Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Ujenzi una hatua zake, na hatua zingine zinatakiwa zitangulie kabla ya zingine. Ukivuruga mpangilio ujue lazima utaingia gharama ya ziada huko mbeleni

Mfano unakuta mtu ameanza kupigilia mbao za dari wakati bado hajapachika bomba za umeme ukutani, baadae akitaka kuweka hizo bomba anaanza kufumua mbao za pembeni ili apitishe bomba.

Ikumbukwe kwamba fundi ukimuita site, yeye atafanya kazi yake husika na hawezi kukuambia kwamba inabidi fundi wa tasnia flani ndio anatakiwa aanze kabla yake kwa kuhofia kuzungukwa na fundi mwenzake na kukosa hiyo kazi kwahivyo wewe mwenye kazi (boss) ndio unatakiwa ujue ikitoka hatua hii inafuata hatua gani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Elimu bora kabisa hii
 
Hizo kazi yake ni kuruhusu mzunguko wa hewa ambapo kama usipoweka, lile joto la hewa iliyopo kati ya paa na dari kipindi jua linawaka inasababisha hewa kuwa na pressure ambayo inaenda kusukuma mikanda ya pembeni ya dari na gympsum board na kusababisha mipasuko ktk maungio
sawa lakini siyo sahihi unaweza kufanya nyumba iwe ndefu na madirisha makubwa kwhaiyo mzunguko wa hewa ukawa poa kabisa , pia siku hizi mamikanda ni old fashion ni mwendo wa plan tu. bytheway mie siku nashauri FLAT ROOFING .
 
Sio mzunguko wa hewa ndani ya nyumba, ni mzunguko wa hewa juu ya dari. Mafundi umeme wanaelewa vizuri joto lake wakiwa wanafanya marekebisho huko juu
 
Umejitahidi kujieleza vizuri, hizi contemporary house unajenga?naona nyingi zinavuja
 
Sio mzunguko wa hewa ndani ya nyumba, ni mzunguko wa hewa juu ya dari. Mafundi umeme wanaelewa vizuri joto lake wakiwa wanafanya marekebisho huko ju

Sio mzunguko wa hewa ndani ya nyumba, ni mzunguko wa hewa juu ya dari. Mafundi umeme wanaelewa vizuri joto lake wakiwa wanafanya marekebisho huko juu
Oooh hilo sasa siyo issue maana mafundi umeme siku hizi wako vizuri wakipita juu ya dari wamepita pia nikuweka ventillation tu
 
Mwisho wa siku uamuzi utabaki kwa mwenye nyumba, aweke ama asiweke. Hiyo sijasema kwamba inawekwa kwa ajili ya mafundi umeme, nilitolea mfano wa mtu wa kumuuliza hali ya joto iliyopo huko juu
 
Ujenzi wa sakafu ya choo/bafu unatakiwa uzingatie drainage ya maji kwa maana hata ikitokea ukachukua ndoo ya maji ukamwaga mlangoni, maji yote yaende kudumbukia kwenye sink la choo bila kuacha vidimbwi pembeni. Hii itasaidia choo chako kuwa kikavu muda wote, na pia itakupunguzia kazi ya kufagia maji kuyaelekeza kwenye sink kila unapoenda kukitumia choo chako.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Hivi sakafu tambarale ama sakafu mwinamo kidogo ipi ni Bora? Kwa maana baadhi ya mafundi seremala husema sakafu mwinamo husababisha mlango uburuze sakafuni.

Mlango kuburuza sakafuni chanzo ni sakafu mwinamo ama ni nini?
 
Slope inayowekwa hapo ni ndogo mno kiasi kwamba huwezi kuiona kwa macho, hata wakati wa kuset inatakiwa ile bubble ya pima maji isitoke yote ktk chumba chake cha kati. Inatakiwa ivuke mstari kidogo sana

Kama mlango mwanzo ulikuwa unafunguka vizuri bila shida, then baadae ndio ukawa unakwama kwama shida inakuwa sio floor tena. Inaweza kuwa labda bawaba zimelegea na kufanya mlango ushuke chini au fremu ya mlango imetitia chini
 
Ulinzi wa nyumba kupitia madirisha unaimarishwa na pattern ya grill zako. Dirisha za aluminium (vioo) zinazuia tu baridi na vumbi, kwa sababu kama mtu amedhamiria kabisa kuiba anaweza akapasua kioo kwa nyundo au jiwe.

