Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametoa wito kwa nchi za Ulaya na Marekani zilizoweka vikwazo vya usafiri kwa Mataifa ya Kusini mwa Afrika yaliyobainika kuwa na maambukizi ya aina mpya ya Virusi vya Corona kuondoa vikwazo hivyo.
Katika hotuba yenye urefu wa dakika 29, Rais Ramaphosa amesema kugundulika kwa aina ya kirusi cha Omicron kunatokana na ufanisi na juhudi za Wataalamu wa Afya nchini Afrika Kusini.
“Marufuku ya Usafiri kwa Mataifa ya Kusini mwa Afrika iliyowekwa haina uhalali wowote na inaongeza ubaguzi kwetu na kwa nchi za Kusini mwa Afrika na haisaidii kuzuia madhara ya maambukizi ya virusi bali inaongeza maumivu ya kiuchumi katika nchi zetu.
“Natoa wito kwa mataifa hayo kuondoa marufuku ya kusafiri haraka kabla madhara ya kiuchumi kwa nchi zetu na madhara kwa maisha ya wananchi hayajatokea zaidi. Hakuna sababu zozote za kimsingi za Kisayansi za kuweka marufuku hiyo.
“Tunafahamu kuwa virusi hivi, kama aina nyingine ya virusi vya corona, hubadilika na uwezekano wa kutokea kwa aina nyingine yenye nguvu zaidi ya virusi hivi ni mkubwa,” alisema Rais Ramaphosa.
Rais Ramaphosa amesisitiza pia kuwepo usawa wa chanjo kwa nchi zinazoendelea, akisema madhara ya virusi vya corona yanaweza kupunguzwa ikiwa wananchi wengi wa nchi zinazoendelea watapata chanjo.
Kirusi cha corona cha B.1.1529 kilichopewa jina Omicron kilitambuliwa nchini Afrika Kusini Novemba 26, na tayari kimekwisha sambaa katika nchi kadhaa za Ulaya, Australia na Asia.