Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Hechy Essy

JF-Expert Member
Mar 30, 2023
328
954
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
20230705_154914.jpg
 
Wakati mwingine sio lazima sana kuchukua vifaa vyote vya ujenzi vikiwa ktk hali yake ya uzima mfano unapoenda kununua tiles, unanunua box za tiles ambazo ni nzima na ukifika site tiles zingine unazikata ili upate vipande vya kujazia na wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa

Hii pia unaweza ukaapply kwenye gympsum board ktk uwekaji wa dari, tofali n.k kwa lengo la lengo kupunguza gharama

Kabla ya kufanya uamuzi inabidi ufanye mahesabu ili upate makisio kwamba nyumba yako itahitaji vitu vizima vingapi, ili uweze kujua sehemu iliyobaki itahitaji kiasi gani cha material ambazo sio nzima (hapa simaanishi ubovu, namaanisha utimilifu)
 
Nime ichukua hii

.
 
Rekebisha hizo vent za huko kwenye paa, hazina kazi yoyote zaidi ya kuozesha ceiling board
Hizo kazi yake ni kuruhusu mzunguko wa hewa ambapo kama usipoweka, lile joto la hewa iliyopo kati ya paa na dari kipindi jua linawaka inasababisha hewa kuwa na pressure ambayo inaenda kusukuma mikanda ya pembeni ya dari na gympsum board na kusababisha mipasuko ktk maungio
 
Wakati mwingine design inaweza kuchangia ongezeko la gharama za ujenzi mfano unaweza ukakuta chumba kina urefu wa mita 3.7 kwa upana wa mita 4.3 ambapo ukija kwenye kazi kama za tiles, gympsum n.k unabaki na wastage (vipande visivyotumika) nyingi wakati kama chumba hicho hicho kingekuwa na urefu wa mita 3.6 kwa upana wa mita 4.2 au 3.9 ungepunguza hii wastage na kuokoa gharama

Nikitolea mfano wa tiles, tiles zipo za 30cmx30cm, 40cmx40cm,50cmx50cm n.k

Mita 3.6 inagawanyika kwa 30cm au 40cm bila kubaki lakini mita 3.7 inagawanyika kwa 30cm na kubaki 10cm hivyo itakulazimu ukate vipande ili uweze kujazia hizo sehemu zilizobakia. Ni vyema ktk designing ukazingatia vitu kama hivi ili mwisho wa siku usiingie gharama zisizo na ulazima
 
Ila mkuu na wewe siku nyingine tumia tafsiri ya vipimo kama fundi kweli! Utasemaje urefu unakuwa mdogo kuliko upana? Inakuwaje 3.7m unaita urefu na 4.3m unaita upana?
 
Plaster nzuri ni ile ambayo ukimwagia ukuta maji, ukuta unakauka bila kuchora alama za matofali. Kiujumla michoro ya tofali katika ukuta uliopigwa plaster hutokea pale ratio ya udongo uliotumika kujengea tofali ni kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kupigia plaster

Kitaalam udongo wa kujengea tofali tunatumia ratio ya 1:6 na udongo wa kupigia plaster tunatumia ratio ya 1:4 na 1:5 (ratio ya 1:4 inatumika kwenye kuta upande wa nje, na 1:5 upande wa ndani)

Ratio ya plaster inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kujengea

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
 
Moja ya mbinu za kupunguza gharama katika ujengaji wa msingi ni kutumia tofali za nchi 6 badala ya tofali za nchi 5

Kwa kuwa katika msingi tofali zake huwa zinalazwa hivyo ukitumia tofali za nchi 6 utajenga mistari michache tofauti na ukitumia tofali za nchi 5

Tuchukulie mfano msingi wako una mita 1.4 (beam excluded) (nimechukua 1.4m kwa sababu inagawanyika kwa 175mm na 200mm bila kubaki, kiuhalisia nyumba za kawaida msingi huwa ni futi 2 mpaka 3 au na zaidi kutegemeana na slope ya eneo)

Kama utatumia tofali za nchi 6 utajenga mistari 7 (150mm ya tofali + 50mm ya udongo =200mm)

Na kama utatumia tofali za nchi 5 utajenga mistari 8 (125mm ya tofali + 50mm ya udongo= 175mm)

Kama kila kozi moja inachukua tofali 50, upande wa tofali za nchi 6 itakuwa 50x7×1100 = Tsh 385,000/=

Kama kila kozi moja inachukua tofali 50, upande wa tofali za nchi 5 itakuwa 50x8×1000 = Tsh 400,000/=

NB: Unene wa udongo nimechukua 50mm ili mahesabu yawe rahisi

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya gharama za ujenzi na vifaa tuwasiliane
 
Namba ya simu kiongozi
 
Baada ya kupanga mawe (hardcore) katika msingi, inashauriwa umwage mchanga mwingi ndipo uje umwage zege la jamvi (oversite concrete). Hii ni kwa sababu unapopanga mawe, ile nafasi iliyopo kati ya jiwe na jiwe zege inaweza isipite kwenda kuziba hizo nafasi. Kama hiyo sakafu itapata mgandamzo mkubwa (mfano gari ikapita) inaweza kusababisha hiyo sakafu kutitia kutokana na uwepo wa uwazi (matundu) uliopo chini yake

Kama unahitaji ramani za kitaalamu na makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)

Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Hii nyumba ni kwa ajili ya maeneo yenye slope au foundation inapandishwa juu hata kwenye tambarare ili zipatikane hizo ngazi?
 
Popote tu (iwe flat au slope) unajenga mkuu, kitaalamu floor ya nyumba inatakiwa iwe angalau futi moja na nusu kutokea usawa wa ardhi, hii itasaidia hata maji ya mvua yanapotiririka ardhini yasiweze kuingia katika nyumba kupitia milangoni
 
Ni muhimu sana kuacha matundu katika kuta za msingi ili kuruhusu ardhi ipumue na kuzuia nyufa zitokanazo na joto kali lililopo chini ya ardhi. Matundu yasiwekwe katika usawa mmoja, weka katika level mbili yaani chini na juu katika kila umbali wa mita moja mpaka mita moja na nusu kati ya tundu na tundu kuzunguka kuta. Kwa kuwa joto huwa linaongezeka zaidi kadri unavyoenda chini, basi weka matundu mawili chini, tundu moja juu kwa kufatana kuzunguka kuta
 
Kabla ya kumwaga zege, ni vizuri kupamwagia maji sehemu ambapo unataka kumwaga hiyo zege ili maji yaliyopo kwenye zege yasifyozwe na kusababisha kasi ya reaction kati ya cement na maji (hydration) kupungua na kufanya zege isifikie ule uwezo wake halisi wa kubeba mzigo
 
Back
Top Bottom