Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Katika ufungaji wa gympsum board, hakikisha spacing kati ya screw moja na screw nyingine haizidi sentimita 20 ambapo kwa hesabu hiyo kila board moja inatakiwa ifungwe screws 55

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane.

Wale wa mikoani pia ramani zitawafikia bila shida yoyote, tuwasiliane ujipatie ramani yako uanze ujenzi mapema kabla mvua za maembe hazijaanza
 
Mizizi ya miti inapokua huwa inatekenya msingi, ndio maana haishauriwi miti kuwa karibu na nyumba kama hivi. Sababu za hili tatizo zinaweza kuwa nyingi, lakini hii ya mizizi pia ni moja wapo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
20260614_145613.jpg
 
In
Msaada wa makadirio ya Mbao kwa ajili ya brandering...ukubwa wa nyumba 9*10=90sq mtrs...nikitumia 2*2 kwa sababu ya gharama ni sawa..zinaweza hitajika ngapi..
Hapo kuwa makini sana maana sisi mafundi umeme uwa tunajionea vingi sana kwenye izo mbao za juu.
 
Msaada wa makadirio ya Mbao kwa ajili ya brandering...ukubwa wa nyumba 9*10=90sq mtrs...nikitumia 2*2 kwa sababu ya gharama ni sawa..zinaweza hitajika ngapi..
Ili kupata makadirio ya mbao kwa usahihi inatakiwa iwepo floor plan ili kuona mgawanyo wa vyumba jinsi ulivyo vinginevyo itakuwa ni kama nimekadiria mbao za kufanya brandering ya ukumbi (hakuna partition kati kati)

Tuwasiliane nikufanyie makadirio ya material yote ya brandering, ikiwemo gympsum boards, mikanda, screws za kufungia board, fibre tape n.k
 
Shukrani mkuu nilishapata makadirio yenye uhalisia, mwanzoni hatukuelewana na fundi nikidhani idadi ni mara mbili ya nilichotemegea,kumbe alinipa options 2..
 
Wakati unamwaga kifusi katika msingi, tabaka la mwisho jitahidi liwe flat ili baadae utakapoweka rough floor usitumie idadi kubwa ya material ambayo ungeweza kuiepuka.

Kama level ya kifusi itakuwa ina slope, maana yake wakati wa kuweka rough floor sehemu zote zenye mabonde zitajazwa na udongo wa mortar au zege ambapo kama level ya kifusi ingekuwa flat ingepunguza idadi ya material ya rough floor

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika upigaji plaster wa kuta, ni afadhali ukaweka plaster nyembamba yenye ratio kali kuliko ukaweka plaster nene yenye ratio dhaifu kwa maana haitochukua muda itaanza kuachana na kuta. Uimara wa plaster unaanza na ratio, kisha unene ndio unafuata

Ratio ya plaster kwa kuta za ndani ni tofauti na Ratio ya plaster kwa kuta za nje

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasliane. Ushauri ni BURE kabisa
 
Ratio Kali(standard plastering) ikoje ndugu?
 
Ratio Kali(standard plastering) ikoje ndugu?
Kuta za ndani 1:5, kuta za nje 1:4
Hiyo ni kwa mchanga ambao ni mzuri katuka matumizi ya plaster, vinginevyo utalazimika kuongeza cement zaidi ili kupata mortar nzuri itayofaa kwa matumizi ya plaster
 
Kuta za ndani 1:5, kuta za nje 1:4
Hiyo ni kwa mchanga ambao ni mzuri katuka matumizi ya plaster, vinginevyo utalazimika kuongeza cement zaidi ili kupata mortar nzuri itayofaa kwa matumizi ya plaster
Kuna fundi ananiambia ndoo za 10ltrs 50 kwa mifuko 3 ya cement
 
🤣🤣🤣 huyo anataka mwaka ukimalizika umuite tena umpe kazi kwa mara ya pili ya plaster
Hivi unajua ratio ya 1:5 ni sawa na ndoo ndogo 20 kwa mfuko, ambapo ni ndoo 60 kwa mifuko 3 ya cement. So unaona hapo ratio ya huyu fundi ipo ni kama 1:42
 
Hivi unajua ratio ya 1:5 ni sawa na ndoo ndogo 20 kwa mfuko, ambapo ni ndoo 60 kwa mifuko 3 ya cement. So unaona hapo ratio ya huyu fundi ipo ni kama 1:42
Kwa mifuko mitatu ni sahihi kabida.nilijua mfuko mmoja
 
Unapofanya wiring weka
1.5mm Taa na Feni
2.5mm Socket TV, Vingamuzi
4mm AC, Pasi Oven na vitu venye Watts 1000 na zaidi
6mm AC BTU 30000, Oven watts 3000

Pia hakikisha kwenye Main Switch MCB zimewekwa wire kutokana na “load” Ampire inayosupply
Kwasada sokoni waya ziko nyingi zenye material ya copper kwa chini ya asilimia 70% sana sana “imported” wire tuwe makini
 
Hivi unajua ratio ya 1:5 ni sawa na ndoo ndogo 20 kwa mfuko, ambapo ni ndoo 60 kwa mifuko 3 ya cement. So unaona hapo ratio ya huyu fundi ipo ni kama 1:42
Kwa mifuko mitatu ni sahihi kabida.nilijua mfuko mmoja
Habari Viongozi,
Naomba Msaada wa Gharama ya Vifaa Kupiga Plasta na Gharama ya Ufundi kwa Kazi ya Kupiga Plasta, Kwa kuzingatia Mchoro hapa Chini
Ushaweka mfumo wa umeme na maji?
 
Habari Viongozi,
Naomba Msaada wa Gharama ya Vifaa Kupiga Plasta na Gharama ya Ufundi kwa Kazi ya Kupiga Plasta, Kwa kuzingatia Mchoro hapa Chini
Huwa nawaambia kila siku, ukinunua ramani kwa mtu hakikisha unambana huyo huyo aliyekuchorea ili usiingie tena gharama mara mbili. Sidhani kama mtu atakuchorea ramani, halafu ukamuuliza kitu akakuchaji tena gharama zingine.

Hizi kazi za mahesabu, ni nadra kukuta mtu anajitolea kukufanyia hesabu bila malipo. Lazima kuwe na kazi iliyotangulia (mfano ramani) au mtu anapata maslahi katika hiyo kazi husika.
 
Wakati wa kupiga ripu kuta zako, sehemu ya kuta za msingi inayotokeza juu ya ardhi ni vizuri zaidi kama utaweka wire mesh kabla ya kupiga plaster.

Hii ni kwa sababu sehemu hii mara nyingi hukutana na unyevu unyevu, hata mvua inaponyesha sehemu hii utakuta imeloa kutokana na maji yanayodunda baada ya kutua ardhini.

Wire mesh itasaidia plaster yako kushika vizuri katika kuta ikisaidiwa na ratio nzuri ya plaster.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Back
Top Bottom