu kama ninavyoona kwenye baaadhi ya posting yaani kupenda tu mpaka unakuwa kipofu, NO viongozi wanawaheshimu watu wanaowafanyia kazi na kuwaambia ukweli, ndio maana Kingunge amefanya na awamu zote nne, sio kwa sababu ya kupenda tuuuu, ni kwa sababu huwa anwapa ukweli wenye nguvu!

Karibu kwenye forum Mzee wa Shughuli unajua jinsi ninavyokuheshimu bro, samahani kwa kuomba hii thread ifungwe ingawaje inaonekana hilo ombi limepunguza NONESENSE, na wengine tuwavumilie tu maana unajua ugeni na forum nao unaweza ukamletea binadanu kiwewe!
 
Bwana tafiti
Leo nimejikuta naanza kusoma mambo yako nikacheka sana juu ya RO kuwa mwisho wa Matatizo kwa ajili ya bongo yake na alivyo pasua mashuleni huko. Sasa ukasema kwa ukali ule bado atakuwa mkali na kazi . Nimeona Mzee Es nakuuliza juu ya M16 na Marehemu Kombe sijaona majibu yako na yeye alikuwa pale London.

Mimi nimeandika hapa baada ya kujiuliza na kuona hali halisi .Kuna mtu kasema jamaa atachapa kazi kwa kuwa ni Muislam Mwadilifu na mikristo ni mijizi .Lakini nasema wako Wakristo wasomi na waliapasua sana na shule zao ni kubwa tu lakini ndiyo wametufikisha hapa tulipo leo .

wakristo hawa na waislam kwa pamoja wameifanya Tanzania kuwa masikini .Wameshiriki mikataba michafu na usomi wao na kupasua sana mashule .Je huyu RO anaweza kweli mwadilifu hadi aweze kuwaambia CCM msiibe kura maana vijana wa polisi na Usalama ndiyo hutumiwa ? kaswali haka tu baadaye mengine yatakuja . Kumbuka nimekuuliza kutokana sifa za kisomo cha Mzee RO.
 
Jamaa yangu flani ambaye siku flani nilibahatika kuona ID card yake (na ndio ikawa mwanzo wa kujua kuwa ni mtu wa Idara ya Usalama kabla ya mwenyewe kukiri baada ya muda mrefu wa kumchimba) alininong'oneza hivi majuzi kuwa kwenye Idara hiyo kuna mixed reactions kuhusu uteuzi wa RO.

Kwa mujibu wa maelezo yake,inaweza kuwa vigumu kujua utendaji kazi wa mtu akiwa kwenye kituo cha nje ila alisema kwamba katika muda ambao RO alikuwa Mkurugenzi wa Utawala hakukuwa na manung'uniko yanayoweza kuitwa makubwa isipokuwa watu walikuwa wanahofia background yake...mambo ya ujana wa mjini.Kuhusu kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi Mkuu wapo wanaodhani anaweza kupiga mzigo kwa nguvu kwa sababu anafahamu wazi watu hawamwamini sana kutokana na lifestyle yake.

Anaweza kujituma ili ku-waprove critics wrong.Wengine wanasema samaki yake maji,ukimtoa samaki kwenye maji ujue umemuua.

Kwa mantiki hiyo wanadhani RO atakuwa haunted with his past,na hiyo wont necessarily change him into mtu wa kujiheshimu zaidi.Niseme hivi,watu wanamwona RO kama version ya JK ndani ya Idara hiyo.

Naomba nifafanue. Wengi wa waliokuwa wana-doubt kuhusu Urais wa JK kabla hajaupata walikuwa wana-base kwenye tabia yake (au uadilifu,kwa kiswahili kizuri). Walikuwa wanafahamu JK mtu wa totoz, sasa wakawa na hofu kuwa mtu ambaye hawezi kuwa mwadilifu ktkt ndoa yake anawezaje kuwa mwadilifu kwenye uongozi wa juu kabisa wa nchi. RO is more or less the same. Inaelezwa kwamba ni mtu wa totoz, japo hakuna uthibitisho kama hilo limekuwa likiathiri utendaji wake.

