Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Mkuu nisaidie hili, naweza kujenga kozi 13 baada ya mkanda wa msingi(3 chini + dirisha kozi 10) ndo nikaweka lenta? Nahitaji nyumba iwe ndefu.
Je juu ya lenta inafaa kozi 3 au 4?
 
Mkuu nisaidie hili, naweza kujenga kozi 13 baada ya mkanda wa msingi(3 chini + dirisha kozi 10) ndo nikaweka lenta? Nahitaji nyumba iwe ndefu.
Je juu ya lenta inafaa kozi 3 au 4?
Kozi 3 baada ya lenta ndo kisasa zaidi kutoka msingi hadi lenta kozi 10 iko pw sana hayo mawazo yangu wengine wachangie
 
Mkuu nisaidie hili, naweza kujenga kozi 13 baada ya mkanda wa msingi(3 chini + dirisha kozi 10) ndo nikaweka lenta? Nahitaji nyumba iwe ndefu.
Je juu ya lenta inafaa kozi 3 au 4?
Ndio inawezekana ndg ila design yako inabidi isiwe na viukuta vifupi, huwa vinasumbua katika kupigilia box za mkanda. Mara nyingi huwa vinakatika

Juu ya lental beam, kawaida huwa ni kozi 3 ila kama paa lako lina slope ya kuzidi angle 40 na unataka overhang ya bati iwe kubwa basi ukiweka kozi 4 itakuwa vyema zaidi kwa maana tofali moja na nusu mpaka mbili zitakuwa zinafishwa na overhang ya bati
 
Viukuta vifupi ndo vipi hivyo mkuu?
 
Hakikisha main switch yako inawekwa katika umbali ambao unaweza kuifikia ukiwa umesimama bila kutumia nyenzo yoyote kama vile stuli, meza n.k

Lakini pia isiwe imefungiwa katika chumba kwa maana itakapotokea shida ya kuhitaji kuizima isimlazimu mtu kuanza kutafuta funguo ya mlango, ndio maana wengi huwa wanaiweka kwenye corrido ili iwe rahisi kwa mtu yeyote kuifikia

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Tunaomba elimu juu ya kifaa kinachoitwa central stabilizer ya nyumba mzima. Je, ushawahi kufunga hiki kifaa, na ni brand ipi ni bora zaidi?.
 
Tunaomba elimu juu ya kifaa kinachoitwa central stabilizer ya nyumba mzima. Je, ushawahi kufunga hiki kifaa, na ni brand ipi ni bora zaidi?.
Central stablizer ni kifaa kinachofungwa katika mfumo wa umeme ili kuulinda huo mfumo dhidi ya kupanda ama kushuka kwa voltage.

Vifaa vyingi vya majumbani vinafanya kazi kwa voltage ya 220V mpaka 240V, sasa mfano kwenye setting, high voltage ukiweka iwe labda 240V, stablizer yako itakuwa inakata umeme pindi inapotokea umeme umezidi 240V na kujiwasha yenyewe pindi voltage inaposhuka na kufika volt 240 kwahivyo itakuwa imekulindia vifaa vyako visiweze kuungua

Pia kuna setting ya low voltage, kwa maana umeme ukishuka chini ya voltage uliyoiset, stablizer pia itakata umeme mpaka pale umeme utakapoongezeka na kufikia voltage uliyoiset ndipo itajiwasha.

Vifaa pia havitakiwi kufanya kazi katika voltage ndogo kwa maana itakuwa inanyonya current kubwa kwahivyo inasababisha waya kuungua. P=VI, kama P ni constant na voltage ikashuka basi current inabidi iwe kubwa kuliko ile ambayo ilitakiwa iwe katika hali ya kawaida (yani 240V)

Kiujumla central stablizer ni kama AVS kiutendaji, AVS inalinda baadhi ya vifaa lakini central stablizer inalinda mfumo mzima wa umeme
 
Taa za nje hata kama zinatumia switch moja, usiziunge kwa kufatana (series) kwa sababu ikiungua taa moja basi taa zote pia hazitofanya kazi hata kama zenyewe zitakuwa bado ni nzima.

Hata taa za kwenye dari pia ziunge in parallel, ili ikileta shida taa moja, zingine ziendelee kufanya kazi kama kawaida.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Siku hizi watu wengi taa za nje wanaweka taa zenye motion sensor, kwa maana taa zinakuwa zinawaka tu pale kunapotokea movement yoyote.

Kimahesabu inaweza ikawa sawa au ikapunguza matumizi ya umeme ukilinganisha na mtu aliyeweka taa ya watt 20 inayowaka kuanzia jioni mpaka asubuhi. Hizi taa zenye sensor zinakuaga na watt mbali mbali, mfano ukiweka taa ya watt 100 jumla ya dakika zote ambazo hii taa itawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi inaweza isizidi dakika 60 ambayo kimatumizi ni sawa na unit 0.1

Taa ya kawaida ya watt 20 ikiwaka kwa muda wa saa 12 (jioni mpaka asubuhi) inakuwa ni sawa na unit 0.24. Hii ni kwa taa moja tu, na bado mwanga wake unakuwa sio sawa na mwanga wa taa ya watt 100

MKUU taa za nnje uwezi ukaweka mfumo wa sensor kwa sababu zinasaidia kwa usalama na muonekano wa nyumba usiku, ukiweka taa za nnje sensor maana yake kama akijakatiza kitu basi nyumba itakuwa ipo gizani kama vile utumii umeme.
Matumizi ya sensor ni kwa ajili ya taa za barabarani na getini.pia unaweza ukaweka chooni.

