Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Hapo ni sawa na viwanja viwili vya mita 19 kwa 25, na mita 19 kwa 20

Ili usiharibu eneo lako, nyumba usiiweke kati kati ya kiwanja. Chagua eneo moja wapo kati ya hilo la 19x25 au la 19x20 ili eneo lingine ufanyie mambo mengine (kama kujenga nyumba za kupangisha, kufugia n.k)

Mbali na hivyo, pia hutakiwi kuiweka kati kati katika hicho kiwanja utakachochagua kwa kuwa nafasi itakayobaki kushoto/kulia na nyuma/mbele utakuwa umeigawa mara mbili.

Mfano katika mita 19, ukitoa mita 8 ya nyumba inabaki mita 11 kwahivyo unaweza ukaacha nafasi ndogo ya njia ubavu mmoja ili ubaki na nafasi kubwa ubavu mwingine. Unaweza ukaacha mita 2 ubavu mmoja, ukabaki na mita 9 ubavu mwingine ambapo utaweza tena kuweka jengo lingine kama vile jiko la nje, mnara wa tank la maji/store n.k

Ukija upande wa mbele/nyuma, ukichukua mita 25 ukatoa mita 8 ya nyumba unabaki na mita 17 ambapo unaweza ukaacha mita 10 mbele kwa ajili ya parking na nyuma ukaacha mita 7 kwa ajili ya nafasi ya makaro ya choo. Kumbuka karo la choo linatakiwa liwe mbali kidogo na nyumba na pia liwe mbali na ukuta wa fence. Usije ukaacha mita 1 kati ya karo na nyumba, mana karo likishuka kidogo tu nyumba nayo itapata lift kutokana na kutikisika kwa msingi [emoji846]
Mkuu hiyo mita 10 ya parking ina include parking na drive way yaani njia ya kutokea kuelekea sasa kwenye geti?
 
Mkuu hiyo mita 10 ya parking ina include parking na drive way yaani njia ya kutokea kuelekea sasa kwenye geti?
Hapana, hiyo maana geti lako unaliweka sehemu ambayo gari itakuwa inaenda moja kwa moja eneo la kupark bìla kukata kona, vinginevyo itabidi uache nafasi kubwa zaidi
 
Hapana, hiyo maana geti lako unaliweka sehemu ambayo gari itakuwa inaenda moja kwa moja eneo la kupark bìla kukata kona, vinginevyo itabidi uache nafasi kubwa zaidi
Mkuu fundi michael ananiambia hapa kwamba perimeter naweza jenga na gofali inch sita alafu partition ya vyumba na mabafu na vyoo ikawa inch 5. Hii inawezekana kweli? Hakutakuwa na tabu pale kuta ya inch 5 inapaswa kuungana na perimeter wall ya inch 6?
 
Ni sahihi na inawezekana, nchi 5 na nchi 6 ni unene wa tofali (urefu na upana kwa tofali zote ni sawa) kwa hivyo hakuna shida yoyote katika makutano ya hizo kuta. Alichokushauri fundi nilishawahi kukiandika humu siku za nyuma, ukitumia tofali za nchi 6 katika kuta za nje utaweza kutumia dirisha za aluminium zenye profile ya upana wa zaidi ya nchi 3 lakini pia kwenye milango ya nje utaweza kuweka mlango wako wa mbao na geti kwa uhuru zaidi. Tofali za nchi 6 ukija kupiga plaster kuta zako ndani na nje, utakuwa na ukuta wenye unene wa nchi 7.
 
Asante mkuu...hapa umenielimisha kabisa. Mie nimeweka jiyo nyumba kona kabisa mwisho wa kiwanja na nimeacha 1.5m kutoka fence ya nyuma na 1.5m kutoka fence ya upande wa kulia. Huku kwengine nimeacha eneo kwa ajili ya karo na water tower.

Fundi kaniambia kuwa karo tujenge mita 2 toka fence ya ubavuni lakini pia atasuka nondo kiasi cha kwamba niweze kupark gari juu yake. Hili lina ukweli na je nondo zinazotumika kuauka mfuniko wa karo zikiwa 16mm itawezekana?
Pia inawezekana ila tu kuna vitu vya kuzingatia ikiwemo aina ya udongo, ubora wa tofali zitakazotumika kujengea karo, unene na ratio ya zege la slab, spacing kati ya nondo na nondo lakini pia ni vyema ukafunga mkanda ili nondo za slab zipate sehemu ya kuzifungia kuliko kulala juu ya kuta moja kwa moja

Nondo za slab zikifungwa kwenye mkanda kuzuia slab isibinuke juu (kàtika maungio ya slab na kuta) pindi slab inapokandamizwa kati kati ndio maana ukichunguza makaro mengi utaona kuna ufa unaonekana katika maungio ya tofali na slab ya karo. Kadri mzigo juu ya slab unavyoongezeka ndipo slab inavyozidi kuachana na kuta na deflection kati kati kuongezeka zaidi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Sii mchezo elimu murwa kabisa...sasa mknda unakuwa na unene wa 23cm maana sii tofali zimelala?
 
Ni sahihi na inawezekana, nchi 5 na nchi 6 ni unene wa tofali (urefu na upana kwa tofali zote ni sawa) kwa hivyo hakuna shida yoyote katika makutano ya hizo kuta. Alichokushauri fundi nilishawahi kukiandika humu siku za nyuma, ukitumia tofali za nchi 6 katika kuta za nje utaweza kutumia dirisha za aluminium zenye profile ya upana wa zaidi ya nchi 3 lakini pia kwenye milango ya nje utaweza kuweka mlango wako wa mbao na geti kwa uhuru zaidi. Tofali za nchi 6 ukija kupiga plaster kuta zako ndani na nje, utakuwa na ukuta wenye unene wa nchi 7.
Asante mkee kwa elimu. Usinichoke maana hapa nipo kupate elimu fundi michael asije niingiza chaka mwanawane.

