Kwa wale wenye macho makali na upembuzi wa picha za TV na za mnato mtakuwa mmetupia macho maeneo maarufu mawili hapa nchini. La kwanza ni kwenye njia za ndani ya ukumbi wa Bunge toka milangoni kuja mpaka kwenye eneo la Spika. Hapa kuna zulia ambalo limetengenezwa makusudi kufuata rangi za bendera ya Tanzania kwenye fito zake.
Sehemu ya pili ni uwanja wa ndege wa JNIA (Dsm) wakati ambapo anakuja kiongozi wa nje kwenye ziara ya kitaifa. Hapo huwa linatandazwa zulia jekundu lenye fito za rangi za bendera ya taifa pembeni pia.
Ninavyoamini na kufahamu ni kwamba bendera ndiyo kitambulisho kikuu cha nchi yoyote duniani na kwa utaratibu wa kistaarabu haipaswi kugusa ardhi "deliberately, accidentally or permanently". Ndiyo maana hata wakati inashushwa huwa askari anayeishusha anahakikisha haivuki hata usawa wa magoti yake kuelekea ardhini.
Je, ni busara gani kama si dharau kuruhusu watu bila kujali wadhifa gani wanao kuikanyaga bendera ambayo ndiyo sura ya taifa aidha wanapoteremka kwenye ndege au wanapoingia na kutoka Bungeni?