Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Moja kati ya hatua ambazo zinahitaji umakini katika ujenzi ni pamoja na hatua ya kujenga kozi za mwisho (kozi za juu ya mkanda)

Kama kozi ya mwisho haitokuwa level moja, italeta shida pia katika hatua ya kupaua ambapo fundi kupaua atalazimika kujaza vibao ili kupata level moja kwahivyo ni muhimu sana katika hii hatua ikatumika pipe level ili kuepuka kazi za ziada ambazo zinaweza kukwepeka

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kuna baadhi ya tiles huwezi kuzitumia bila kuziloweka kwenye maji na kuna tiles zingine unaweza ukazitumia bila kuziloweka.

Kabla ya kuanza hiyo kazi, ni vyema ukajua tiles zako ni za aina gani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane. Bado offer ya punguzo la bei inaendelea mpaka mwisho wa mwezi huu. Miezi ya kujenga ndio hii
 
Kama una makazi sehemu ambayo ujenzi ndio unaanza anza mfano maeneo kama Vikindu na maeneo mengine, tafuta mbao zako kadhaa uwe unakodisha. Uhitaji ni mkubwa sana, vitu vingine ambavyo unaweza ukawakodishia watu ni kama vile mapipa ya maji (yale ya ndoo 12), machepe, ngazi, mpira wa maji, toroli nk

Huko ujenzi ni kila siku, huyu akipumzika kujenga mwingine ndio anaanza kwahiyo wateja utawakimbia mwenyewe. Utapata wateja wengi kwa sababu sehemu kama hizi hardware ziko mbali kwahivyo mteja option yake ya kwanza itakuwa ni kwako

Mkuu hivi nyumba ambayo sio ghorofa ni lazima kupanga mawe ndio umwage jamvi?

Au baada ya kifusi na kushindilia unaweza mwaga jamvi moja kwa moja bila kuweka mawe?
 
Mizizi ya miti inapokua huwa inatekenya msingi, ndio maana haishauriwi miti kuwa karibu na nyumba kama hivi. Sababu za hili tatizo zinaweza kuwa nyingi, lakini hii ya mizizi pia ni moja wapo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasilianeView attachment 3607596
Mkuu niache mita ngapi toka kwenye fensi ndio uuanze ukuta wa nyumba?

Na je master bedroom inapendeza kuwa uelekeo gani kwa maana ya kaskazini kusini mashariki au magharibi?
 
Plaster nzuri ni ile ambayo ukimwagia ukuta maji, ukuta unakauka bila kuchora alama za matofali. Kiujumla michoro ya tofali katika ukuta uliopigwa plaster hutokea pale ratio ya udongo uliotumika kujengea tofali ni kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kupigia plaster

Kitaalam udongo wa kujengea tofali tunatumia ratio ya 1:6 na udongo wa kupigia plaster tunatumia ratio ya 1:4 na 1:5 (ratio ya 1:4 inatumika kwenye kuta upande wa nje, na 1:5 upande wa ndani)

Ratio ya plaster inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kujengea

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Hiyo 1:6 ndio inakuwaje mkuu? Mfuko mmja wa cement kwa ndoo ngapi kubwaza mchanga?
 
Baada ya kupanga mawe (hardcore) katika msingi, inashauriwa umwage mchanga mwingi ndipo uje umwage zege la jamvi (oversite concrete). Hii ni kwa sababu unapopanga mawe, ile nafasi iliyopo kati ya jiwe na jiwe zege inaweza isipite kwenda kuziba hizo nafasi. Kama hiyo sakafu itapata mgandamzo mkubwa (mfano gari ikapita) inaweza kusababisha hiyo sakafu kutitia kutokana na uwepo wa uwazi (matundu) uliopo chini yake

Kama unahitaji ramani za kitaalamu na makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Yaani ata ki apartment cha chumba self na sebule acho msingi nipange mawe?
 
Mkuu hivi nyumba ambayo sio ghorofa ni lazima kupanga mawe ndio umwage jamvi?

Au baada ya kifusi na kushindilia unaweza mwaga jamvi moja kwa moja bila kuweka mawe?
Kuweka mawe ni muhimu ila sio lazima, unachotakiwa ni kuhakikisha kifusi chako kinashindiliwa kwa matabaka. Usijaze kifusi chote halafu uje ushindilie mwishoni baada ya kumaliza kujaza.
Jaza kiasi shindilia, jaza tena shindilia mpaka unamaliza kufukia pote.
 
Mkuu niache mita ngapi toka kwenye fensi ndio uuanze ukuta wa nyumba?

