Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Kama ulinunuaga kiwanja kipindi ambacho hakuna mvua, basi na mvua hizi ndio muda mzuri wa kwenda kuangalia hali ya kiwanja chako jinsi kinavyokuwa kabla hujaanza ujenzi huko mbeleni

Na kama bado hujanunua kiwanja, basi muda mzuri wa kwenda na dalali kuangalia hicho kiwanja ni kipindi hiki cha mvua maana wengi huwa wanakuja kugundua kuwa kiwanja kinajaa maji baada ya kujenga na kuhamia.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ni hatari sana kujenga choo juu ya karo la maji taka kwa lengo la kuokoa eneo katika kiwanja. Kumekuwa na matukio mengi ya vyoo kuanguka ghafla kutokana na uzito uliobebeshwa juu ya karo.

Tofali zikikaa sana kwenye maji huwa zinachoka haraka kwa kuwa zinafyonza sana maji tofauti na mawe ndio maana wengine huwa wanapiga plaster kisha wanapaka nilu (cement paste) ili kuzuia tofali zisifyonze maji.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Nisaidie hili mkuu, nahitaji kuweka tank la maji litre 5,000 juu ya slab ya veranda ya jiko, niijengeje slab hiyo ili iwe na uwezo wa kubeba tank la uzito huo?
 
Lita 5000 ni nyingi ndg (kwa uzito ni sawa na tani 5), sikushauri uweke tank la huo ujazo katika slab ya kibaraza, hapo ni bora ukajenga mnara wa tank pembeni. Sehemu ya uzito wa slab ya kibaraza huwa inabebwa na kuta za nyumba ambazo tofali zake zimejengwa kwa kusimamishwa kwahivyo kuhimili uzito mkubwa kiasi hicho ni changamoto

Jenga mnara wa nguzo nne, na pia tumia nondo za milimita 16 katika nguzo
 
Nyumba ndogo lakini kwa familia kubwa (viwanja vidogo)

Sebule (Sitting room) 1
Jiko (Kitchen) 1
Chumba na choo (self room) 2
Chumba bila choo (single room) 1
Choo bafu cha jumuiya (public toilet) 1
Vibaraza viwili (mbele na nyuma)

Ukubwa wa nyumba mita 11 kwa mita 12
2B.PNG
 
Watu wengi wanatumia feni kipindi cha joto tu, hawajui kwamba wanaweza wakaitumia pia hata katika kipindi cha baridi.

Katika feni kuna switch ndogo ambayo unaweza ukabadilisha uelekeo wa mzunguko wa feni (feni ikawa inaenda reverse). Hii itaifanya feni iwe inavuta juu hewa ya baridi iliyopo chini, na kushusha chini hewa ya joto (warm air) iliyopo juu ya feni.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
mkuu nahitaji kujenga mnara wa tank lenye ujazo wa Lita 3000, ila chini nipate small laundry room na choo cha nje. Naomba msaada nisije nkakosea uzito wa tank likiwa na maji likaangusha Kuta?
 
Watu wengi wanatumia feni kipindi cha joto tu, hawajui kwamba wanaweza wakaitumia pia hata katika kipindi cha baridi.

Katika feni kuna switch ndogo ambayo unaweza ukabadilisha uelekeo wa mzunguko wa feni (feni ikawa inaenda reverse). Hii itaifanya feni iwe inavuta juu hewa ya baridi iliyopo chini, na kushusha chini hewa ya joto (warm air) iliyopo juu ya feni.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Yahusu Beam ya barazani.

Naomba ufafanuzi juu ya namna bora ya ku-set beam ya veranda. Je, ni sahihi ku-set beam hiyo kwa usawa wa beam ya milango na madirisha?. Nimekuwa nikiona kwenye majengo mengi beam ya veranda inakuwa kama ipo kwa juu kidogo kutoka usawa wa beam ya kawaida na kama ndiyo hivyo, huwa wanapandisha beam ya veranda max na min kozi ngapi kutoka kwenye usawa wa beam ya kawaida?.

NB: Beam ya veranda iwe T shaped na siyo zile zenye urembo wa U shape na namna nyingine.
 
Ungekuwa na picha yake ingekuwa vizuri zaidi ila nitaelezea hivyo hivyo kwa jinsi nikivyoyaelewa maelezo yako.

Kawaida mkanda wa juu wote unatakiwa uwe level moja, ila kama kutakuwa na ulazima wa portion ya mkanda iwe katika level tofauti basi ni vyema hiyo portion ikawa inabebwa na nguzo na sio kulala tena juu ya tofali kwa sababu nondo zake zitakosa mahali pa kufanyia termination.