Hakikisha pattern ya grill zako utakayochagua iwe ni complex kidogo, sio mtu akipachua point mbili tu tayari ameshapata upenyo wa kuingia ndani.

Mwizi kawaida huwa anacheza na hesabu za muda, akiona dirisha lako ni rahisi kupachua let say atatumia labda dakika moja au mbili kupachua, basi ni rahisi kufanya maamuzi ya kupachua na kuingia tofauti na angekutana na dirisha lenye pattern ngumu ambapo atahofia kutumia muda mwingi na kukutwa akiwa bado hajafanikisha dhamira yake.

Upo sahihi kabisa
 
Kabla ya kupiga ripu kuta zako, hakikisha kwanza kuta zako kama zimenyooka au lah. Usije ukaweka tu plaster ya unene mmoja kutoka juu mpaka chini wakati kuta zako hazijanyooka, ukifanya hivyo maana yake na plaster nayo itakuwa haijanyooka.

Kama kuta hazinyooka, unene wa plaster hauwezi ukalingana pote. Kuna sehemu za kuta itakuwa na nyama nene, na kuna sehemu za kuta zitakuwa na nyama nyembamba. Hapo ndio unakuwa umenyoosha kuta kwa kutumia plaster.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Uķipita site nyingi, utakutana na hili tatizo la mkanda wa msingi kuwa na level moja nyumba nzima.

Mkanda wa msingi unaopita sehemu ya kibaraza unatakiwa uwe chini kwa kozi moja mfano kama msingi wako umejenga kozi 7, basi sehemu ya kibaraza jenga kozi 6 tu.

Ni bora ukajenga nyumba ya vyumba vitatu ambayo ina sebule na jiko bila dinning room kuliko kuwa na nyumba ya vyumba viwili yenye sebule, jiko na dinning.

Dinning ni sehemu ambayo inatumika muda mchache sana, kwahivyo kama uchumi hauruhusu sio lazima kuwa na dinning (kwa hizo situation mbili hapo juu, ni heri ukaongeza chumba cha kulala ukaskip dining, watu wanaweza wakala hata sebleni).

Wageni kula chakula sebleni na usiku wakapata chumba cha kulala ni bora kuliko wageni wakala chakula dinning lakini usiku wakalala sebleni kutokana na kukosa chumba cha wao kulala.

Ushauli mzuri kabisa huu ubalikiwe sana
 
Uķipita site nyingi, utakutana na hili tatizo la mkanda wa msingi kuwa na level moja nyumba nzima.

Mkanda wa msingi unaopita sehemu ya kibaraza unatakiwa uwe chini kwa kozi moja mfano kama msingi wako umejenga kozi 7, basi sehemu ya kibaraza jenga kozi 6 tu.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Habari picha
20260331_074558.jpg
 
Katika ujenzi wa boma, pambana zaidi kunyoosha kozi ya kwanza maana kozi zote zinazofuata juu zinaifuata kozi ya kwanza na ndio maana utaona kozi ya kwanza huwa inasetiwa kwa kufunga kamba mbili (chini na juu ya tofali). Baada ya hapo kazi inakuwa nyepesi kwa kozi zinazofuata, sio tena fundi ahangaike kushusha kobilo mpaka kwenye msingi katika kila kozi anayojenga.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukienda mahali kununua kiwanja, na ukakuta kuna viwanja vingi, kama mfuko unaruhusu usinunue kiwanja kimoja (nunua hata viwili, vitatu n.k)

Viwanja vingine utakavyonunua (ukiachana na hicho ambacho utategemea kujenga nyumba yako), baadae vitakuwa kama visiwa kwa maana maeneo mengine yote katika huo mtaa yatakuwa yameshajengwa nyumba.

Kwa kuwa mji utakuwa umeshakua mkubwa, wahitaji wa viwanja katika hilo eneo watakuwa ni wengi kwahivyo madalali watakuwa wanakuja kukugongea hodi kila siku. Hapo sasa bei unapanga wewe kwa kuwa wao ndio wanaokutafuta, kiwanja ulichonunua milioni 2 sasa hivi usishangae thamani yake ikafika milion 30 au zaidi baada ya miaka 10 mbele

Back
Top Bottom