Nyumba inapendezeshwa na taa.
 
Nimekupata Fundi Umeme,

Kwamba ukiweka taa zote nje ni sensor means kama hakuna mtu basi nyumba nzima inakua ni giza mpaka pale atakapopita mtu.

Lakini mleta mada anamaanisha kukiwa giza na hajakatiza mtu bado nyumba iko salama. Sasa yeye anajali zaidi usalama kuliko kupendeza na hizo taa.

Nadhan acha tu ziwake baadhi ya maeneo Sababu giza nalo sio rafiki hata kama hakuna mtu.
 
MKUU taa za nnje uwezi ukaweka mfumo wa sensor kwa sababu zinasaidia kwa usalama na muonekano wa nyumba usiku, ukiweka taa za nnje sensor maana yake kama akijakatiza kitu basi nyumba itakuwa ipo gizani kama vile utumii umeme.
Matumizi ya sensor ni kwa ajili ya taa za barabarani na getini.pia unaweza ukaweka chooni.

Nyumba inapendezeshwa na taa.
Hapo hapo kwenye usalama ndio ilikuwa dhamira yangu, na hizo taa za sensor zipo za aina tofauti. Kuna zile ambazo zinakuwa zinawaka mwanga mdogo ila ikitokea movement yoyote, mwanga unaongezeka na kuwa mkali zaidi kwa hivyo sio kwamba nyumba itakuwa kiza asilimia 100
 
Mimi nahisi wewe una maanisha taa za support(street light) na sio taa za kwenye nyumba uwa hazina sensor bali wewe unazifungia sensor kila upande mtu akitokeza sensor inamuona.
Zile street light uwa ina sensor na pia in dimmer ndani.kwa iyo sensor ikikata dimmer inapunguza mwanga kwenye taa.sensor ikimulika dimmer inaongeza mwanga kwenye taa.
 
Pia kuna swala ambalo wengi awajui.umeamua kufunga taa za urembo basi kubali kugharamika.usikubali fundi akaenda kukununulisha taa za kariakoo zile hata mwaka ngumu kumaliza.unakuta nyumba mpya hata miezi 6 aina ila taa zimeanza kuzima. Kama unaitaji taa nenda Clock tower pale unaona duka la Legrand.pale kuna bulb inauzwa elfu 20 ambazo kariakoo unapata kwa elfu 3.ila toka tuzifunge huu ni mwaka wa 6 bulb haijawai kungua hata moja.

Ukiona bei zipo juu kuliko uwezo wa mfuko wako basi nenda tronic(kisutu) pale napo utapata taa za kila aina zenye kudumu muda mrefu.
Achana na mataa ya kariakoo
 
PSFLOT_33938f63-a177-4c0d-8caa-afd51f607e71_740x.jpg

Hii inaitwa float switch(marufu kama Boya) hii kazi yake kubwa ufungwa ndani ya tank la maji ili yanapokaribia kujaa pump iweze kujizima isipandishe tena maji, na pia maji yanapokaribia kuisha boya ufanya pump iwake ili ipandishe maji kwenye tank.
Mafundi wengi uwa wanaunga Boya na umeme kwa kutokujua kuwa Boya limetengenezwa na mwanadamu,linaweza kwa bahati mbaya likapitisha maji ndani umeme ukawa upo kwenye maji, mtu akatoka zake huko anataka kuoga anafungua maji anapigwa shoti.
Kwa kuzingatia usalama fundi anataikwa kutumia contactor katika ufungaji wa Boya ili kumlinda mtumiaji.Contactor itapeleka signal tu kwenye Boya na sio umeme.umeme utaishia kwenye contactor na contactor inakuwa inaruhusu pump iwake na kuzima.
 
Ujirani mwema huwa unaanzia mbali

Kama unajenga nyumba yako, na unaona pia kuna mwenzako pembeni nae anajenga nyumba yake, anzeni kuazimana vitu kama ngazi, sijui mpira wa maji n.k

Inasaidia sana kuokoa gharama zisizo za lazima lakini pia inatengeneza ujirani mzuri baina yenu kabla hata hamjahamia kwenye nyumba zenu.

Kama mmeshindwa hata kuazimana vitu wakati wa ujenzi, kwamba kila mtu anaamua ajenge tu kivyake basi hata mkihamia ujirani wenu utakuwa ni ujirani wa salamu tu kitu ambacho sio kizuri.

Jirani ukiishi nae vizuri, anaweza akawa kama ndugu yako wa damu. Siku umepata tatizo, iwe ni kuugua au msiba nk yeye ndio anakuwa wa kwanza kukusaidia kabla ndugu zako walio mbali hawajafika.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Msingi wastan kozi ngapi
Kama kiwanja kiko flat, idadi itategemea na urefu wa msingi unaoutaka mfano mwingine anaweza akajenga kozi 7 (kozi 4 chini ya ardhi, kozi 3 juu ya ardhi) lakini mwingine anaweza akaweka zaidi ya kazi 7 ili msingi uwe juu zaidi

Kama kiwanja kina slope, level ya juu ya kiwanja ndio itakayokupa jibu ujenge kozi ngapi japo kuta zake huwa zinajengwa kwa step tofauti na ujenzi katika kiwanja ambacho ni flat.
Wengine huamua kukata kifusi sehemu ya kiwanja ambayo iko juu, na kukijaza hicho kifusi katika sehemu ya kiwanja ambayo ina bonde ili kiwanja kiwe flat. Ukiwa unaenda Segerea kupitia njia ya Malamba Mawili utaona huo ujenzi kule milimani
 
Back
Top Bottom