Baadhi ya mafundi huwa wanapandisha mkanda wa kibaraza kwa lengo la kuongeza height hasa nyumba inapokuwa fupi (mfano nyumba ikawa ina kozi 10 kutoka mkanda wa chini na mkanda wa juu)
 
Picha ya kwanza. Mkanda level moja
20260420_155955.jpg

Picha ya pili. Mkanda wa veranda upo juu ya mkanda wa dirisha.
20260420_160022.jpg

Kwahiyo hapo kwenye ukuta ambako mkanda wa veranda umelalia ndiyo panatakiwa kuwa na column?.
 
Picha ya kwanza. Mkanda level moja View attachment 3575961

Picha ya pili. Mkanda wa veranda upo juu ya mkanda wa dirisha. View attachment 3575962
Kwahiyo hapo kwenye ukuta ambako mkanda wa veranda umelalia ndiyo panatakiwa kuwa na column?.
Yah, lakini ni vizuri kama mtu anataka height iwe kubwa basi ajenge idadi ya kozi kulingana na urefu anaotaka ili mkanda uwe na level moja nyumba nzima kuliko mikanda kupishana.
 
Kama unaweka ukuta wa gable, zingatia yafuatayo kuhusu mkanda (beam)

1. Idadi ya nondo, katika usukaji wa nondo funga nondo nne (chini nondo mbili na juu nondo mbili)

2. Hakikisha mkanda wako wa juu una depth ya kutosha kubeba huo mzigo unaokaa juu yake (minimum isipungue nchi 8 sawa na 20cm)

3. Punguza nafasi kati ya ringi moja na ringi nyingine, angalau isizidi sentimita 20. Ukiwa unapima urefu wa mkanda, pima pia na umbali wa mlango/dirisha lilipo ili kipande cha beam kilichokaa usawa wa dirisha/mlango uweke ringi zako karibu karibu.

4. Ratio ya zege, zingatia uwiano wa cement mchanga na kokoto katika uchanganyaji wa zege. Minimum isipungue grade 15 (1:3:6)

5. Size ya ringi, size ya ringi inatakiwa iwe na ukubwa sawa na ukubwa wa mkanda kutoa nchi 2 ili utakapofungua box zako, nondo ziwe zimemezwa ndani ya zege. Mfano kama mkanda wako una size ya nchi 6 kwa nchi 8 (6x8), basi ringi zako utakazotumia zinatakiwa ziwe 4x6.

Pia unaweza ukayazingatia hayo yote hata kama hutoweka ukuta wa Gable

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane, siku ya May Mosi kutakuwa na ofa ya punguzo la bei kwa asilimia 5.1
 
MKuu ofa ya May Mosi ni Ramani, Makadirio au Ushauri?
 
Vp kiongozi kwenye kutengeneza mnala wa tank la maji lenye vyoo chini ipi njia ya kuokoa garama kati ya kujenga kwa tofali za kulala mpaka juu au kwa kutumia nguzo za zege mpaka juu bila kulaza matofali
 
Hapo inategemea na ujazo wa tank lenyewe lakini pia na ardhi yako jinsi ilivyo.
Yote kwa yote hata kama utalaza tofali, ni muhimu pia ukaweka na nguzo kuongeza uimara maana tofali za siku hizi sio za kuziamini sana (zinatengenezwa kibiashara zaidi tofauti na tofali za miaka ya nyuma)
 
Uwazi wa dirisha la choo/bafu unatakiwa uanze baada ya kozi ya saba au juu ya hapo kwa maana kama umejenga kozi 10 kutoka mkanda wa chini hadi mkanda wa juu basi dirisha litakuwa likae katika kozi ya 8, 9 na 10.

Kama utahitaji kuweka dirisha refu zaidi, itabidi uongeze idadi ya kozi kutoka mkanda hadi mkanda mfano unaweza ukajenga kozi 11, dirisha likakaa katika kozi ya 8,9,10 na 11 au ukajenga kozi 12 dirisha likakaa katika kozi ya 9, 10, 11 na 12

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Lita 5000 ni nyingi ndg (kwa uzito ni sawa na tani 5), sikushauri uweke tank la huo ujazo katika slab ya kibaraza, hapo ni bora ukajenga mnara wa tank pembeni. Sehemu ya uzito wa slab ya kibaraza huwa inabebwa na kuta za nyumba ambazo tofali zake zimejengwa kwa kusimamishwa kwahivyo kuhimili uzito mkubwa kiasi hicho ni changamoto

Jenga mnara wa nguzo nne, na pia tumia nondo za milimita 16 katika nguzo
Mimi nimeweka nguzo tatu za nondo za mm16 upande mwingine umebebwa na ukuta, slab ya kibaraza upande wa jiko. Zege inch 6, hapo naweza kuweka tank la lita ngapi?
 
Na kwenye slab nondo zake zimesukwaje? Kichanja kimoja au vichanja viwili?
 
Back
Top Bottom