Haya kujenga kitaalam unatakiwa ujenge kozi ngapi maximu kwa siku?

Pili, distance kati ya dirisha na mlango minimum ni cm ngapi? Na pia distance toka kwenye kona ambayo kuta mbili zinakutana mpaka mwanzo wa dirisha kwa kila upande distance inapendeza ikiwa cm ngapi?
 
Naomba msaada wa namna ya kubargain bei ya ujenzi wa msingi n vigezo gani vya kutumia ili kuendana na value for money?
-Nyuma n sqm 218.
-Ur mita 15 upana mita 20
- vyumba vitatu self, master, jiko na sebule kubwa, veranda tatu
 
Sii mchezo elimu murwa kabisa...sasa mknda unakuwa na unene wa 23cm maana sii tofali zimelala?
Yah, upana utakuwa ni 23cm. Kina cha mkanda kinatakiwa kizidi upana kwahivyo unaweza ukaweka kina cha 30cm inatosha. Nikisema kina namaanisha depth ya beam
 
Naomba msaada wa namna ya kubargain bei ya ujenzi wa msingi n vigezo gani vya kutumia ili kuendana na value for money?
-Nyuma n sqm 218.
-Ur mita 15 upana mita 20
- vyumba vitatu self, master, jiko na sebule kubwa, veranda tatu
Aisee sii mchezo bonge la bangalow...humo nda i sii mnacheza ata rondo mwanawane. Mie naomba kazi hapo kama msimamizi wa ujenzi
 
Kabla ya kuanza kupandisha tofali za boma, ni vizuri ukatandika nailoni maalum (Damp proof course ,DPC) juu ya tofali za msingi(au mkanda kama umeweka) ambapo itasaidia kuzuia unyevu nyevu usiweze kupanda juu na kuathiri kuta za boma.
Ewaaah mkuu hii DPC gharama yake ikoje na je wanauza la running metre au sqm?
Na unaweka udongo juu ya mkanda ndio dpc au unailaza tuu dpc juu ya mkanda pasipo mortar?
 
Kwenye nguzo za vibaraza sio lazima uweke nguzo za zege, unaweza ukaweka nguzo ya shape ya "L" kwa kutumia tofali na bado nyumba yako ikavutia lakini pia ikakupunguzia gharama za nondo na ufundi
Hizi tofali zina simama au ndio zina lala?
 
Kabla hujaanza ujenzi, ni vizuri ukajua upande ambao jua huwa linachomoza (mashariki)...Mada ni ndefu, kwa leo nitaelezea upande ambao jiko (kitchen room) linatakiwa likae

Jiko linatakiwa likae upande wa Kusini Mashariki ambapo mida ya asubuhi jua linakuwa ni la wastani (jua la vitamin D, hapa mpishi atapata muda wa kuandaa breakfast akiwa comfortable kabisa), baada ya hapo jua litakuwa linaendelea kuhama taratibu ambapo mpaka kufikia mida ya saa tano tano kuelekea saa sita, jua litakuwa lipo juu ya nyumba linapiga bati kwa juu (hapa pia mpishi atakuwa katika mazingira rafiki kuandaa chakula cha mchana bila kusumbuliwa na joto la jua)

Ramani, Makadirio, Ushauri tuwasiliane
Mkuu sometimes unakuta muelekeo wa barabara unalazimu kitchen ikae mashariki....sii u ajua tena lazima uangalie geti lako.
Mfano katika kiwanja geti na barabara kuu ipo magharibi na pande zote 3 kuna nyumba za majirani na pia mashariki ndio nyuma ya kiwanja. hapo muelekeo sii inakuwa changamoto.
 
Ni vizuri ukasubiri kwanza kuta zote za msingi zikauke vizuri ndipo ujaze kifusi na kukishindilia, ukijaza kifusi kabla ukuta haujakauka vizuri itasababisha ile pressure ya udongo inayosukuma ukuta kutengeneza nyufa hasa upande wa chini ambao huwa unachelewa kukauka. Ukuta ukiwa umekauka vizuri, na pressure ya udongo ikawa kubwa, nyufa zinakimbilia sehemu ambapo fundi aliweka udongo (mortar) mnene zaidi
Mkuu vipi kifusi cha mchanga kinafaa?
 
Tofali unazilaza
Sasa mkuu sii zitapishana ureku kaenda juu na hizi zingine zinazokuwa zimesimamamishwa. Yaani 15cm huku za kusimama zinakuwa 23 cm. Kufika kwe ye lintel idadi za kusimama na kulaza haziwezi kuwa sawa
 
Sasa mkuu sii zitapishana ureku kaenda juu na hizi zingine zinazokuwa zimesimamamishwa. Yaani 15cm huku za kusimama zinakuwa 23 cm. Kufika kwe ye lintel idadi za kusimama na kulaza haziwezi kuwa sawa
Ndio idadi ya kozi haziwezi kuwa sawa, na sio lazima ziwe sawa kwa sababu kùta haziungani, cha msingi tu inatakiwa kuta zote juu ziwe level moja kwa hivyo utabalance unene wa udongo wakati unakaribia kufika juu (mfano kozi 5 kabla ya kufika juu). Ukushafunga mkanda wa juu, kozi za juu unasimamisha tofali pote ambapo huko ndio kuta zitaungana
 
Hiyo L inatakiwa kuwa mita ngapi kwa ngapi minimum?
 
Back
Top Bottom