Na je master bedroom inapendeza kuwa uelekeo gani kwa maana ya kaskazini kusini mashariki au magharibi?
Kulia na kushoto mwa nyumba inatakiwa isipungue mita 1.5

Mbele na nyuma inategemea na site plan ya kiwanja chako, muhimu karo la choo liwe umbali usiopungua mita 3 kutoka nyumba/fence inapoanzia (nyuma ni kama mita 8 hivi inatosha yani 3m+2m+3m)

Upande wa mbele itakuwa ni sawa na urefu/upana wa kiwanja kutoka mbele kwenda nyuma kutoa mita 8 kutoa urefu wa nyumba mfano (30m - 8m - 12m =10m)
 
Bro mbona ndio umenichanganya sasa...ujue mie back bencher mathematics nilidaka are we together pekee na integration by parts
 
Unapofanya wiring weka
1.5mm Taa na Feni
2.5mm Socket TV, Vingamuzi
4mm AC, Pasi Oven na vitu venye Watts 1000 na zaidi
6mm AC BTU 30000, Oven watts 3000

Pia hakikisha kwenye Main Switch MCB zimewekwa wire kutokana na “load” Ampire inayosupply
Kwasada sokoni waya ziko nyingi zenye material ya copper kwa chini ya asilimia 70% sana sana “imported” wire tuwe makini
Naomba ushauri kuhusu 6 way distribution board brand ya HPL, single phase ubora wake ukilinganisha na havells au tronics
 
Kama una makazi sehemu ambayo ujenzi ndio unaanza anza mfano maeneo kama Vikindu na maeneo mengine, tafuta mbao zako kadhaa uwe unakodisha. Uhitaji ni mkubwa sana, vitu vingine ambavyo unaweza ukawakodishia watu ni kama vile mapipa ya maji (yale ya ndoo 12), machepe, ngazi, mpira wa maji, toroli nk

Huko ujenzi ni kila siku, huyu akipumzika kujenga mwingine ndio anaanza kwahiyo wateja utawakimbia mwenyewe. Utapata wateja wengi kwa sababu sehemu kama hizi hardware ziko mbali kwahivyo mteja option yake ya kwanza itakuwa ni kwako

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Naomba ushauri kuhusu 6 way distribution board brand ya HPL, single phase ubora wake ukilinganisha na havells au tronics
 
Mita 45 kwa 19
Nyumba m8 x 8
Hapo ni sawa na viwanja viwili vya mita 19 kwa 25, na mita 19 kwa 20

Ili usiharibu eneo lako, nyumba usiiweke kati kati ya kiwanja. Chagua eneo moja wapo kati ya hilo la 19x25 au la 19x20 ili eneo lingine ufanyie mambo mengine (kama kujenga nyumba za kupangisha, kufugia n.k)

Mbali na hivyo, pia hutakiwi kuiweka kati kati katika hicho kiwanja utakachochagua kwa kuwa nafasi itakayobaki kushoto/kulia na nyuma/mbele utakuwa umeigawa mara mbili.

Mfano katika mita 19, ukitoa mita 8 ya nyumba inabaki mita 11 kwahivyo unaweza ukaacha nafasi ndogo ya njia ubavu mmoja ili ubaki na nafasi kubwa ubavu mwingine. Unaweza ukaacha mita 2 ubavu mmoja, ukabaki na mita 9 ubavu mwingine ambapo utaweza tena kuweka jengo lingine kama vile jiko la nje, mnara wa tank la maji/store n.k

Ukija upande wa mbele/nyuma, ukichukua mita 25 ukatoa mita 8 ya nyumba unabaki na mita 17 ambapo unaweza ukaacha mita 10 mbele kwa ajili ya parking na nyuma ukaacha mita 7 kwa ajili ya nafasi ya makaro ya choo. Kumbuka karo la choo linatakiwa liwe mbali kidogo na nyumba na pia liwe mbali na ukuta wa fence. Usije ukaacha mita 1 kati ya karo na nyumba, mana karo likishuka kidogo tu nyumba nayo itapata lift kutokana na kutikisika kwa msingi [emoji846]
 
Asante mkuu...hapa umenielimisha kabisa. Mie nimeweka jiyo nyumba kona kabisa mwisho wa kiwanja na nimeacha 1.5m kutoka fence ya nyuma na 1.5m kutoka fence ya upande wa kulia. Huku kwengine nimeacha eneo kwa ajili ya karo na water tower.

Fundi kaniambia kuwa karo tujenge mita 2 toka fence ya ubavuni lakini pia atasuka nondo kiasi cha kwamba niweze kupark gari juu yake. Hili lina ukweli na je nondo zinazotumika kuauka mfuniko wa karo zikiwa 16mm itawezekana?
 
Back
Top Bottom