Ila simple logic na experience inaweza kutueleza kuwa watu wa totoz huishia kuyumba kwa namna flani hata wakiwa wachapa kazi namna gani.Pengine ni suala la muda tu, japo katika hali tuliyonayo pengine isingekuwa busara kumchagua mtu mwenye questionable character (ktk angle ya totoz)
 
Kingwele
Salaam na heshima sana kwa mchango wako . Lakini Kingwele umekuja kuturudisha nyuma. What is Mahiga hapa ? Ni nani kule Tanzania huyu Mahiga . Mana kila mara Mahiga Mahiga .Nasema hakuna Mahiga hapa .Mwenye mada hii Mzeeshughuli Bwana sijaona kama kaandika lolote kuhusu Mahiga . Again naona kama una kitu unataka kukilazimisha. I will not dwell in that ila nadhani mada si Mahiga still in RO . Huyu Es unaye lia naye ni mtu kama wewe alileta mawazo yake na mambo anao yajua akayatetea sisi hapa ni kusoma na kuchambua na kuchukua mwelekeo huna haja ya kupigia mistari juu ya Mzee RO . tafiti nimemmshuku baada ya kueleza mambo hapa lakini akaja kutupotosha kwenye mada ya balozi .Es kama kaanza kuona mwelekeo mimi naungana na wachache kusema nina wasi wasi mno na data za tafiti baada ya kuja na uzushi juu ua hali a Ubalozi Uholanzi

Again matusi si mahala pake ila pia uongo ili kulinda maslahi ya bwana mkubwa we cannot be fooled bwana.Magazeti ya TZ kimyaaaaaaa hakuna mtu mmoja anahoji utendaji wa Serikali sasa tuko hapa kutunyamazisha ni ngumu na tutawatafuta kila kona kama alivyosema Mzee Es. Mjadala ni Mzee RO na si Mahiga .
 
Yes, jukwaa limekuwa safi zaidi lately. Thumbs up wahusika. Let's keep it that way. Pengine viongozi wetu wakaamua kupita humu mara kwa mara ... you never know, yaweza fikia wabunge wa kawaida wakija kuchukua pointi humu za kuulizia maswali magumu kwa mawaziri husika. Won't that be something?

Kuhusu vipande vya CV vilivyoletwa na tafiti, badhi yake nimeviskia kwa watu wengine wamjuao RO..especially shule alizosoma. Binafsi nlikuwa nikifahamu kuwa amepita Ilboru (and yes it has been among the 'special schools'... like Mzumbe na nyinginezo.. though I am not sure it was already special during his time), mlimani na masters at Sheffield. Na pia nlikuwa nafahamu alikuwa stationed Zanzibar kwa zaidi ya miaka kumi, bila kujua kuwa alikuwa ndio Govt Vetting officer. My point is, the pieces brought by tafiti still viko inline na nlivyovipata mimi... only that amekuja na details zaidi kuhusu passes zake na responsibilities za kazi. Sishangai sana kuwa kuna wanaovikataa vipande hivyo maana hili nlilitarajia na nlishasema kuwa wenye misimamo yao watapinga hata bila kufanya alternative check. Badala ya kuvitilia mashaka au kuvikataa vyoote eti kwa kuwa tafiti amekosea baadhi ya facts katika topic nyingine (ambayo hata mimi sikukubaliana nae ktk topic hiyo) naona si fair.. itakuwa vizuri mtu mwingine nae akatafute kivyake halafu akikuta ni uongo mtupu ndio aje na data tofauti. Nimenotice kuwa miaka mingine ya masomo tafiti ameifanyia 'derivation', kwa hiyo kama mtu kapania hasa ... go look 'around those years'.. as anaweza kuwa amekosea zisiwe exact ones.

Kimsingi RO, kama binadamu mwingine hawezi kuwa 100% perfect, na mixed reactions ofisini mtu mmoja anapopandishwa cheo ni kawaida, binafsi siko hapa kumtetea tu kishabiki. Ilikuwa inakera kusoma stuff kuwa kapewa cheo kwa kuwa tu kazi yake kubwa pale London ilikuwa ni kumtafutia mabibi mzee! Pia siwezi kukaa kimya mtu anapodai jamaa karukishwa vyeo from 'agenti wa kawaida' kufikia ukurugenzi katika kipindi cha 'miezi kumi tu' wakati najua ni uongo.

Suala la Kombe na MI6 sina comments, as kwa bahati mbaya lilinipita pembeni ndio naliona humu. Assuming.. and just assuming.. kuwa hili lilikuwa katika 'domain' ya RO na likampita, je tunajua ni mangapi yaliyo makubwa zaidi kwa usalama wa nchi aliyoyahandle vizuri sana? Kufanya juhudi ya kutafuta udhaifu tuuuu ni dalili ya prejudice.

Masuala ya totoz, kama ni ya kweli, I consider it his personal and private life unless mtu aje na proof kuwa huwa inaathiri utendaji wake wa kazi.

Nawaheshimu zaidi walio na ujasiri wa kuweka wazi kuwa approval rate yao imepanda baada ya kupewa data mbadala, hata kama bado ni low.. of course haiwezi kuvuka 50% overnight. Ni hatua nzuri ..na ni dalili ya kuwa na open mind.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom