Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,580
- 23,915
- Mkulu Masanja, salute ndugu yangu unajua sisi tulisema toka mwanzo kwamba wa-Tanzania tumepotea step sana na hii awamu ya nne, tukatukanwa wee, tukaitwa majina yote machafu huko duniani,
- Ninakumbuka jinsi karibu forum nzima ya BCS ikimshangilia Muungwana kwamba taifa letu linahitaji kijana kama yeye, ninashukuru kwamba wananchi sasa wanaweza kuyasoma tuliyosema then na kujumlisha kwa nini tupo hapa tulipo, ukweli ni kwamba tuliyataka wenyewe!
Respect.
FMes!
Hapa umenena Mkuu. Mimi nilisema kutoka mapema kuwa hapa tumetoka zero, lo nilivyoshambuliwa na mashabiki - karibu marafiki zangu wote wanikimbie. Tatizo la watanzania ni kuwa tunamtafuta mtu kwanza halafu ndio tunamtafutia sifa na kama hana tunajipongeza kwa kuadai tumempata mtu wa watu - eti asiye na makuu. Mara chache tunachukua muda kujiuliza huyo mtu kafanya nini huko nyuma kiasi cha kukabidhiwa uongozi, tena wa juu kabisa.
Iliitokea kwa Mwinyi na sifa moja iliyotumika kumwuza kwa wananchi ni kuwa aliwahi kuwajibika kwa makosa yaliyofanyika under his watch - jamani ! Ikatokea tena kwa Mkapa na sifa pekee iliyotajwa haikuwa kwa aliyoweza kutenda bali kashfa inayomhusu kutojulikana - eti mr. clean ! Kama vile hatuna akili tumeweza kwa mara ya tatu kuruhusu hali hiyo kwa Kikwete ambaye eti tabasamu lake tu liliweza kuwachengua wapiga kura hadi kumpa ushindi wa wa tsunami - my, God !
Ajabu inatusubiri mwaka 2010 ambapo tunatakiwa kumrudisha madarakani kwa kushindwa kutekeleza aliyoyaahidi hivyo aongezewe muda. Na wako watu na akili zao timamu watasimama majukwaani na kumnadi hivyo hivyo kwamba pamoja na kushindwa hapo mwanzo bado anafaa. Nimeshukuru sana kwa aliyeweza kuirudisha hii thread, naona wenzangu mlianzia mbali - wengine tulikuwa tunaugulia tu kimya kimya kumbe hawavumi lakini wapo.
Mficha ficha maradhi, kilio humuumbua.